Infinite_Kiumeni
JF-Expert Member
- Jan 23, 2023
- 382
- 687
Wakati unajifunza kutongoza unaweza danganya. Utadanganya kwa vile vitu vinavyokufanya uonekane una thamani. Nyumba, pesa, gari au unajuana na watu wakubwa.
Lakini haina maana ndo ukalie njia hiyo hiyo miaka yote. Ni muhimu ujifunze kumvutia na kumtunza mwanamke kwa mfumo unaosema ukweli na unaomfanya mwanamke akutake zaidi ye mwenyewe.
Hizi ni baadhi ya sababu kwanini usitegemee mfumo wa kudanganya kwenye kumvutia mwanamke.
Ni mfumo dhaifu.
Ni njia rahisi na ya haraka kumpata mwanamke. Lakini haina misingi mizuri.
Haina matokeo kwa muda mrefu. Hata maneno yako yanakua hayatoki moyoni.
Utapata urahisi kwa wanawake wasio na uzoefu wa wanaume, ila wale wenye uzoefu wataona uongo wako. Ni heri ujifunze kumvutia mwanamke bila kumdanganya kuliko kudanganya na kutumia muda mwingi kukumbuka uongo/ kukwepa uongo.
Utajisikia ushindi zaidi kwa kumpata mwanamke bila kumdanganya. Na utapa kujiamini zaidi.
Inaharibu mahusiano ya muda mrefu
Kwa mapenzi ya haraka haraka uongo utakusaidia. Lakini mahusiano ya muda mrefu atagundua tu ulipodanganya.
Ataona maisha yenu yote mliyoishi ni uongo. Na hatakua na haja ya kuendelea kuishi kwenye uongo. Na itakua ngumu kuweka mipango naye ya maisha. Hivyo, kama unataka mahusiano ya muda mrefu jiepushe na uongo.
Uongo unazaa uongo
Shida kubwa ya uongo ni kuutunza.
Ukisema uongo mmoja, inabidi uufiche na uongo mwingine mara mbili. Na uongo uongo marambili inabidi uufiche na uongo mara tatu. Mwisho wa siku unajikuta umejaa uongo.
Kitu kitakachozuia kujenga mahusiano imara kwa muda mrefu. Uongo pia unazaa na kuchochea tabia zingine zisizofaa.
Utavutia waongo wenzako
Ndege wafananao huruka pamoja.
Utajikuta kila mwanamke unayekua naye anakudanganya danganya tu. Kitu kitakachokufanya uamini zaidi kwenye uongo. Na kurudia mzunguko huo huo kwa kila mwanamke unayekua naye.
Cha msingi ni kujiepusha na uongo usio na maana. Na ili kuepuka uongo kirahisi, usijiweke kwenye mazingira yatakaokufanya useme uongo baadaye. Yaani jiepushe na vyanzo vya uongo.
Na hata ukitumia uongo, usiutumie sana kiasi kwamba ukashindwa kujitetea.
Share na Wengine Wapate Kujifunza.