Madhara ya unywaji wa soda kwenye afya ya Binadamu

ni kwlei soda haisaidii chochote ktk miili yetu.
 
ni kweli kabisa soda ni hatari kwa afya zetu.
 
mkuu soda ni hatari sana ata hivyo mi ntazungumzia sana soda kwani chupa moja ya soda hujaza vijiko 9 za sukari unategemea nini kama si kupata ugonjwa wa kisukari though hii pia inategemeana na kongosho yako.
 
Mara kadhaa nimepata kusikia juu ya soda kuwepo madhara kiafya, kwa hili sasa, bye bye Pepsi products, Coke products n Azam Cola.

Afya kwanza bana.
 
kila kitu madhara mimi napiga kama kawaida, tena mmenitamanisha ngoja nichukue chupa niende dukani
 

this is no research but a list of fallacies, enjoy your coke.
 
Wakuu vitu kibao vina madhara sio soda 2 mpaka chai ni nouma. Wataalam 2pieni hapo madhara ya chai, kahawa na dear gambe...
 

Mamilioni ya watanzania wanaotumia vinywaji aina ya soda ipo hatarini baada ya kugunduliwa uwepo wa chembechembe zenye kemikali za sumu ndani ya vinywaji hivyo, MTANZANIA jumatano linaripoti.

Utafiti uliofanywa na Muungano wa Waandishi wa habari Tanzania (Investigative Journalists Union of Tanzania-IJUTA) pamoja na tafiti zilizofanywa na wataalamu waliobobea katika afya duniani umebaini kuwa vinywaji baridi aina ya soda ni hatari kuliko utumiaji sigara inayosabisha maradhi ya kansa katika mwili wa binadamu.

Kwa mujibu wa utafiti wa wanasayansi, yapo madhara makubwa ya utumiaji wa vinywaji vya aina ya soda katika mwili wa binadamu.

Utafiti umeonyesha kuwa zipo sababu nane kuu zinazokiweka kinywaji cha soda kwenye kundi la vinywaji vyenye sumu.

IJUTA imebaini kuwa makampuni makubwa yanayotengeneza vinywaji kuwa makampuni yanayotengeneza soda yanatumia mabilioni ya dola kila mwaka kujitangaza na kutoa misaada kijamii kutokana na mauzo yake, bila kutaja madhara ya vinywaji hivyo.

Utafiti wa IJUTA umeonyesha kuwa utamu wa kupindukia uliomo ndani ya soda unawapumbaza wanywaji ili wasisikie ladha kali ya acid iliyomo ndani ya soda.

IJUTA imegundua kuwa kiwango cha acid kilichomo ndani ya soda hakiwekwi wazi kwa sababu ya kuhofia kuwa watu wakibaini wataacha kutumia kinywaji hicho.

Inaelezwa kuwa madini ya cola yaliyomo yana kilevi cha aina ya kafein kinachomteka mnywaji kuwa teja wa kinywaji hicho.

Dr. Mercola wa Marekani amekaririwa na tafiti mbalimbali akieleza kuwa soda ni hatari kwa binadamu sawa na mtu anayevuta sigara au zaidi.

...Soda yenye chembe za cola husababisha figo kuwa na mawe kwa sababu ya acid na chemicals zinazofichwa vipimo vyake kwa watumiaji.

Wakati utafiti huo ukidhihiriksha hayo, Taasisi ya chakula na Dawa Tanzania (TFDA) imeshindwa kutoa tamko lolote kuhusu utafiti huo, hata baada ya kupelekewa maswali kwa maandishi yanayoomba ufafanuzi wa ubora wa vinywaji vya soda katika mwili wa binadamu.



SOURCE: MTANZANIA
ISSN : 0856-5678, Na. 7310
Toleo la leo
ukurasa wa 3

UTAFITI: SODA NI SUMU KULIKO SIGARA.... - MPEKUZI HURU
 
Kwa hiyo wale wa Guinness na Coke Baba, kwisha kabisa ?
 
Aisee!!ndo maana watu wengine wanatumia soda kama mbadala wa JIK wanaposafisha choo au sink la kunawia.ebu mwaga kwenye sink then subiri kama saa 6 hivi then anza kuosha,wewee ni zaidi ya JIK.Ina maana hata matumbo yetu (stomach membrane)yanakuwa eroded kama ule uchafu wa sink!! hasa ukitumia zile soda za rangi nyeusi!
Chezea c...la au there for more wewe!!
 
HILI LIPO WAZI.
>Familia yangu nimeielimisha vya kutosha japo kuwa haikuwa kazi rahisi kuwashawishi waniele.

MADHARA YA SODA NIYAJUAYO:

>Usababisha ukibogoyo na udhaifu wa mifupa.
"soda/vinywaji vyote vya kopo vinatunzwa na madini ya 'PHOSPHORUS' "

Phosphorus ndiyo inayoungana na madini ya CALCIUM (na madini kadhaa) kutengeneza MIFUPA,

Phosphorus iliyoko kwenye soda/vinywaji vya kopo, usababisha mifupa kudhoofika( it tend to excract bones calcium)

>SODA/vinywaji vya kopo usababisha Aleji.

>
>
>

MKUU MZIZI MKAVU,
hongera kwa kuelimisha jamii.
 
Soda ina sumu kali sana iligundulika mda mrefu huko marekan wajameni tunakufa taratibu bila kujijua
nimekuwa nikisumbuliwa sana na kichwa kwa mda mrefu nakumbuka mwaka juzi nilipima damu na ikagundulika nilikuwa na sumu iliyotokana na soda na nikashauriwa niache kabisa kunywa na kwa kusafisha sumu hiyo nikashauriwa kunywa maji ya kutosha
 
Hivi karibuni baadhi ya vyombo vya habari viliripoti kuwa kinywaji aina ya soda ni hatari kwa kuwa kina sumu. Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imekanusha taarifa hiyo na kusema kuwa taarifa hiyo haikufuata misingi ya kisayansi na kuwa kinywaji hicho hakina madhara kama ilivyodaiwa kwenye taarifa hiyo. Taarifa ya TFDA imesema kinywaji hicho hutumika duniani kote na kinazalishwa kwa kuzingatia viwango vya ubora na usalama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…