Hakuna mahali ambapo dhuluma iliwahi kushinda. Kwa kafiri tunavyoenda, hali itazidi kuwa mbaya zaidi.
Madhara ya utawala mbaya wa awamu ya 5, yataanza kuonekana kwenye utawala wa awamu ya 6, na yataendelea kulitafuna Taifa kwa muda usipinvua miaka 15.
Kutoka tulipo na kuzyia mambo mabaya zaidi kutokea:
1) Tuwe na bunge lililotokana na matakwa ya wananchi. Kilichopo sasa, kinachoitwa Bunge, ni genge la wahalifu ambao waliteuliwa na marehemu Magufuli kwa matakwa na vigezo vyake. Robo tatu ya waliomo kwenye hilo genge, hata kwenye kura za maoni ndani ya CCM, hawakushinda.
2) CCM iondoke kutoka kuwa genge la wauaji (greenguards wengi ndio hao wasiojulikana. Kazi yao ni ku-terrorize watu. Kwa maana ya ugaidi, CCM ni kikundi chenye sifa za kigaidi), na kuwa chama cha siasa, kinachoheshimu matakwa ya wananchi.
3) Mahakama na Bunge ziwe mihimili kamili ya dola kuliko kuwa idara za CCM na Serikali.
4) Jeshi la polisi liundwe upya ili kulibadili kutoka kuwa genge la uhalifu dhidi ya wananchi na Jamhuri na kuwa chombo cha kulinda raia, kulinda haki za kiraia, haki za vyama vya siasa, haki za vyombo vya habari na ulinzi wa mali za za wananchi na umma.
5) Ofusi ya msajili wa vyama, tume ya uchanguzi, zifutwe na kuundwa upya baada ya kutungiwa sheria mpya.
6) Sheria zote za kigaidi kama zile za vyama vya siasa, vyombo vya habari, sheria ya mitandao, sheria zinazoruhusu DC na RC kuwaweka watu ndani, zifutwe
7) Makosa yote yawe na dhamana isipokuwa makosa ya mauaji tu.
8) Itungwe sheria ya kudhibiti matumizi mabaya ya vyombo vya dola ambao anayetoa amri na anayetekeleza, ikithibitika walifanya kwa uonevu na kwa kudhamiria, wahusika wote watumikie jela, hii ikiwa ni pamoja na polisi wanaowabambikia watu kesi.
5)