Madhara ya unywaji wa soda kwenye afya ya Binadamu

Madhara ya unywaji wa soda kwenye afya ya Binadamu

sio kweli,baadhi zilizopo hapo ni za uongo na zimekaa kisda sana,hazina ushahd wa kisayansi,ziko kwa kufikirika,acheni kudanganya watu.

HATIMAYE KINYWAJI CHA SODA CHAANZA KUPIGWA MARUFUKU NCHI ZA NJE

*Yakatazwa shuleni, watoto chini ya miaka 12
*Sasa yabainika kuwa ina sumu inayoua taratibu
*Yagundulika kupumbaza na kusababisha uteja



SIKU chache baada ya gazeti la Mtanzania kuripoti madhara yanayosababishwa na kinywaji aina ya soda, katika utafiti wake gazeti hilo limebaini mengine mapya.

Kwa mujibu wa utafiti huo, imebainika kuwa soda imepigwa marufuku kutumiwa na watoto walio na umri chini ya miaka 12 na walio shuleni katika baadhi ya mataifa ya Ulaya na Marekani, kutokana na madhara ya kiafya yanayosababishwa na kinywaji hicho.

Taarifa zilizotolewa na Shirika la Habari la The Press Television Technology Advertising and Branding (Adweek) zinazonukuu taarifa ya kampuni moja kubwa duniani inayozalisha kinywaji aina ya soda, imeamua kupambana na unene (obesity), unaosababishwa na unywaji wa soda kwa kuondoa matangazo ya vinywaji vyake kwenye vyombo vya habari.

Kampuni hiyo kupitia taarifa yake hiyo iliyotolewa katika moja ya sherehe zake, ilieleza kuwa lengo la kuondoa matangazo hayo ni kuwanusuru watoto wadogo na matumizi ya vinywaji aina ya soda vilivyobainika kuwa na madhara katika mwili wa binadamu.

Nchini Marekani, tayari imekwishapitishwa sheria inayokataza watoto walio na umri wa chini ya miaka 12, kunywa kinywaji aina ya soda.

Mwenyekiti wa Kampuni hiyo, alieleza kuwa mipango ya mbeleni ya kampuni yake ni kutengeneza kinywaji hicho kikiwa na kiwango kidogo cha Kalori na kubuni kinywaji cha aina hiyo ambacho kitakuwa hakina Kalori.

Alisema mipango hiyo itatekelezwa duniani kote ambako kinywaji cha aina ya soda kinatengenezwa na nchini Marekani tayari imekwishaanza kutekelezwa.

Aidha, Kampuni hiyo imeahidi kuweka wazi virutubisho vyote vinavyotumika kutengeneza bidhaa zake na kuahidi kutoa misaada ya hali na mali kwa nchi zote 200 duniani ambako kinywaji cha soda kinauzwa.

Mbali na Marekani, kinywaji cha aina ya Soda kimekwishapigwa marufuku shuleni katika nchi za Uingereza, Ufaransa na katika majimbo ya Los Angeles, Philadelphia na Miami nchini Marekani na kwa watu wazima matumizi yake yanaelekezwa kuwa ya kiwango kidogo sana.

Vyombo vya habari vya nchini New Zealand, mwezi Machi mwaka huu viliripoti kuwa mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Natasha Harris (31), alifariki kutokana na unywaji wa soda nyingi.

Shirika la habari la AFP la Ufaransa, liliripoti tukio hilo kwa kueleza kuwa Natasha alikuwa akinywa soda nyingi kila siku, jambo ambalo liligeuka kuwa sehemu ya maisha yake kwa kipindi cha miaka mingi.

Kwamba familia ilikuwa ikimuita teja wa soda, baada ya meno yake kuoza kwa sababu ya kunywa soda, alijifungua mtoto ambaye hakuwa na fizi jambo ambalo liligundulika baadaye kuwa lilisababishwa na matumizi makubwa ya kinywaji hicho.

"Tumegundua kwamba, kwa kuzingatia ushahidi uliopo, kama sio unywaji wa soda uliopitiliza, Natasha Harris asingekufa katika muda ule na katika hali alivyokufa

"Ripoti ya Daktari aliyechunguza maiti yake (Pathologia), iligundua kwamba ini lake lilipanuka sana, likawa na mrundiko mkubwa wa mafuta kutokana na kula sukari kwa wingi. Kuwepo kwa madini aina ya ‘potasiam' kwa kiwango kidogo sana kwenye damu yake, pia kulitokana na unywaji wa soda." Taarifa ya kitabibu katika Hospitali aliyofia nchini New Zealand ilieleza.

Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali za kisayansi zilizo kwenye mitandao ya wanasayansi waliobobea duniani, unywaji wa soda humpumbaza mtumiaji na kumsahaulisha kula vyakula vyenye madini muhimu mwilini.

Moja ya andishi linalotahadharisha utumiaji wa kinywaji cha soda na kukitaja kuwa cha hatari kwa matumuzi ya binadamu, ni Jack Winkler, Profesa wa sera za lishe katika Chuo Kikuu cha Metropolitan nchini London, linaloeleza kuwa Soda ni bidhaa ya kishetani inayoua binadamu taratibu baada ya kinywaji hicho kumzalishia magonjwa mengi mwilini yanayomfanya kuwa tegemezi wa dawa.

Wakati msomi huyo akieleza hayo katika utafiti wake, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Dk. Raymond Wigenge, amelieleza gazeti hili soda siyo kinywaji hatari kwa matumizi ya binadamu kwa sababu kinatumiwa na mamilioni ya watu duniani kote.

Akizungumza na MTANZANIA Jumatano ofisini kwake wiki iliyopita baada ya kutoa ufafanuzi kuhusu madhara yanayosababishwa na kinywaji aina ya soda katika mwili wa binadamu, Dk. Wigenge alisema pamoja na changamoto zilizopo katika kinywaji hicho, taasisi yake haipingi uwepo wa kinywaji hicho sokoni.

"Soda haina shida kwa binadamu na hata mkiendelea kuandika suala hili, sisi tutaendelea kuueleza umma kwamba waendelee kupata kinywaji, hivyo kama ambavyo tumekuwa tukifanya," alisema.

Alipoulizwa kama anakubaliana na tafiti za wanasayansi bingwa wa magonjwa ya binadamu walioeleza katika tafiti zao kuwa unywaji wa soda una madhara katika mwili wa binadamu, alisema hizo ni changamoto za kawaida, kwa sababu madhara yaliyomo kwenye soda hayamuathiri mtu mara moja bali huchukua muda mrefu.

Wakati Dk. Wigenge akieleza msimamo wake kuhusu kinywaji aina ya soda, nchini Mexico, taasisi ya El Poder del Consumidor inayojihusisha na kutetea walaji, inashinikiza Serikali ya nchi hiyo kuzilazimisha kampuni za soda kuorodhesha madini na chembechembe zote za kemikali zinazotumika kutengeneza kinywaji hicho.

Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Alejandro Calvillo, amekaririwa na vyombo vya habari vya nchi hiyo akieleza kuwa unywaji wa soda ni hatari na hilo limethibitishwa na wataalamu wa afya duniani kuwa soda ni sumu mbaya, inauwa taratibu.

Tafiti mbalimbali za wanasayansi zinaeleza kuwa soda ina asidi aina ya ‘phosphoric' yenye uwezo wa kuvuruga madini ya ‘calcium' yaliyoko mwilini na kusababisha mifupa na meno kudhoofika.

Aidha, asidi aina ya ‘phosphoric' huvuruga asidi aina ya ‘hydrochloric' iliyo tumboni mwa binadamu na hivyo kuharibu mfumo wa kusaga chakula.

Viwanda vya soda ndio watumiaji wakubwa wa sukari na wanasayansi wanasema sukari hupandisha kiwango cha ‘insulin' ambayo husababisha kasi ya mzunguko wa damu, ugonjwa wa moyo, kupanda kwa ‘Cholesterol, kisukari, kuzeeka mapema, ongezeko la uzito na maradhi mengine.

Aidha inadaiwa kuwa viwanda vya soda pia hutumia dawa ya kulevya aina ya kafeini. Wataalamu wanasema vinywaji vyenye kafeini, husababisha kupanda kwa mapigo ya moyo, kasi ya mzunguko wa damu na matatizo ya kizazi.
 
sio kweli,baadhi zilizopo hapo ni za uongo na zimekaa kisda sana,hazina ushahd wa kisayansi,ziko kwa kufikirika,acheni kudanganya watu.

Soda huongeza uzito mwilini


9162214-set-of-refreshing-soda-drinks-in-metal-cans.jpg

kwa mjibu wa utafiti wake, dr.Batmanghelidj, anasema, ingawa soda hazina kalori inayoweza kuainika, zinaweza kuwa kisababisho cha kuongezeka uzito kupita kiasi kwa wale wanaozinywa kwa malengo ya kudhibiti uzito wao.

Kitendawili hiki katika uelewa wetu juu ya uhusiano baina ya unywaji wa vimiminika ambavyo havichangii moja kwa moja uchukuaji wa kalori wa mwili na kuongezeka kwa uzito, kinahitaji ufafanuzi. Kwa mjibu wa utafiti huo, kuna watu wengi waliochukua uamuzi wa kunywa soda ili kudhibiti uzito, lakini matokeo yamekuwa kinyume chake.


Viwanda vya vinywaji vinakuwa kwa kasi kubwa (apace), jarida la The Nation la aprili 27, 1998 liliripoti kuwa, watoto na vijana walio wengi wanakisiwa kunywa mpaka galoni 64 za soda kwa mwaka, kiasi ambacho kiliongezeka mara tatu zaidi tangu mwaka 1978, kikaongezeka mara mbili zaidi kwa mafungu ya umri kati ya miaka 6-11 na kuongezeka kwa robo kwa watoto chini ya miaka 5 (chanzo: utafiti, kitengo cha kilimo 1994, marekani).

Inavutia pia kuandika hapa kuwa, kuongezeka huku kwa matumizi ya soda kwa watoto chini ya miaka 5, kuweza kuwa ndiyo sababu ya kuongezeka mara tatu zaidi ya ugonjwa wa pumu (asthma) kwa watoto wa umri huo kati ya mwaka 1980 na 1994.

Utafiti mmoja katika kampasi ya chuo kikuu cha pennsylvania nchini marekani, ulionesha baadhi ya wanafunzi kunywa soda 14 kwa siku, msichana mmoja alitumia soda 37 kwa siku mbili. Wengi wamekiri kuwa hawataweza kuishi bila vinywaji hivi baridi.

Ikiwa vinywaji hivi vitaondolewa sokoni, watu hawa wataonesha dalili zilizosawa na zile zinazowatokea waliokuwa wategemezi kwa madawa mengine ya kulevya.
Jarida la Boys Life, liliwatafiti wasomaji wake na kugunduwa kuwa, asilimia 8 ya wasomaji wake wanakunywa soda 8 au zaidi kwa siku. Viongozi wa kambi moja ya skauti (boy scout jamboree), walikusanya chupa 200,000 tupu za soda kwa ajili ya matumizi mengine (recycling), chama cha vinywaji baridi kimefanya utafiti juu ya matumizi ya vinywaji hivi baridi mahospitalini nchini marekani na kugunduwa zaidi ya asilimia 85 wakihudumia wagonjwa chakula pamoja na vinywaji hivi baridi.

Kwa kiasi kikubwa, imeaminika kuwa vinywaji hivi vinaweza kuwa mubadalawa mahitaji ya mwili kwa maji. Imedhaniwa kuwa, kwa sababu tu vinywaji hivi vina maji, mwili utakuwa umekamilishiwa mahitaji yake ya maji. Dhana hii ni potofu.

Kuongezeka kwa matumizi ya soda zenye kafeina, kunaunda vyanzo vingi vya matatizo ya kiafya kwenye jamii zetu. Imani hii potofu kwamba vimiminika vyote ni sawa na maji kwa mahitaji ya mwili, ndiyo chanzo kikuu cha magonjwa kwa mwili wa binadamu ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa uzito kupita kiasi.

Ili kuielewa dhana hii, inatubidi kutambua baadhi ya kanuni rahisi za kianatomia na kifizioloji za ubongo ambazo huongoza hisia za kula na kunywa.

Umbile kubwa la mwili bila mpangilio kwa kusanyiko la mafuta, ni hatua ya mwanzo ya kuanguka kwa mwili wa binadamu, na kwa mjibu wa maoni ya dr.Batmanghelidj, ni matokeo ya kuchagua kusiko sahihi kwa uchukuaji wa vimiminika. Baadhi ya vinywaji vina madhara zaidi ya vingine.
Kafeina, moja ya vitu mhimu katika soda nyingi, ni dawa ya kulevya!!!.

Hii ndiyo sababu kwa wale waliozoea kunywa chai ya rangi asubuhi wasipokunywa hujisikia kichwa kuuma (they are addicted).

Ina sifa ya kumfanya mtu mtegemezi kwayo sababu ya matendo yake moja kwa moja kwenye ubongo. Inaingilia pia katika ini na kusababisha kuongezeka kwa uzarishaji wa mkojo.

Hivyo, kafeina ni kikojoshi (diuretic).


Kifiziolojia, kafeina ni wakala mkausha maji mwilini. Hii ndiyo sababu mtu analazimika kunywa soda nyingi kwa siku bila kutosheka. Maji hayabaki mwilini kwa muda mrefu.


Wakati huo huo, watu wengi wanajichanganya kwa kutokutambua hisia zao za kiu kwa kudhani kuwa wamekunywa maji ya kutosha toka katika soda, wanajihisi kuwa ni wenye njaa na kuanza kula chakula zaidi ya mahitaji yao ya mwili. Kwa hiyo upungufu wa maji (dehydration) uliosababishwa na vinywaji baridi venye kafeina, kwa muda utasababisha kuongezeka kwa uzito kutokana na kula kupita kiasi ambako ni matokeo ya moja kwa moja ya kushindwa kuzielewa hisia za njaa na kiu.


Kafeina, ni kiamsho (pick-me-up), husisimua ubongo na mwili hata wakati mtu amechoka. Inajionesha kuwa, kafeina hupunguza udhibiti wa stoo ya kwanza ya ubongo (ATP). Hifadhi hii ya kwanza hutumika kwa baadhi ya kazi ambazo kwa kawaida zisingeweza kufikiwa kunapokuwa na usawa uliosawa wa hifadhi hii.


Ikitokea soda imeongezwa sukari, walau baadhi ya mahitaji ya ubongo kwa sukari hufikiwa. Ikiwa kafeina inatoa nguvu toka stoo ya kwanza ya nguvu za ubongo kusaidia ufanyikaji kazi, walau sukari yake itarudishia baadhi ya akiba za stoo ya kwanza hata kama matokeo ya mwisho ni matumizi hasi ya ulalo (deficit) ya stoo ya kwanza kwa ubongo.


Mwanzoni mwa miaka ya 1980, kiongeza utamu cha kutengenezwa (artificial sweetener) kiitwacho ‘aspartame', kilianza kutumika kwenye viwanda vya vinywaji baridi. Aspartame ina utamu mara 180 zaidi ya utamu wa sukari ya kawaida, bila nguvu yeyote (kalori) izarishwayo nayo.

Aspartame sasa inatumika kama kitu kisicho na madhara kwa sababu Taasisi ya Madawa (Federal Drug Administration ya marekani) imeitetea (deemed it) kama kitu kisicho na madhara kikitumika kama mubadala wa sukari.

Ndani ya utumbo mdogo, aspartame inabadilishwa kwenda transimita nyurolojia mbili, asidi amino aspartame na phenylalamine, vivyo hivyo methyl alikohol au formaldehyde. Inatetewa kuwa Ini huichukulia methyl alikoholi kuwa si sumu. ‘Binafsi nafikiri madai haya hutolewa kunyamazisha sauti zinazopinga biashara za vyakula vilivyotengenezwa viwandani vijulikanavyo kuwa na kemikali hatari kwa binadamu – dr.Batmanghelidj'.

Kafeina huibadilisha Adenosine Triphosphate (ATP) kwenda Adenosine Monophosphate (AMP) ambayo ni nishati iliyokwishatumika (ash) na aspartate huibadilisha Guanosine Triphosphate (GTP) kwenda Guanosine Monophosphate (GMP).

Adenosine monophosphate na Guanosine monophosphate zote ni nishati zilizokwishatumika (ash) na husababisha kiu na njaa ili kuzirudishia stoo za nguvu nishati iliyopotea kwenye seli za ubongo. Kwahiyo, unywaji soda husababisha matumizi yasiyo ya busara ya hifadhi za nguvu za seli za ubongo.

Ni ukweli unaojulikana kisayansi kuwa, nishati iliyotumika AMP, huleta hisia za njaa. kafeina husababisha utegemezi (addiction), na watu wanaoitumia mara kwa mara wanatakiwa wajihesabu kama wanatembea katika soda (sodaholics).

Hivyo matumizi ya soda zenye kafeina kwa watu wasiofanya mazoezi lazima yatapelekea kuongezeka uzito, kwa kuzunguka, unywaji wa soda unasisimua kula zaidi sababu ya ubongo kulazimishwa kutumia hifadhi zake za nguvu.


Kumbuka ni baadhi tu ya thamani ya nguvu ya chakula itachukuliwa na ubongo. Sehemu kubwa ya nguvu iliyochukuliwa itahifadhiwa katika mfumo wa mafuta ikiwa haitatumika katika shughuli za mishipa (mazoezi).


Matokeo haya ya uzito kuongezeka kupita kiasi ni moja kati ya matokeo mengine mengi yatokanayo na matumizi ya soda. Kafeina hupatikana pia katika chai ya rangi, kahawa na katika vinywaji vingine vingi vya viwandani.


Tabia moja mhimu inayokuja kujiimarisha ni mwitikio wa ubongo kwa radha za utamu. Lugha ya kitaalamu inayotumika kuelezea mwitikio huu ni, ‘cephalic phase response'. Mwitikio huu wa kulazimishwa unakuja kujengwa kama matokeo ya mazoea ya muda mrefu kwa radha zenye utamu zinazoambatana na utambulishaji wa nguvu mpya ndani ya mwili.


Wakati radha zenye utamu zinaposisimua katika ulimi, ubongo unaliamuru Ini kujiandaa kupokea nguvu mpya (sukari) kutoka nje. Ini nalo litasimama kutengeneza sukari toka hifadhi ya protini na wanga ya mwili, na kuanza kuhifadhi nishati ya kimetaboli inayozunguka kwenye mzunguko wa damu.

Kama Michael G Tardoff, Mark I Friedman na wanasayansi wengine, wameonesha kuwa ‘cephalic phase' huwa na matokeo ya kuongeza shughuli za kimetaboli ili kuhifadhi lishe, nishati inayopatikana kwa ajili ya mabadiliko hupungua na kusababisha kuongezeka kwa njaa.

Ikiwa ni sukari hasa ndiyo inayosisimua ulimini, matokeo kwenye ini yatakuwa ni urekebishaji wa hicho kilichoingia mwilini. Ingawa ikiwa radha ya utamu haina lishe ndani yake, hisia za kutaka kula zitakuwa ndiyo matokeo yake. Ni Ini ndilo linalotengeneza hisia za kula. Kadiri radha utamu bila kalori ndani yake zinavyosisimua kionjea radha, vivyo hivyo zinavyokuja zaidi hisia za kutaka kula.


Matokeo ya ‘cephalic phase' kwa radha za utamu yamethibitishwa katika majaribio kwa wanyama kwa kutumia ‘saccharin' (dawa yenye utamu kama sukari). Kwa kutumia aspartame, wanasayansi kadhaa wameonesha matokeo yanayofanana ya kutaka kula kupita kiasi kwa binadamu.


Blundel na Hill wameonesha kuwa viongeza utamu visivyo na kalori hasa aspartame huongeza njaa na kuongeza uchukuaji wa chakula kwa muda mfupi. Wanaripoti, "baada ya kunyweshwa aspartame, wapendwa waliachwa na njaa iliyobaki ikilinganishwa na walivyoachwa baada ya Glukozi. Njaa hii iliyobaki husababisha kuongezeka kwa matumizi ya chakula".


Tardoff na Friedman wameonesha kuwa hisia hizi za kutaka kula zaidi chakula baada ya viongeza utamu vya kutengenezwa vimetumika, zinaweza kudumu mpaka dakika 90 baada ya kinywaji kitamu hata wakati majaribio yote ya damu kuonesha thamani ya kawaida. Wameonesha kuwa hata wakati usawa wa damu kwa insulini, usawa wa juu ambao unafikiriwa kuwa unasababisha njaa, umefikia usawa wa kawaida, majaribio kwa wanyama yameonesha hitaji la kutaka kula zaidi ya udhibiti.


Hii inamaanisha kwamba ubongo unashikilia kwa muda mrefu zaidi hisia za kutaka kula inapotokea tezi za kuhisia sukari zimesisimuliwa bila sukari kuwa imeingia kwenye mfumo. Radha utamu husababisha ubongo kuliamuru ini kuhifadhi ziada badala ya kuitumia toka katika akiba za mwili.

Kimsingi, mwitikio huu wa kifiziolojia kwa viongeza utamu bila kuwa na kalori ambazo mwili unazitumainia, unamlazimisha mtu kutafuta kalori hizo kokote na hatimaye kuhitaji kula.

Wakati kafeina na aspartame vimeingia mwilini, huanza kuonesha (dictates) matokeo yake ya kusisimua kwenye fiziolojia ya seli kwenye ubongo, kwenye ini, kwenye figo, kwenye kongosho, kwenye tezi mbalimbali na kadharika.


Aspartame hubadilishwa kuwa ‘phenylalanine' na ‘aspartate', zote huwa na matokeo ya moja kwa moja ya usisimuaji kwa ubongo. Kwa haraka matokeo ya kafeina na aspartame yanajenga namna mpya za kazi kwa ubongo, kwa sababu vinapatikana kwa kujirudia kwa kiasi kikubwa zaidi ya kile ambacho pengine kingeleta usawa wa kifiziolojia.


Transimita nyurolojia zilizo nyingi, ni mazao ya pili kutoka moja au asidi amino zingine. Hata hivyo aspartate ni moja kati ya jozi ya asidi amino za pekee ambazo hazihitaji kubadilishwa kuwa zao la pili ili kufanya kazi kwenye ubongo. Kuna nukta zinazopokea (receptors) hizi asidi amino mbili kwenye neva seli maalumu ambazo huathiri fiziolojia ya mwili haraka zaidi.


Matumizi ya viongeza utamu kwa usisimuaji wake wa kimakosa wa miishio ya neva ambayo husajili usambazaji wa kuingia wa nguvu kwenye mwili, yana matokeo mengine zaidi yasiyotarajiwa zaidi ya kusababisha kuongezeka uzito kupita kiasi.


Kwa muda wote, kemikali hizi zinaning'inia kwenye fiziolojia ya mwili kwenye mwelekeo unaoamuliwa na mfumo wa neva zinazozisisimua. Matumizi yake bila uelewa wa matokeo yake ya muda mrefu mwilini sababu tu yanasisimua tezi za radha, bado hayajaainishwa.


Utafiti umeonesha kuwa mapokezi ya aspartame yanapatikana pia kwa baadhi ya mifumo ya fahamu ambayo matokeo yake husisimua pia ogani za uzazi na matiti. Usisimuaji wa kudumu kwa tezi za matiti bila sababu nyingine zinazohusiana na ujauzito, unahusishwa kama moja ya sababu za kuongezeka kwa saratani ya matiti kwa wanawake.


Homoni iitwayo prolactini ndiyo inahusika zaidi katika mwelekeo huu. Moja ya vitu ambavyo havijafanyiwa utafiti wa kutosha juu ya madhara ya aspartame, ni matokeo yake ya madhara yanayoweza kupelekea kutokea kwa saratani ya ubongo. Majaribio kwa panya na wanyama wengine, yote yameonesha aspartame kuhusika kutengeneza uvimbe kwenye ubongo.


Dr.H.J.Roberts ameyaainisha baadhi ya matatizo ya kiafya yanayosababishwa na aspartame, na kuyaita yote kwa pamoja kama, ‘magonjwa ya aspartame', katika kitabu chake; "Breast Implants or Aspartame Diseases?", ameyataja baadhi ya magonjwa kama vile kuumwa kichwa, kizunguzungu, kukosa usingizi, kuchanganyikiwa, kupoteza kumbukumbu, uchovu sugu, kushuka kwa damu sukari, maumivu ya maungio, nywele kupotea, na kadharika, kama ni magonjwa yasababishwayo na aspartame. Ameandika makala na vitabu vingine vingi juu ya mada hii.


Sayansi ya sasa ya kudhibiti kuongezeka uzito kupita kiasi inayohusisha ukatazaji wa baadhi ya vyakula, hata kama baadhi ya kilo zitapungua, zitaongezeka tena baada ya muda mfupi. Cha kushangaza zaidi ni fasheni mpya inayojitokeza siku hizi, mtu anakuwa mtumwa wa kuchagua chakula hiki au kile kama mbwa mnusaji hasa katika suala la helemu (cholesterol).


Usishituke!, "tofauti na imani iliyojengeka ya kupunguza au kuondoa kabisa matumizi ya mayai katika milo yetu, mimi nakula mayai mengi nitakavyo – dr.Batmanghelidj". Mayai yana protini nzuri iliyosawazishwa. Anasema, anaelewa pia ni namna gani utengenezwaji wa kolesteroli unavyohusiana na upungufu wa muda mrefu wa maji mwilini (prolonged dehydration).


Ikumbukwe kuwa, kafeina ni dawa ya kulevya (addictive drug) ambayo matumizi yake yamehalarishwa. Watoto wadogo kwa upande wao wanatokea kuwa wategemezi kirahisi zaidi kwa vinywaji vyenye kafeina. Hii ndiyo sababu ya kwanza watoto wengi mashuleni siku hizi hawafundishiki, tunabaki kuwalaumu bure.


Usisimuaji huu wa miili kwa vinywaji vyenye kemikali kwa watoto, hupelekea baadhi yao kuwa wategemezi wa madawa ya kulevya makubwa zaidi wakati wanapokuwa wakubwa.


Kama tulivyofafanua muda wote, mwili hutoa ishara anuwai unapokuwa na maji chini ya kiwango. Wakati huu (uzito unapozidi), mwili unakuwa unahitaji maji pekee. Mwili unaanza kuchanganya habari wakati mtu anapoamua kutumia vinywaji vya kutengenezwa kama mubadala wa mahitaji ya mwili kwa maji.


Kwa hiyo, utumiaji wa muda mrefu na wa kudumu wa soda, lazima uchukuliwe kama moja ya visababisho vya matatizo mengi ya kiafya katika jamii zetu.
 
sio kweli,baadhi zilizopo hapo ni za uongo na zimekaa kisda sana,hazina ushahd wa kisayansi,ziko kwa kufikirika,acheni kudanganya watu.

Soda na Juisi za viwandani huharibu KINGA YA MWILI

9162214-set-of-refreshing-soda-drinks-in-metal-cans.jpg


Namna vinywaji baridi/soda na juisi za viwandani vinavyochangia kuharibu mfumo wa kinga ya mwili:

Gugumia-gugumia-gugumia! Mmm …ahhh! (lazima ujilambe midomo) hakuna kinachoenda chini vizuri zaidi ya soda yako uipendayo wakati ukijipatia msosi wako iwe mchana au usiku au chakula chako kingine chochote feki (junk foods), lakini nini kinga yako ya mwili inaweza kusema kuhusiana na uamuzi wako wa kunywa vinywaji hivi baridi vyenye kaboni?.

Nini? Vinywaji hivi vyenye kaboni (carbonated drink) vina gesi ya Kabonidaioksaidi (CO2) ndani yake. Nini inafanya ndani ya mwili wako hii gesi ya kabonidaioksaidi?.

Unaweza ukajidhania ni kwa mara moja moja tu ndiyo wewe hunywa soda, pengine mara moja kwa wiki au pengine zaidi ya mara moja kwa wiki, lakini nani anakaa kuhesabu amekunywa soda ngapi? ikiwa utaamua kufanya hesabu ni chupa ngapi za soda unakunywa kwa wiki mara mwaka mmoja hasa wakati wa misimu ya sikukuu, unaweza kupatwa na mshituko wa idadi ya soda ulizokunywa!

Ni hivi, sisi binadamu huwa tunavuta ndani ya mwili hewa ya oksijeni na kutoa nje hewa chafu ambayo ni sumu pia ijulikananayo kama kabonidaioksaidi. Cha kushangaza ni kuwa katika soda huwa tunakuwa tunaingiza ndani ya mwili hewa ya kabonidaioksaidi ambayo tulipaswa ndiyo tuwe tunaitoa nje kama uchafu/sumu!

Swali: Ni muda unatakiwa kunywa soda?

Jibu: Unapokuwa jangwani na umekaukiwa maji huku kila unakogeuka hakuna kinywaji kingine, ndipo unaweza kunywa soda!

Mwanzoni mwa mwaka huu 2013, kampuni kubwa duniani ya uzarishaji wa vinywaji hivi baridi maarufu kama Coca-cola, imekiri hadharani kuwa huwa wanaongeza kilevi (alcohol) ndani ya soda yao ya coca- cola kiasi cha aunsi 8, na kwa mara ya kwanza wakatoa hadharani fomula yao wanayotumia kutengeneza kinywaji hicho!!!. Unataka makala hii ikudanganye nini tena?

Naamu, Sasa tuone nini kinatokea ndani ya miili yetu na katika kinga yetu ya mwili unapokuwa umekunywa kinywaji chenye kaboni ndani yake. Jambo la kwanza kabisa, kama ni kiywaji ambacho kimeongezwa zigo la sukari, ini lako na tishu za mishipa vitaihifadhi baadhi sehemu ya hii sukari katika mfumo wa glycogen. Kisha kongosho lako litaanza kuipampu insulini kwenye mishipa yako ya damu ambayo huiondoa zaidi glukozi iliyozidi na kuibadili kuwa mafuta kwa ajili ya kuihifadhi. Ikiwa kiasi chako cha mafuta katika damu (triglycerides) tayari ni kikubwa, basi kitendo hiki kitakuwa na madhara hasi zaidi juu ya afya ya moyo wako.

Kwa upande mwingine iwapo soda unywayo imeongezwa vitu vingine kama ‘aspartame', ‘Acesulfame potassium' au ‘Sucralose' basi hbari huwa ni mbaya zaidi. Kila kimojawawapo ya vilivyotajwa hapo ni kemikali zinazoathiri kemia ya mwili wako na ni visababishi vikubwa vya ugonjwa wa kansa.

Ugomvi uliopo hapa umegawaganyika katika makundi kadhaa, kwahiyo hebu tuendelee tuone ni wapi inakoenda hii gesi ya kabonidaioksaidi katika mwili wako na matatizo yatakayoileta katika kinga ya mwili wako. Wakati chakula na kinywaji kinameng'enywa hupita tumboni kupitia valvu iitwayo ‘pyloric valve' na kisha katika duodeni/mbuti (duodenum) ambayo ni sehemu ya kwanza ya utumbo mdogo. Unaweza ukawaza ikiwa gesi ya kabonidaioksaidi iliundwa kwa njia hii ni lazima iwe na madhara hasi katika mfumo wa kinga yako ya mwili, kwa jinsi gani lakini? Gesi hii huendelea kujishikiza pembeni mwa ukuta wa utumbo mdogo na kukizuia chakula kinachopita ili kisimeng'enywe na hivyo kupunguza uwezekano wa viinilishe mhimu vilivyomo kwenye chakula kuweza kuchukuliwa na kutumika na mwili jambo linalopelekea kuathiri kinga ya mwili na kinga hubaki imechezewa hivi mpaka masaa 24! Na mbaya zaidi usawa wako mzuri wa potential hydrogen (ph) wa 7.36 huathiriwa vibaya sana na kuifanya damu yako kuwa na asidi zaidi na kuwa nzito!

Kingine kibaya kilichopo katika vinywaji hivi baridi ni ‘phosphoric acid' ambayo yenyewe husababisha kupotea au kupungua kwa madini ya kalsiamu toka mwilini mwako na kupelekea uharibifu wa mifupa na kuifanya milegevu na kuharibu mifupa kuweza kujitengeneza au kujiimarisha upya, hii hujumuisha pia kulika kwa fizi na kuharibu meno, kwahiyo kwa kifupi soda zinaathiri kubwa sana upande wa mifupa.

Angalizo linalotolewa hapa ni kuhakikisha kuwa endapo unajihisi kinga yako ya mwili inaanza kuporomoka basi ni vema ukakaa mbali na vinywaji vyote baridi vya viwandani vikijumuisha soda za aina zote na juisi zote za viwandani hadi hapo kinga yako itakapoimarika tena.
 
sio kweli,baadhi zilizopo hapo ni za uongo na zimekaa kisda sana,hazina ushahd wa kisayansi,ziko kwa kufikirika,acheni kudanganya watu.

[h=2]Health Effects of Soda Consumption[/h]
I've been warning readers of the dangers of soda since I started this site, well over a decade ago. Since then, science has caught up; now definitively showing the profound health risks of this popular beverage.


Amazingly, as of 2005, white bread was dethroned by soft drinks as the number one source of calories in the American diet! I keep repeating that statistic because I find it so incredible. According to recent statistics, Americans consume close to 50 billion liters of soda per year, which equates to about 216 liters, or about 57 gallons per person. That equates to a staggering amount of sugar!


Play-By-Play of what Happens in Your Body when You Drink a Soda


Soda is on my list of the five absolute worst foods and drinks you can consume. The video above offers a compelling illustration of why I make this claim.


In it, reporter Yunji DeNies drinks a 20-ounce glass of cola, which contains the equivalent of 16 teaspoons of sugar in the form of high fructose corn syrup (HFCS). This is nearly three times the maximum daily sugar intake recommended by the American Heart Association.


HFCS typically contains a mixture of 45 percent glucose and 55 percent fructose (although recent investigations have found that many brand-name sodas actually contain 65 percent fructose!).


Once ingested, your pancreas rapidly begins to create insulin in response to the sugar. The rise in blood sugar is quite rapid. Here's a play-by-play of what happens in your body upon drinking a can of soda:


Within 20 minutes, your blood sugar spikes, and your liver responds to the resulting insulin burst by turning massive amounts of sugar into fat.

Within 40 minutes, caffeine absorption is complete; your pupils dilate, your blood pressure rises, and your liver dumps more sugar into your bloodstream. As you could see in the report above, DeNies' blood glucose level was 79 at the outset of the experiment, and after 40 minutes it had risen to 111!

Around 45 minutes, your body increases dopamine production, which stimulates the pleasure centers of your brain – a physically identical response to that of heroin, by the way.
After 60 minutes, you'll start to have a blood sugar crash, and you may be tempted to reach for another sweet snack or beverage.

As I've discussed on numerous occasions, chronically elevated insulin levels (which you would definitely have if you regularly drink soda) and the subsequent insulin resistance is a foundational factor of most chronic disease, from diabetes to cancer.


Fructose Turns into Fat Far Faster than Other Sugars, and Fats


Lately, the media has finally begun reporting on the science of fructose, which clearly shows it is far worse than other sugars.


Fructose is processed in your liver, and unlike other sugars, most of it gets shuttled into fat storage. This is why fructose is a primary culprit behind obesity-far more so than other sugars. According to the news report above, drinking two bottles of soda per day can make you gain a pound of fat per week!


Aside from the weight gain, eating too much fructose is linked to increased triglyceride levels. In one study, eating fructose raised triglyceride levels by 32 percent in men! Triglycerides, the chemical form of fat found in foods and in your body, are not something you want in excess amounts.


Intense research over the past 40 years has confirmed that elevated blood levels of triglycerides, known as hypertriglyceridemia, puts you at an increased risk of heart disease.


Meanwhile, one of the most thorough scientific analyses published to date on this topic found that fructose consumption not only leads to insulin resistance but also decreases leptin signaling to your central nervous system. Leptin is responsible for controlling your appetite and fat storage, as well as telling your liver what to do with its stored glucose.


When your body can no longer "hear" leptin's signals, weight gain, diabetes and a host of related conditions may occur. So, as you can see, fructose contributes to poor health through a number of mechanisms...


What Else is in Soda?


Before you grab that next can, take a look at some of the major components found in most sodas:


High fructose corn syrup: When you eat 120 calories of glucose, less than one calorie is stored as fat. 120 calories of fructose, on the other hand, results in 40 calories being stored as fat. Consuming fructose is essentially consuming fat!


The metabolism of fructose by your liver creates a long list of waste products and toxins, including a large amount of uric acid, which drives up blood pressure and causes gout.


Fructose also interferes with your brain's communication with leptin, resulting in overeating.


Benzene. While the federal limit for benzene in drinking water is 5 parts per billion (ppb), researchers have found benzene levels as high as 79 ppb in some soft drinks, and of 100 brands tested, most had at least some detectable level of benzene present.
About 150 empty calories, most of which will turn into fat Phosphoric acid, which can interfere with your body's ability to use calcium, leading to osteoporosis or softening of your teeth and bones.

Between 30 to 55 mg of caffeine, which can cause jitters, insomnia, high blood pressure, irregular heartbeat, elevated blood cholesterol levels, vitamin and mineral depletion, breast lumps, birth defects, and perhaps some forms of cancer. Aspartame: This chemical is used as a sugar substitute in diet soda. There are over 92 different health side effects associated with aspartame consumption including brain tumors, birth defects, diabetes, emotional disorders and epilispsy/seizures.
Artificial food colors, including caramel coloring, which has recently been identified as carcinogenic. The artificial brown coloring is made by reacting corn sugar with ammonia and sulfites under high pressures and at high temperatures.


This produces the chemicals 2-methylimidazole and 4-methylimidazole, which have been found to cause lung, liver and thyroid cancer in lab rats and mice.


Tap Water: I recommend that everyone avoid drinking tap water because it can carry any number of chemicals including chlorine, trihalomethanes, lead, cadmium, and various organic pollutants. Tap water is the main ingredient in bottled soft drinks.
Sulfites. People who are sulfite sensitive can experience headaches, breathing problems, and rashes. In severe cases, sulfites can actually cause death. Sodium benzoate, a common preservative found in many soft drinks, which can cause DNA damage. This could eventually lead to diseases such as cirrhosis of the liver and Parkinson's.
Health Effects of Soda Consumption


After looking at the list above, is it any wonder that a number of studies have now linked soda consumption with obesity and related health problems?


One such independent, peer-reviewed study published in the British medical journal The Lancet found that 12-year-olds who drank soft drinks regularly were more likely to be overweight than those who didn't. In fact, for each additional daily serving of sugar-sweetened soft drink consumed during the nearly two-year study, the risk of obesity jumped by 60 percent!


As mentioned earlier, soda clearly elevates your insulin levels, and elevated insulin levels are the foundation of most chronic disease. Not only does drinking just one soda per day increase your risk of diabetes by 85 percent, it also increases your risk of:


Heart disease
Cancer
Arthritis
Osteoporosis
Gout
Non-alcoholic fatty liver disease (NAFLD)
One of the Simplest Ways to Radically Improve Your Health


By now you probably know what that is...


Quit drinking soda.


Eliminating soft drinks is one of the most crucial factors to address many of the health problems you or your children suffer. Again, this is because normalizing your insulin levels is one of the most powerful physical actions you can take to improve your health and lower your risk of disease and long-term chronic health conditions.


Pure water is a much better choice, or if you must drink a carbonated beverage, try sparkling mineral water with some lime or lemon juice.


If you struggle with an addiction to soda, (remember, sugar is actually more addictive than cocaine) I strongly recommend you consider Turbo Tapping as a simple yet highly effective tool to help you stop this health-sucking habit. Turbo Tapping is a simple and clever use of the Emotional Freedom Technique, designed to resolve many aspects of an issue in a concentrated period of time.
 
Kama utakuwa na swali jingine unaweza kunitumia hata kwenye PM tukamalizana fresh tu!

sio kweli,baadhi zilizopo hapo ni za uongo na zimekaa kisda sana,hazina ushahd wa kisayansi,ziko kwa kufikirika,acheni kudanganya watu.
 
Nikweli vinywaji vina madhara. Sio hivyo tu mi nishaona mafundi magari wakimwagia kwenye nut yenye kutu, baada ya muda nut ilifunguka kwa urahisi. Je kwa binadamu itakuaje?

Binadamu na chuma chenye kutu ni vitu viwili tofauti kabisa chemically.
 
pia inasemekana kuwa vinywaji aina ya peps, cocacola, m dew, mirinda, sprite, 7up, fanta na vingine vina kichangamshi kiitwacho coke ambayo inasisimua mwili ili utengeneze kemikali iitwayo cyanide, cyanide husababisha cell za kongosho(pancrease), islet of lang han kushindwa kufanya kaz vizuri hivyo kushindwa kutengeneza insulin, baadaye kisukari huanza.
 
10151782_10153941933245198_315440756_n.jpg


SODA NI SUMU

*Utafiti wabaini ina kiwango kikubwa cha kemikali hatari mwilini mwa binadamu

AFYA za mamilioni ya Watanzania wanaotumia vinywaji vya aina ya soda ipo hatarini, baada ya kugunduliwa uwepo wa chembechembe zenye kemikali za sumu ndani ya vinywaji hivyo, MTANZANIA Jumatano linaripoti.

Utafiti uliofanywa na Muungano wa Waandishi wa Habari za Uchunguzi Tanzania (Investigative Journalists Union of Tanzania- IJUTA) pamoja na tafiti zilizofanywa na wataalamu waliobobea katika afya ya umma duniani, umebaini kuwa vinywaji baridi aina ya soda ni hatari kuliko utumiaji wa sigara inayosababisha maradhi ya kansa katika mwili wa binadamu.
Kwa mujibu wa utafiti wa wanasayansi mbalimbali duniani, yapo madhara makubwa ya utumiaji wa vinywaji vya aina ya soda katika mwili wa binadamu.

Utafiti huo unaonyesha kuwa zipo sababu nane kuu zinazokiweka kinywaji aina ya soda kwenye kundi la vinywaji vyenye sumu ambavyo havifai kwa matumizi ya binadamu.

IJUTA imebaini kuwa makampuni makubwa yanayotengeneza vinywaji baridi aina ya soda yanatumia mabilioni ya dola kila mwaka kujitangaza na kutoa misaada ya kijamii kutokana na mauzo yake, bila kutaja madhara ya vinywaji hivyo kwa binadamu.

Kwamba matangazo hayo yanayogharimu mamilioni ya fedha ndiyo yanayokifanya kinywaji hicho kuwa maarufu zaidi duniani, licha ya kuwa na madhara makubwa katika mwili wa binadamu.

Aidha, utafiti huo unaonyesha kuwa umaarufu mwingine wa kinywaji aina ya soda ni utamu wa kupindukia ulio ndani ya soda.

Utafiti wa IJUTA unaonyesha kuwa utamu wa kupindukia iliomo ndani ya soda unawapumbaza wanywaji ili wasisikie ladha kali ya asidi iliyomo ndani ya soda.

IJUTA imegundua kuwa kiwango cha asidi kilicho ndani ya soda hakiwekwi wazi kwa walaji kwa sababu ya kuhofia kuwa wakibaini wataacha kikutumia kinywaji hicho.

Inaelezwa pia kuwa madini ya cola yaliyo ndani ya soda yana kilevi aina kafein kinachomteka mnywaji kuwa teja wa kinywaji hicho.

Tafiti za kitaalamu zimeonyesha kuwa soda inahusishwa na matatizo mengi ya kiafya kwa watoto na watu wazima, yakiwemo matatizo ya kuongezeka unene kupita kiasi, ugonjwa wa ini na mengineyo.

Utafiti uliofanywa nchini Marekani unaonyesha kuwa soda huwekewa ‘fructose' (sukari) nyingi kupitia mfumo wa sirapu (fructose corn syrup) ambayo inaongoza kwa kusababisha magonjwa ya unene, kisukari, ugonjwa wa moyo na magonjwa mengine sugu yanayowakabili Wamarekani wengi hivi sasa na dunia kwa ujumla.

Dk. Mercola, ambaye ni mtaalamu wa masuala ya lishe asilia na tiba mbadala nchini Marekani, amekaririwa na tafiti mbalimbali zilizofanyika nchini humo akieleza kuwa kinywaji aina ya soda ni hatari kwa binadamu, sawa na mtu anayevuta sigara au zaidi, jambo alilosisitiza kuwa siyo la kutia chumvi, bali ukweli halisi.

Watumiaji wa vinywaji aina ya soda wanaelezwa kuwa wamekuwa wakinywa kiasi kikubwa cha kaboni, kafeini (dawa ya kulevya), sukari ya kupundukia na asidi kali ambayo huvuruga afya ya mtumiaji kwa kiwango cha juu.

Soda pia imebainika kutokuwa na lishe ya aina yoyote zaidi ya maji na sukari.

Uchunguzi wa IJUTA na utafiti ya wanasayansi mbalimbali duniani, umeonyesha kuwa watu wengi hawajui kuwa unywaji wa soda huwaongezea kiasi kikubwa cha madini joto.

Chupa moja ya soda yenye ujazo wa mililita 330 husababisha unene kwa kiwango cha paundi moja kwa mwezi.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Kisukari Tanzania (TDA), Ramadhan Mongi, amepata kukaririwa na vyombo vya habari hapa nchini akieleza kuwa ugonjwa wa kisukari Tanzania umeongezeka mara sita katika siku za hivi karibuni.

Alisema miaka kumi iliyopita, hali ya kisukari ilikuwa asilimia tatu (3), lakini katika miaka ya karibuni umeongezeka mara sita.

"Tunastahili kuongeza jitihada ya kupambana na gonjwa hili la kisukari kwa gharama zote kwa sababu kisukari ni moja ya magonjwa manne yanayomaliza Watanzania," alisema.

Utafiti uliofanyika Mkoa wa Dar es Salaam ulibaini kwamba kati ya watu watano waathirika wa kisukari, mmoja tu ndiyo hupata matibabu ya serikali.

Unywaji kwa mpigo wa kabohaidrets iliyo na sukari nyingi kwenye soda hudhoofisha seli zinazozalisha vimeng'enya tofauti na vyakula vingine na pia imebainika kuwa sukari ikiingia kwa wepesi kwenye mzunguko wa damu husababisha kongosho kuzalisha vimeng'enya vingi mwilini.

Uchunguzi wa kitabibu katika Hospitali ya wanawake ya Boston nchini Marekani na katika Chuo cha Kitabibu cha Harvard umeonyesha wanawake 51,000 hawakuwa na kisukari mwanzoni mwaka wa 1991, lakini miezi minane baadaye wanawake 741 waligundulika na kisukari.

Ripoti ya utafiti huo ilionyesha kuwa wanawake waliokuwa wakitumia kinywaji aina ya soda moja ama mbili kwa siku waliongezeka uzito maradufu na walikuwa hatarini kupata ugonjwa wa kisukari.

Pia ilionyesha kuwa soda hudhoofisha mifupa na husababisha hali ya mifupa kupuputika, hali inayomuweka mtumiaji kuwa katika hatari ya kuvunjika mifupa kirahisi.

Madhara mengine yaliyobainika kusababishwa na unywaji soda ni kupukutika kwa meno na ama kuoza. Pia soda husababisha matatizo ya figo.

Soda yenye chembe ya cola husababisha figo kuwa na mawe kwa sababu ya asidi na kemikali mbalimbali zinazofichwa vipimo vyake kwa walaji.

Madaktari bingwa wa wanamichezo wanaeleza madhara yanayosababishwa na soda mwilini kuwa ni pamoja na shinikizo la damu, uharibifu wa ini, huvurugu mfumo wa kumeng'enya chakula tumboni kutokana asidi ya kiwango cha juu iliyo kwenye soda.

Wanashauri kuwa soda haistahili kutumika kama kishawishi kwenye mchezo, kwa sababu ina madhara makubwa kwa wanamichezo kwa sababu hunyonya maji kwenye mwili na kudhoofisha mwili.

Wakati utafiti huo ukidhihirisha hayo, Taasisi ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) imeshindwa kutoa tamko lolote kuhusu utafiti huo, hata baada ya kupelekewa maswali kwa maandishi yanayoomba ufafanuzi wa ubora wa vinywaji vya soda katika mwili wa binadamu.

Toa Maoni yako kwa habari hii
 
Leo nmetumiwa video ikionesha hatariii na madhara ya soda asee wakuu acheni kunywa soda, vinginevyo wakati unakunywa andaa na bajeti ya matibabu, nmeshindwa kui attach, mwenye nayo ataiweka,,,,

Ila wakuu soda mmmm basi
 
Me ninayo video siwezi kuattach nimeitafakari nikaona ni kweli soda ni sumu 100% soma ingredients zake hakuna hata chembe ya chochote kinachotoka kwenye soda kikasaidia mwilimi upande wa pili inaweza kuwa ni mbinu ya kibiashara kwani video inaonesha madhara ya kampuni moja tu
 
Me ninayo video siwezi kuattach nimeitafakari nikaona ni kweli soda ni sumu 100% soma
ingredients zake hakuna hata chembe ya chochote kinachotoka kwenye soda kikasaidia mwilimi upande wa pili inaweza kuwa ni mbinu ya kibiashara kwani video inaonesha madhara ya kampuni moja tu
Mkuu nmejarib kuattach bt inagoma, ila kiukweli soda n tatzo kubwa,
 
Wengine hapa tunawazia mihela wengine wanapigia hesabu soda
 
Korea ya kusini hasa Seoul bei ya soda ni kubwa kuliko ya bia na yote ni kudiscourage matumizi ya soda
 
Nimeshatupia Pepsi kama nne had asaiv kwa wiki napiga cret zima nikihesabu duuuh izo sumu nilizonazo ss shida
 
Back
Top Bottom