Madhara ya unywaji wa soda kwenye afya ya Binadamu

Madhara ya unywaji wa soda kwenye afya ya Binadamu

hizo ni kwa zinazotengenezwa TZ au dunia nzima?....journalists kuwa scientists, kweli nchi hii ina vituko.
 
Huo ndiyo ukweli wenyewe, tunashukuru kama mambo haya yanaandikwa na kwenye magazeti, hongera kwa wanaozifikia habari hizi na wakaamua kuchukuwa hatua kwa ajili ya familia zao. SODA NI TAKATAKA. Na kwa wasioelewa niwaambie tu HAKUNA SODA NZURI hata kama si nyeusi. Kwa anayetamani soda basi anaweza kutengeneza juisi yake nyumbani (homemade) na akaifurahia kuliko kunywa soda, mbaya zaidi mpaka watoto wa darasa la kwanza mnawapa hizo soda sijuwi mnakitakia nini kizazi hiki.
 

SODA VS UZITO NA UNENE KUPITA KIASI NA MATATIZO MENGINE YALETWAYO NA SODA MWILINI:

kwa mjibu wa utafiti wake, dr.Batmanghelidj, anasema, ingawa soda hazina kalori inayoweza kuainika, zinaweza kuwa kisababisho cha kuongezeka uzito kupita kiasi kwa wale wanaozinywa kwa malengo ya kudhibiti uzito wao.

Kitendawili hiki katika uelewa wetu juu ya uhusiano baina ya unywaji wa vimiminika ambavyo havichangii moja kwa moja uchukuaji wa kalori wa mwili na kuongezeka kwa uzito, kinahitaji ufafanuzi. Kwa mjibu wa utafiti huo, kuna watu wengi waliochukua uamuzi wa kunywa soda ili kudhibiti uzito, lakini matokeo yamekuwa kinyume chake.

Viwanda vya vinywaji vinakuwa kwa kasi kubwa (apace), jarida la The Nation la aprili 27, 1998 liliripoti kuwa, watoto na vijana walio wengi wanakisiwa kunywa mpaka galoni 64 za soda kwa mwaka, kiasi ambacho kiliongezeka mara tatu zaidi tangu mwaka 1978, kikaongezeka mara mbili zaidi kwa mafungu ya umri kati ya miaka 6-11 na kuongezeka kwa robo kwa watoto chini ya miaka 5(chanzo: utafiti, kitengo cha kilimo 1994, marekani).

Inavutia pia kuandika hapa kuwa, kuongezeka huku kwa matumizi ya soda kwa watoto chini ya miaka 5, kuweza kuwa ndiyo sababu ya kuongezeka mara tatu zaidi ya ugonjwa wa pumu (asthma) kwa watoto wa umri huo kati ya mwaka 1980 na 1994.

Utafiti mmoja katika kampasi ya chuo kikuu cha pennsylvania nchini marekani, ulionesha baadhi ya wanafunzi kunywa soda 14 kwa siku, msichana mmoja alitumia soda 37 kwa siku mbili. Wengi wamekiri kuwa hawataweza kuishi bila vinywaji hivi baridi.

Ikiwa vinywaji hivi vitaondolewa sokoni, watu hawa wataonesha dalili zilizosawa na zile zinazowatokea waliokuwa wategemezi kwa madawa mengine ya kulevya.

Jarida la Boys Life, liliwatafiti wasomaji wake na kugunduwa kuwa, asilimia 8 ya wasomaji wake wanakunywa soda 8 au zaidi kwa siku. Viongozi wa kambi moja ya skauti (boy scout jamboree), walikusanya chupa 200,000 tupu za soda kwa ajili ya matumizi mengine (recycling), chama cha vinywaji baridi kimefanya utafiti juu ya matumizi ya vinywaji hivi baridi mahospitalini nchini marekani na kugunduwa zaidi ya asilimia 85 wakihudumia wagonjwa chakula pamoja na vinywaji hivi baridi.

Kwa kiasi kikubwa, imeaminika kuwa vinywaji hivi vinaweza kuwa mubadala wa mahitaji ya mwili kwa maji. Imedhaniwa kuwa, kwa sababu tu vinywaji hivi vina maji, mwili utakuwa umekamilishiwa mahitaji yake ya maji. Dhana hii ni potofu.

Kuongezeka kwa matumizi ya soda zenye kafeina,kunaunda vyanzo vingi vya matatizo ya kiafya kwenye jamii zetu. Imani hii potofu kwamba vimiminika vyote ni sawa na maji kwa mahitaji ya mwili, ndiyo chanzo kikuu cha magonjwa kwa mwili wa binadamu ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa uzito kupita kiasi.

Ili kuielewa dhana hii, inatubidi kutambua baadhi ya kanuni rahisi za kianatomia na kifizioloji za ubongo ambazo huongoza hisia za kula na kunywa.

Umbile kubwa la mwili bila mpangilio kwa kusanyiko la mafuta, ni hatua ya mwanzo ya kuanguka kwa mwili wa binadamu, na kwa mjibu wa maoni ya dr.Batmanghelidj, ni matokeo ya kuchagua kusiko sahihi kwa uchukuaji wa vimiminika. Baadhi ya vinywaji vina madhara zaidi ya vingine.

Kafeina, moja ya vitu mhimu katika soda nyingi, ni dawa ya kulevya!!!.

Hii ndiyo sababu kwa wale waliozoea kunywa chai ya rangi asubuhi wasipokunywa hujisikia kichwa kuuma (they are addicted).

Ina sifa ya kumfanya mtu mtegemezi kwayo sababu ya matendo yake moja kwa moja kwenye ubongo. Inaingilia pia katika ini na kusababisha kuongezeka kwa uzarishaji wa mkojo.

Hivyo, kafeina ni kikojoshi (diuretic).

Kifiziolojia, kafeina ni wakala mkausha maji mwilini. Hii ndiyo sababu mtu analazimika kunywa soda nyingi kwa siku bila kutosheka. Maji hayabaki mwilini kwa muda mrefu.

Wakati huo huo, watu wengi wanajichanganya kwa kutokutambua hisia zao za kiu kwa kudhani kuwa wamekunywa maji ya kutosha toka katika soda, wanajihisi kuwa ni wenye njaa na kuanza kula chakula zaidi ya mahitaji yao ya mwili. Kwa hiyoupungufu wa maji (dehydration) uliosababishwa na vinywaji baridi venye kafeina, kwa muda utasababisha kuongezeka kwa uzitokutokana na kula kupita kiasi ambako ni matokeo ya moja kwa moja ya kushindwa kuzielewa hisia za njaa na kiu.

Kafeina, ni kiamsho (pick-me-up), husisimua ubongo na mwili hata wakati mtu amechoka. Inajionesha kuwa, kafeina hupunguza udhibiti wa stoo ya kwanza ya ubongo (ATP). Hifadhi hii ya kwanza hutumika kwa baadhi ya kazi ambazo kwa kawaida zisingeweza kufikiwa kunapokuwa na usawa uliosawa wa hifadhi hii.

Ikitokea soda imeongezwa sukari, walau baadhi ya mahitaji ya ubongo kwa sukari hufikiwa. Ikiwa kafeina inatoa nguvu toka stoo ya kwanza ya nguvu za ubongo kusaidia ufanyikaji kazi, walau sukari yake itarudishia baadhi ya akiba za stoo ya kwanza hata kama matokeo ya mwisho ni matumizi hasi ya ulalo (deficit) ya stoo ya kwanza kwa ubongo.

Mwanzoni mwa miaka ya 1980, kiongeza utamu cha kutengenezwa (artificial sweetener) kiitwacho 'aspartame', kilianza kutumika kwenye viwanda vya vinywaji baridi. Aspartame ina utamu mara 180 zaidi ya utamu wa sukari ya kawaida, bila nguvu yeyote (kalori) izarishwayo nayo.

Aspartame sasa inatumika kama kitu kisicho na madhara kwa sababu Taasisi ya Madawa (Federal Drug Administration ya marekani) imeitetea (deemed it) kama kitu kisicho na madhara kikitumika kama mubadala wa sukari.

Ndani ya utumbo mdogo, aspartame inabadilishwa kwenda transimita nyurolojia mbili, asidi amino aspartame na phenylalamine, vivyo hivyo methyl alikohol au formaldehyde. Inatetewa kuwa Ini huichukulia methyl alikoholi kuwa si sumu. 'Binafsi nafikiri madai haya hutolewa kunyamazisha sauti zinazopinga biashara za vyakula vilivyotengenezwa viwandani vijulikanavyo kuwa na kemikali hatari kwa binadamu - dr.Batmanghelidj'.

Kafeina huibadilisha Adenosine Triphosphate (ATP) kwenda Adenosine Monophosphate (AMP) ambayo ni nishati iliyokwishatumika (ash) na aspartate huibadilisha GuanosineTriphosphate (GTP) kwenda Guanosine Monophosphate (GMP).

Adenosine monophosphate na Guanosine monophosphate zote ni nishati zilizokwishatumika (ash) na husababisha kiu na njaa ili kuzirudishia stoo za nguvu nishati iliyopotea kwenye seli za ubongo. Kwahiyo, unywaji soda husababisha matumizi yasiyo ya busara ya hifadhi za nguvu za seli za ubongo.

Ni ukweli unaojulikana kisayansi kuwa, nishati iliyotumika AMP, huleta hisia za njaa. kafeina husababisha utegemezi (addiction), na watu wanaoitumia mara kwa mara wanatakiwa wajihesabu kama wanatembea katika soda (sodaholics).

Hivyo matumizi ya soda zenye kafeina kwa watu wasiofanya mazoezi lazima yatapelekea kuongezeka uzito, kwa kuzunguka, unywaji wa soda unasisimua kula zaidi sababu ya ubongo kulazimishwa kutumia hifadhi zake za nguvu.

Kumbuka ni baadhi tu ya thamani ya nguvu ya chakula itachukuliwa na ubongo. Sehemu kubwa ya nguvu iliyochukuliwa itahifadhiwa katika mfumo wa mafuta ikiwa haitatumika katika shughuli za mishipa (mazoezi).

Matokeo haya ya uzito kuongezeka kupita kiasi ni moja kati ya matokeo mengine mengi yatokanayo na matumizi ya soda. Kafeina hupatikana pia katika chai ya rangi, kahawa na katika vinywaji vingine vingi vya viwandani.

Tabia moja mhimu inayokuja kujiimarisha ni mwitikio wa ubongo kwa radha za utamu. Lugha ya kitaalamu inayotumika kuelezea mwitikio huu ni,'cephalic phase response'. Mwitikio huu wa kulazimishwa unakuja kujengwa kama matokeo ya mazoea ya muda mrefu kwa radha zenye utamu zinazoambatana na utambulishaji wa nguvu mpya ndani ya mwili.

Wakati radha zenye utamu zinaposisimua katika ulimi, ubongo unaliamuru Ini kujiandaa kupokea nguvu mpya (sukari) kutoka nje. Ini nalo litasimama kutengeneza sukari toka hifadhi ya protini na wanga ya mwili, na kuanza kuhifadhi nishati ya kimetaboli inayozunguka kwenye mzunguko wa damu.

Kama Michael G Tardoff, Mark I Friedman na wanasayansi wengine, wameonesha kuwa 'cephalic phase' huwa na matokeo ya kuongeza shughuli za kimetaboli ili kuhifadhi lishe, nishati inayopatikana kwa ajili ya mabadiliko hupungua na kusababisha kuongezeka kwa njaa.

Ikiwa ni sukari hasa ndiyo inayosisimua ulimini, matokeo kwenye ini yatakuwa ni urekebishaji wa hicho kilichoingia mwilini. Ingawa ikiwa radha ya utamu haina lishe ndani yake, hisia za kutaka kula zitakuwa ndiyo matokeo yake.Ni Ini ndilo linalotengeneza hisia za kula. Kadiri radha utamu bila kalori ndani yake zinavyosisimua kionjea radha, vivyo hivyo zinavyokuja zaidi hisia za kutaka kula.

Matokeo ya 'cephalic phase' kwa radha za utamu yamethibitishwa katika majaribio kwa wanyama kwa kutumia 'saccharin' (dawa yenye utamu kama sukari). Kwa kutumia aspartame, wanasayansi kadhaa wameonesha matokeo yanayofanana ya kutaka kula kupita kiasi kwa binadamu.

Blundel na Hill wameonesha kuwa viongeza utamu visivyo na kalori hasa aspartame huongeza njaa na kuongeza uchukuaji wa chakula kwa muda mfupi. Wanaripoti, ''baada ya kunyweshwa aspartame, wapendwa waliachwa na njaa iliyobaki ikilinganishwa na walivyoachwa baada ya Glukozi. Njaa hii iliyobaki husababisha kuongezeka kwa matumizi ya chakula''.

Tardoff na Friedman wameonesha kuwa hisia hizi za kutaka kula zaidi chakula baada ya viongeza utamu vya kutengenezwa vimetumika, zinaweza kudumu mpaka dakika 90 baada ya kinywaji kitamu hata wakati majaribio yote ya damu kuonesha thamani ya kawaida. Wameonesha kuwa hata wakati usawa wa damu kwa insulini, usawa wa juu ambao unafikiriwa kuwa unasababisha njaa, umefikia usawa wa kawaida, majaribio kwa wanyama yameonesha hitaji la kutaka kula zaidi ya udhibiti.

Hii inamaanisha kwamba ubongo unashikilia kwa muda mrefu zaidi hisia za kutaka kula inapotokea tezi za kuhisia sukari zimesisimuliwa bila sukari kuwa imeingia kwenye mfumo. Radha utamu husababisha ubongo kuliamuru ini kuhifadhi ziada badala ya kuitumia toka katika akiba za mwili.

Kimsingi, mwitikio huu wa kifiziolojia kwa viongeza utamu bila kuwa na kalori ambazo mwili unazitumainia, unamlazimisha mtu kutafuta kalori hizo kokote na hatimaye kuhitaji kula.

Wakati kafeina na aspartame vimeingia mwilini, huanza kuonesha (dictates) matokeo yake ya kusisimua kwenye fiziolojia ya seli kwenye ubongo, kwenye ini, kwenye figo, kwenye kongosho, kwenye tezi mbalimbali na kadharika.

Aspartame hubadilishwa kuwa 'phenylalanine' na 'aspartate', zote huwa na matokeo ya moja kwa moja ya usisimuaji kwa ubongo. Kwa haraka matokeo ya kafeina na aspartame yanajenga namna mpya za kazi kwa ubongo, kwa sababu vinapatikana kwa kujirudia kwa kiasi kikubwa zaidi ya kile ambacho pengine kingeleta usawa wa kifiziolojia.

Transimita nyurolojia zilizo nyingi, ni mazao ya pili kutoka moja au asidi amino zingine. Hata hivyo aspartate ni moja kati ya jozi ya asidi amino za pekee ambazo hazihitaji kubadilishwa kuwa zao la pili ili kufanya kazi kwenye ubongo. Kuna nukta zinazopokea (receptors) hizi asidi amino mbili kwenye neva seli maalumu ambazo huathiri fiziolojia ya mwili haraka zaidi.

Matumizi ya viongeza utamu kwa usisimuaji wake wa kimakosa wa miishio ya neva ambayo husajili usambazaji wa kuingia wa nguvu kwenye mwili, yana matokeo mengine zaidi yasiyotarajiwa zaidi ya kusababisha kuongezeka uzito kupita kiasi.

Kwa muda wote, kemikali hizi zinaning'inia kwenye fiziolojia ya mwili kwenye mwelekeo unaoamuliwa na mfumo wa neva zinazozisisimua. Matumizi yake bila uelewa wa matokeo yake ya muda mrefu mwilini sababu tu yanasisimua tezi za radha, bado hayajaainishwa.

Utafiti umeonesha kuwa mapokezi ya aspartame yanapatikana pia kwa baadhi ya mifumo ya fahamu ambayo matokeo yake husisimua pia ogani za uzazi na matiti. Usisimuaji wa kudumu kwa tezi za matiti bila sababu nyingine zinazohusiana na ujauzito, unahusishwa kama moja ya sababu za kuongezeka kwa saratani ya matiti kwa wanawake.

Homoni iitwayo prolactini ndiyo inahusika zaidi katika mwelekeo huu. Moja ya vitu ambavyo havijafanyiwa utafiti wa kutosha juu ya madhara ya aspartame, ni matokeo yake ya madhara yanayoweza kupelekea kutokea kwa saratani ya ubongo. Majaribio kwa panya na wanyama wengine, yote yameonesha aspartame kuhusika kutengeneza uvimbe kwenye ubongo.

Dr.H.J.Roberts ameyaainisha baadhi ya matatizo ya kiafya yanayosababishwa na aspartame, na kuyaita yote kwa pamoja kama, 'magonjwa ya aspartame',katika kitabu chake; ''Breast Implants or Aspartame Diseases?'', ameyataja baadhi ya magonjwa kama vile kuumwa kichwa, kizunguzungu, kukosa usingizi, kuchanganyikiwa, kupoteza kumbukumbu, uchovu sugu, kushuka kwa damu sukari, maumivu ya maungio, nywele kupotea, na kadharika, kama ni magonjwa yasababishwayo na aspartame. Ameandika makala na vitabu vingine vingi juu ya mada hii.

Sayansi ya sasa ya kudhibiti kuongezeka uzito kupita kiasi inayohusisha ukatazaji wa baadhi ya vyakula, hata kama baadhi ya kilo zitapungua, zitaongezeka tena baada ya muda mfupi. Cha kushangaza zaidi ni fasheni mpya inayojitokeza siku hizi, mtu anakuwa mtumwa wa kuchagua chakula hiki au kile kama mbwa mnusaji hasa katika suala la helemu (cholesterol).

Usishituke!, ''tofauti na imani iliyojengeka ya kupunguza au kuondoa kabisa matumizi ya mayai katika milo yetu, mimi nakula mayai mengi nitakavyo – dr.Batmanghelidj''. Mayai yana protini nzuri iliyosawazishwa. Anasema, anaelewa pia ni namna gani utengenezwaji wa kolesteroli unavyohusiana na upungufu wa muda mrefu wa maji mwilini (prolonged dehydration).

Ikumbukwe kuwa, kafeina ni dawa ya kulevya(addictive drug) ambayo matumizi yake yamehalarishwa. Watoto wadogo kwa upande wao wanatokea kuwa wategemezi kirahisi zaidi kwa vinywaji vyenye kafeina. Hii ndiyo sababu ya kwanza watoto wengi mashuleni siku hizi hawafundishiki, tunabaki kuwalaumu bure.

Usisimuaji huu wa miili kwa vinywaji vyenye kemikali kwa watoto, hupelekea baadhi yao kuwa wategemezi wa madawa ya kulevya makubwa zaidi wakati wanapokuwa wakubwa.

Kama tulivyofafanua muda wote, mwili hutoa ishara anuwai unapokuwa na maji chini ya kiwango. Wakati huu (uzito unapozidi), mwili unakuwa unahitaji maji pekee.Mwili unaanza kuchanganya habari wakati mtu anapoamua kutumia vinywaji vya kutengenezwa kama mubadala wa mahitaji ya mwili kwa maji.

Kwa hiyo, utumiaji wa muda mrefu na wa kudumu wa soda, lazima uchukuliwe kama moja ya visababisho vya matatizo mengi ya kiafya katika jamii zetu.
 
Siachi kunywa hata kwa fimbo........maana naona kilakitu ni sumu. Kitimoto mnasema ni sumu, kuku oooohhh mafua ya Ndege. Sasa mmehamia kwenye vinywaji gongo nalo mnasema ni sumu.......aagggrrrh am confused.

Eti hata bangi ni sumu.......no no katazeni vyote ila pombe ya mnazi niachieni jamani. oooohh Tanga kwetu
 
Siachi kunywa hata kwa fimbo........maana naona kilakitu ni sumu. Kitimoto mnasema ni sumu, kuku oooohhh mafua ya Ndege. Sasa mmehamia kwenye vinywaji gongo nalo mnasema ni sumu.......aagggrrrh am confused.

Eti hata bangi ni sumu.......no no katazeni vyote ila pombe ya mnazi niachieni jamani. oooohh Tanga kwetu
We bwia tu siko ukiona unashindwa vitu vya msingi ndonutaelewa wenzako wanachosema kunywa ukwaju acha hizo!
 
Kumbuka lile tangazo lao moja linasema: ''MORE FANTA, LESS SERIOUS''. Wanapoandika matangazo kama haya wenyewe wanajuwa wanamaanisha nini. Wewe kunywa tu ila elimu nayo utapewa tu. Mnazi kunywa mkuu hata gongo na kitimoto haina ubaya wowote labda kama hufanyi mazoezi ila SODA usiwashirikishe watoto wako wanaoenda shuleni wataenda kusinziasinzia tu darasani.

Siachi kunywa hata kwa fimbo........maana naona kilakitu ni sumu. Kitimoto mnasema ni sumu, kuku oooohhh mafua ya Ndege. Sasa mmehamia kwenye vinywaji gongo nalo mnasema ni sumu.......aagggrrrh am confused.

Eti hata bangi ni sumu.......no no katazeni vyote ila pombe ya mnazi niachieni jamani. oooohh Tanga kwetu
 
Pombe ni mbaya hasa unapozidisha. Tatizo la soda ni kuwa wanakunywa hata watoto wadogo na madhara yake ni mengi na yanadumu kwa miaka na vizazi.

Shukrani mkuu fadhili nitazingatia ushauri wako.!
 
Last edited by a moderator:
Pombe na Soda vinamadhara ila serikali itawaelewa? Mjue pie , The highest Tax payers in TZ ni SODA NA BEER na SIGARA,
 
Soda ni sumu


Utafiti wa wanasayansi mbalimbali duniani unaonesha kuwa kuna madhara makubwa ya utumiaji wa vinywaji aina ya soda katika mwili wa mwanadamu

AFYA za mamilioni ya Watanzania wanaotumia vinywaji vya aina ya soda ipo hatarini, baada ya kugunduliwa uwepo wa chembechembe zenye kemikali za sumu ndani ya vinywaji hivyo, MTANZANIA Jumatano linaripoti.

Utafiti uliofanywa na Muungano wa Waandishi wa Habari za Uchunguzi Tanzania (Investigative Journalists Union of Tanzania- IJUTA) pamoja na tafiti zilizofanywa na wataalamu waliobobea katika afya ya umma duniani, umebaini kuwa vinywaji baridi aina ya soda ni hatari kuliko utumiaji wa sigara inayosababisha maradhi ya kansa katika mwili wa binadamu.
Kwa mujibu wa utafiti wa wanasayansi mbalimbali duniani, yapo madhara makubwa ya utumiaji wa vinywaji vya aina ya soda katika mwili wa binadamu.

Utafiti huo unaonyesha kuwa zipo sababu nane kuu zinazokiweka kinywaji aina ya soda kwenye kundi la vinywaji vyenye sumu ambavyo havifai kwa matumizi ya binadamu.

IJUTA imebaini kuwa makampuni makubwa yanayotengeneza vinywaji baridi aina ya soda yanatumia mabilioni ya dola kila mwaka kujitangaza na kutoa misaada ya kijamii kutokana na mauzo yake, bila kutaja madhara ya vinywaji hivyo kwa binadamu.

Kwamba matangazo hayo yanayogharimu mamilioni ya fedha ndiyo yanayokifanya kinywaji hicho kuwa maarufu zaidi duniani, licha ya kuwa na madhara makubwa katika mwili wa binadamu.

Aidha, utafiti huo unaonyesha kuwa umaarufu mwingine wa kinywaji aina ya soda ni utamu wa kupindukia ulio ndani ya soda.

Utafiti wa IJUTA unaonyesha kuwa utamu wa kupindukia iliomo ndani ya soda unawapumbaza wanywaji ili wasisikie ladha kali ya asidi iliyomo ndani ya soda.

IJUTA imegundua kuwa kiwango cha asidi kilicho ndani ya soda hakiwekwi wazi kwa walaji kwa sababu ya kuhofia kuwa wakibaini wataacha kikutumia kinywaji hicho.

Inaelezwa pia kuwa madini ya cola yaliyo ndani ya soda yana kilevi aina kafein kinachomteka mnywaji kuwa teja wa kinywaji hicho.

Tafiti za kitaalamu zimeonyesha kuwa soda inahusishwa na matatizo mengi ya kiafya kwa watoto na watu wazima, yakiwemo matatizo ya kuongezeka unene kupita kiasi, ugonjwa wa ini na mengineyo.

Utafiti uliofanywa nchini Marekani unaonyesha kuwa soda huwekewa ‘fructose’ (sukari) nyingi kupitia mfumo wa sirapu (fructose corn syrup) ambayo inaongoza kwa kusababisha magonjwa ya unene, kisukari, ugonjwa wa moyo na magonjwa mengine sugu yanayowakabili Wamarekani wengi hivi sasa na dunia kwa ujumla.

Dk. Mercola, ambaye ni mtaalamu wa masuala ya lishe asilia na tiba mbadala nchini Marekani, amekaririwa na tafiti mbalimbali zilizofanyika nchini humo akieleza kuwa kinywaji aina ya soda ni hatari kwa binadamu, sawa na mtu anayevuta sigara au zaidi, jambo alilosisitiza kuwa siyo la kutia chumvi, bali ukweli halisi.

Watumiaji wa vinywaji aina ya soda wanaelezwa kuwa wamekuwa wakinywa kiasi kikubwa cha kaboni, kafeini (dawa ya kulevya), sukari ya kupundukia na asidi kali ambayo huvuruga afya ya mtumiaji kwa kiwango cha juu.

Soda pia imebainika kutokuwa na lishe ya aina yoyote zaidi ya maji na sukari.

Uchunguzi wa IJUTA na utafiti ya wanasayansi mbalimbali duniani, umeonyesha kuwa watu wengi hawajui kuwa unywaji wa soda huwaongezea kiasi kikubwa cha madini joto.

Chupa moja ya soda yenye ujazo wa mililita 330 husababisha unene kwa kiwango cha paundi moja kwa mwezi.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Kisukari Tanzania (TDA), Ramadhan Mongi, amepata kukaririwa na vyombo vya habari hapa nchini akieleza kuwa ugonjwa wa kisukari Tanzania umeongezeka mara sita katika siku za hivi karibuni.

Alisema miaka kumi iliyopita, hali ya kisukari ilikuwa asilimia tatu (3), lakini katika miaka ya karibuni umeongezeka mara sita.

“Tunastahili kuongeza jitihada ya kupambana na gonjwa hili la kisukari kwa gharama zote kwa sababu kisukari ni moja ya magonjwa manne yanayomaliza Watanzania,” alisema.

Utafiti uliofanyika Mkoa wa Dar es Salaam ulibaini kwamba kati ya watu watano waathirika wa kisukari, mmoja tu ndiyo hupata matibabu ya serikali.

Unywaji kwa mpigo wa kabohaidrets iliyo na sukari nyingi kwenye soda hudhoofisha seli zinazozalisha vimeng’enya tofauti na vyakula vingine na pia imebainika kuwa sukari ikiingia kwa wepesi kwenye mzunguko wa damu husababisha kongosho kuzalisha vimeng’enya vingi mwilini.

Uchunguzi wa kitabibu katika Hospitali ya wanawake ya Boston nchini Marekani na katika Chuo cha Kitabibu cha Harvard umeonyesha wanawake 51,000 hawakuwa na kisukari mwanzoni mwaka wa 1991, lakini miezi minane baadaye wanawake 741 waligundulika na kisukari.

Ripoti ya utafiti huo ilionyesha kuwa wanawake waliokuwa wakitumia kinywaji aina ya soda moja ama mbili kwa siku waliongezeka uzito maradufu na walikuwa hatarini kupata ugonjwa wa kisukari.

Pia ilionyesha kuwa soda hudhoofisha mifupa na husababisha hali ya mifupa kupuputika, hali inayomuweka mtumiaji kuwa katika hatari ya kuvunjika mifupa kirahisi.

Madhara mengine yaliyobainika kusababishwa na unywaji soda ni kupukutika kwa meno na ama kuoza. Pia soda husababisha matatizo ya figo.

Soda yenye chembe ya cola husababisha figo kuwa na mawe kwa sababu ya asidi na kemikali mbalimbali zinazofichwa vipimo vyake kwa walaji.

Madaktari bingwa wa wanamichezo wanaeleza madhara yanayosababishwa na soda mwilini kuwa ni pamoja na shinikizo la damu, uharibifu wa ini, huvurugu mfumo wa kumeng’enya chakula tumboni kutokana asidi ya kiwango cha juu iliyo kwenye soda.

Wanashauri kuwa soda haistahili kutumika kama kishawishi kwenye mchezo, kwa sababu ina madhara makubwa kwa wanamichezo kwa sababu hunyonya maji kwenye mwili na kudhoofisha mwili.

Wakati utafiti huo ukidhihirisha hayo, Taasisi ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) imeshindwa kutoa tamko lolote kuhusu utafiti huo, hata baada ya kupelekewa maswali kwa maandishi yanayoomba ufafanuzi wa ubora wa vinywaji vya soda katika mwili wa binadamu.

Source mtanzania
 
Mkuu haya yanajulikana miaka mingi sana iliyopita, Redbull ndo hatari zaidi na kuna baadhi ya nchi imepigwa marufuku, lakini hapa kwetu ndo inatumika kama mbadala wa viagra! akina dada nao wanaona kama ni kinywaji chenye hadhi bila ya kujua madhara yaliyomo ndani yake...
Watanzania lazima watambue kuwa Saratani ndo ugonjwa unao ongoza kwa kuua watu wengi zaidi kuliko magonjwa ya Ukimwi + Malaria + Kifua Kikuu kwa ujumla wake! Inasikitisha kuona kampeni nyingi sana za kutokomeza malaria na Ukimwi zikipigiwa chapuo na wanasiasa na kuacha Ugonjwa wa saratani wenye kuleta madhara makubwa zaidi kwa jamii...
 
Kinana premium lager vip?kwan kupata bila angalau 5 mmhhhh!
 
tatizo ni jinsi ambavyo taarifa kama hizi zitavyowafikia watanzania wengi zaidi ili wafahamu madhara ya utumiaji wa vinywaji vya namna hii
 
hilo suala linajulikana hata wenyewe coca wanajua na ndio wa kaanzisha different coca kama diet, zero nk so inakuwa chaguo lako lakini bado hata hizo zina matatizo kiasi ingawa sijajua kiundani zaidi
 
Back
Top Bottom