Madhara ya kuzaa nje: Familia inajuta mpaka leo kwa uamuzi walioufanya kwenye urithi wa kaka yao. So sad

Haujatueleza madhara,au ......
 
Kuna uzi nilileta humu, unahusu kuwarithisha mali wake zenu; hii ndio itakuwa suluhisho
Kabisa ndo maana huwa nasema mwanamke kama kaamua kukubali kuwa nyumba ndogo basi apambane na yeye ajenge uchumi wa mwanaye..Maana wengi wa nyumba ndogo huwa wanakubali luwa nyumba ndogo kwa mwanaume anayejiweza kwa kuwa anajua fika atapata mahitaji. Wengi wao wanachukua nafasi hiyo kuwa nikishazaa basi mahitaji pia yataongezeka. Ndo yanakuja kutoa ya kutokea lawama zinakuja kwa mke wa ndoa kuwa anaroho mbaya hataki kutoa urithi kwa watoto wa wenzao.

Sawa ni watoto lkn je wakati anahangaika usiku na mchana kutafuta,,haya bado haitoshi hao watoto ni zao la usaliti je moyo wake unauma kiasi gani.


Wanawake ifike hatua tubadilike.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chukulia mfano,
Wewe na mumeo mnawatoto 4 wakike tupu.
Miaka 20 iliyopita wewe ulimshauri mume wako mununue ekari 4 mbali na mjini. Mume wako akasema sawa ila wewe ukaamua kumchangia mume wako kidogo.
Mkanunua, baadae mkaamua kujenga taratibu nyumba nne pale.

Mlijinyima sana. Wewe kama mke mumeo akiwa mbali huko ulikuwa unasimamia ujenzi na kwenda kununua vifaa , mume anatoa pesa na wewe kidogo unachangia kwenye ujenzi, wakati mwingine hata unabana pesa ya matumizi home ili tuu mjenge.
Nyumba nne zinaisha baada ya miaka kadhaa.
Wewe unajua baadae mabinti zako watagawana pale nyumba moja moja .
Na kadili mji unavyosogea ndipo thamani ya eneo linaongezeka.

Baadae mpo kwenye miaka 30 ya ndoa.
Mume wako anakuja na watoto 2 wa kiume mapacha, wamefanana hatari ni wakubwa kama 20 years.
Afu anakuambia dear sorry nilikuficha.

Mali zenu zipo kwa jina la mume wako. Afu wewe huna ushahidi kuwa umechangia.

Baadae unasikia mumeo anasema watoto wangu wa kiume ndio watarithi mali zangu.
Vipi wewe utakuwa poa ama???
 
Hapo anakuwa amekosea kuwapa zote,ila kugawana moyo wangu nijuavyo ni sawa tu
 
Kwangu watoto wa nje watarithi jasho la Baba yao, jasho langu haliwahusu kamwe....ndo maana naipenda Sheria ya mirathi ya kiislamu.....jasho la mke linatolewa linawekwa Kando kinachobaki kinapigwa pasu, na mke anarithi kwenye Hicho kinachobaki.
Mimi ninavyojua hata mke na mume wakagawana kabla ya mume kufa kulimtu akabeba zake.
Na hamkuachana.
Mama anakuwa na mali zake na Baba anamali zake.
Baba akifa hizo mali za baba watapata watoto wa ndani ya ndoa , wa nje na mke wa ndoa anapata pia kwa kutumia cheti cha ndoa.
Ila mali za mama wa ndoa watoto wa nje hawapati ng'o.

Ndivyo ninavyojua mimi
 
Unao uhakika gani kama Mzee hakupata kisukari sababu ya kutengwa na mkewe na watoto?
 
Hapo anakuwa amekosea kuwapa zote,ila kugawana moyo wangu nijuavyo ni sawa tu
Kuna dada wiki hii alileta uzi kuhusu.
Mume wake kuzaa nje akasema mali zangu mrithi ni huyu wa kiume.
Aliaamua ni kudanga ili kuwajengea watoto wake kwa siri
 
HujapAnga vzr habar yako,
 
Hapo anakuwa amekosea kuwapa zote,ila kugawana moyo wangu nijuavyo ni sawa tu
Sawa unaweza mkafanha hivyo ili its so pain kwa wanawake.
Njia mzuri ni kugawana na mkeo mkeo achukue zake na wewe uchukue zako.
 
Muite chemba mdogo wako, kuna jambo analijua kati yenu familia.
 
[emoji1666]

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 

Acha kutisha watu kwa uoga wako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…