Madhara ya dhambi ya uzinzi

Madhara ya dhambi ya uzinzi

Dhambi ya uzinzi inahesabika pale mtu alipolala na mke wa mtu na sio vinginevyo. Ikimaanisha kuwa adhabu ilitolewa kwa mke aliyechepuka na kama angekamatwa na mwanamume huyo wangeuwawa wote wawili. Ila kwa mwanamume kutembea na binti hata kama ameoa sheria haiwi uzinzi hivyo ni kusema aliyefungwa ni mke aliyeolewa huyu hapaswi kuingiliwa kamwe na ukimwingilia ndipo Methali inakuita wewe ( mwanamume) mjinga usiye na akili kwa ni ni? Maana umekosa wanawake mpaka ukaenda kujitia unajisi kwenye shahawa za mwanamume mwenzako?. Inaendelea kusema.....
Mithali 6
33. Atapata jeraha na kuvunjiwa heshima; <br>Wala fedheha yake haitafutika.
34. Maana wivu ni ghadhabu ya mtu; <br>Wala hatahurumia siku ya kujilipiza kisasi.
35. Hatakubali ukombozi uwao wote; <br>Wala hatakuwa radhi, ujapomlipa vitu vingi.
Yaani hata kufirwa inakuwa haki yako ukiingilia mke wa mtu.

Ila kuhusiana na mwanamwali ukimuingilia ukadakwa waweza toa mahari akawa mkeo au ikiwa baba mzazi haridhii umuoe itatoa mahari kisha ataenda zake. Hii ni kibiblia kabisa
Duh!... Hii ni tafsiri mpya ya Uzinzi....

Rabbon Yesu Anakuja
 
umeongea vyema sana mkuu,
uzinzi na uasherati unaweza ushinda kwa namna nyingi
kwanza kubali kuwa ni kosa,
jiepushe na pombe, jiepushe na miziki ya kidunia, movies na tamthiliya , mitandao isiyo ya kimaadili kama tik tok na instgram, fanya mazoezi, jaribu kuchuja aina ya taarifa ambazo unazipokea,epuka vyakula vya wanga, fanya mazoezi na zaidi concentrate katika kujifunza stadi mpya ambazo zitakuingizia kipato yote kwa yote zingatia ibada

Ndipo niliposema, Ole wangu! Kwa maana nimepotea; kwa sababu mimi ni mtu mwenye midomo michafu, nami ninakaa kati ya watu wenye midomo michafu; na macho yangu yamemwona Mfalme, BWANA wa majeshi...

Mungu atusaidie 🙏
 
sadaka haimunufaishi Mchungaji inakunufaisha ww mtoaji, ndo maana hta mchungaji haitumiii bali inatumika kwa ajili ya kueneza injili ili iwafikie watu wengi zaidi, hata ww ukienda kwa mganga ukatoa kuku unadhan hyo kuku ni kwa ajili ya mganga, ni kwa ajili yako
Hapa umedqnganya
 
Yesu Kristo alikufa kwa ajili gani?
asante kwa swali zuri nitakuelezea kwa msaada wa MUNGU
Mungu alipomuumba adamu na Hawa ,alimpa mamlaka ya kutawala , kuongezeka na kukua zaidi,
na huu ndo ulikuwa urithi wa vizazi vyote, inamaana binadamu alikuwa na acess ya moja kwa moja na Mungu, dhambi ilipoingia kupitia wazazi wetu wa mwanzo, ile nguvu ambayo walipewa iliisha au ilipotea, Mungu aliahidi au aliweka agano kuwa ile nguvu ya kutiisha, utawala na mamlaka angeirejesha kwa wanadamu, kumbuka kila binadamu anayezaliwa anazaliwa chini ya laana, hivyo Mungu alimtoa mwana wa pekee ambaye ni YESU( Hii ndo Neema ) ili aje aishi maisha ya duniani, kwa mfano wa mwa ,mwandamu, ili kila binadamu amwamini YEYE ili kurejesha nguvu ya asili ambayo tuliporwa na shetani, hivyo ukimwamini Yesu umeyapata yote
 
Hakuna kitu kinaitwa uzinzi au uasherati , huo ni ustaarabu wetu sisi binadamu tu ili kujitofautisha na wanyama wengine .

Huyo mungu mnaedaiwa yupo angekua anachukia uzinzi sana, angefanya mimba ishike kwa wana ndoa tu , kama unaweza lala na mke wa mtu akashika mimba ndio ujue hakuna tofauti yoyote na mnyama zaidi ya ustaarabu tu .


Na haya majina ya uzinzi na uasherati ni sisi wenyewe tumeyatengeneza tu ili kuulinda ustaarabu kama binadamu tu.
 
Nimekaa muda mrefu bila kufanya mapenzi

Nilichokuja kugundua ukisipo fanya mapenzi muda mrefu akili yako kuna time kama ina sizi hivi ata huwe mtu wa mazoezi kiasi gaji hili swala halikwepeki mkuu
Nimemaliza mwaka jana wote now natafuta mwaka wa pili mbona nipo kawaida tu ? Ni kujiendekeza tu .
 
Lini Mungu aliteua kanisa ? Kila mtu anajua kanisa Africa ulikua mpango kabambe wakuja kama kitangulizi cha wakoloni kwa ajili ya kutunyonya yaani wamisionari wa kikoloni . Wewe unavyosema mpango wa Mungu kivip na Mungu yupi na lini na ulijuaje?
sio kweli, wacha nikuelezee kidogo hapa, kwa mifano
Watu wa Afrika Kaskazini walisafiri na kukaa pia katika miji ya Ulaya na Asia. Kutokana na mawasiliano mazuri tunaona Waafrika mbalimbali katika taarifa za Biblia Tuone mifano: - Yesu alipobeba msalaba wake kule Yerusalemu akaanguka chini. Maaskari wakamkamata mtu aliyepita mtaani jina lake ni Simoni wa Kurene. Jina linaonyesha ya kwamba alikuwa mgeni kutoka Kurene (Libia). (Lk 23:26) - wakati wa ushirika wa kwanza kule Yerusalemu, Filipo mwinjilisti alikutana na msafiri kutoka Kushi akambatiza. Kushi ni jina la kale la sehemu ya Sudan Kusini ya leo ,matoleo mengine ya Biblia hutafsiri: Mhabeshi au Mwethopia). (Mdo 8:26 n.k.). - katika ushirika wa mji mkubwa wa Antiokia (Asia Magharibi) tunasikia juu ya watu wa asili ya Afrika waliokuwa viongozi wa ushirika huo. Mmoja ni Lukio Mkurene. Mwingine ni "Simeoni aitwaye Nigeri". Neno "Nigeri" linatafsiriwa "Mweusi". Kumbe hata huyu anaonekana ametokea Afrika kutokana na rangi yake. (Mdo 13)
 
Vipi sadaka za mtu alie zaliwa kwa hicho mnachokiita uzinzi mnachukua?
pesa na dhahabu ni mali za Bwana,..ila dhambi ni zako mwenyewe,....karibu ibadani ukiwa na sadaka yako mkononi..
 
Hongera, mimi nimeshindwa
unaweza mkuu, kama unataka kufanikiwa kiuchumi na kijamii anza kushughulikia na hili jambo,hujawahi kuwaza kwann dunia inapambana sana kuhamasisha uzinzi kuliko ndoa? unapigwa bila ww kujua , simama imara
 
Uzinzi na uasherati ni dhana zinazohusiana na mwenendo wa kimaadili, hasa katika muktadha wa dini na jamii, zinazorejelea tabia zisizokubalika za kingono.

1. Uzinzi: Huu ni tendo la kushiriki mahusiano ya kimapenzi au kingono na mtu ambaye si mume au mke wa ndoa. Uzinzi kwa kawaida huchukuliwa kuwa dhambi au kosa kubwa katika dini na tamaduni nyingi kwa sababu huvunja ahadi za uaminifu ndani ya ndoa.


2. Uasherati: Hili linarejelea mahusiano ya kingono nje ya ndoa au kabla ya ndoa. Ni neno pana zaidi linalojumuisha tabia za kingono zinazochukuliwa kuwa zisizo za maadili, kama vile ngono ya kiholela, uzinzi, au vitendo vingine vinavyokiuka maadili ya kidini au kijamii.



Kwa ujumla, dhana hizi mbili zinahusiana na kanuni za kijamii, kidini, na maadili zinazokusudia kuimarisha heshima, uaminifu, na utakatifu wa mahusiano ya kibinadamu.
 
unaweza mkuu, kama unataka kufanikiwa kiuchumi na kijamii anza kushughulikia na hili jambo,hujawahi kuwaza kwann dunia inapambana sana kuhamasisha uzinzi kuliko ndoa? unapigwa bila ww kujua , simama imara
Nitaoa mkuu,mambo yanakaa poa soon tu
 
Punyeto, kwa lugha ya Kiswahili, ni tendo la kujiridhisha kimwili au kingono kwa kutumia mikono au njia nyingine bila kushirikisha mtu mwingine. Hili ni tendo linalojulikana pia kama masturbation kwa Kiingereza.

Muktadha wa Punyeto:

1. Kimaadili na Kidini:

Katika baadhi ya dini na jamii, punyeto huchukuliwa kama tendo lisilofaa na mara nyingine huonwa kuwa dhambi.

Inahusishwa na mitazamo ya kimaadili, ambapo jamii fulani huliona kama kikwazo cha maendeleo ya kiroho au kinachopotosha akili.



2. Kitaalam:

Wataalam wa afya wanasema kwamba, kwa kiasi fulani, punyeto si hatari kwa afya ya kimwili au kiakili kwa watu wengi. Inaweza pia kusaidia kupunguza msongo wa mawazo.

Hata hivyo, iwapo inafanyika kupita kiasi au kuathiri maisha ya kawaida, inaweza kupelekea madhara kama vile utegemezi wa kingono au hisia za hatia.



3. Mitazamo ya Kijamii:

Jamii tofauti zina mitazamo mbalimbali kuhusu punyeto, huku baadhi zikiliona kama jambo la kawaida na nyingine zikiendekeza unyanyapaa dhidi yake.




Kwa hivyo, mitazamo juu ya punyeto hutegemea sana imani za kidini, tamaduni, na maoni ya mtu binafsi.
 
Back
Top Bottom