Binafsi kabla ya kuandika chochote au kutuhumu mtu flani sababu ya matendo yake lazima uwe na critical thinking,unatakiwa kufanya arguments za kutosha,unatakiwa kutuliza nafsi yako vya kutosha,unatakiwa kudhibiti emotions kwa kiwango cha juu sana,lazima uwe mtu ambae hana chuki na mtu yoyote,lazima uwe mtu mwenye uimara wa kudhibiti mihemuko ndo watu watakuelewa.
Kila mtu ni kichaa kwa jinsi ya maumbile yake,sema hatukujua na hatuwezi kujua kiwango cha ukichaa wako sababu hujapata nafasi ya kuwatumikia watu wakakutathimini akili yako na uwezo wako wa kuwatumikia, inawezekana wewe una kichaa zaidi ya uliyemtuhumu ila sababu hatujaona ukichaa wako hatuwezi kukufahamu.
Kihistoria sijui kama unaifahamu vizuri familia ya Magufuli,sijui hata kama unafahamu ukoo wa Magufuli, lakini sababu ya chuki zako binafsi unaweza ongea chochote utakacho labda sababu ya kufurahisha watu au ugomvi wako binafsi juu ya kitu flani.