Madhara ya Utawala wa Awamu ya Tano yameanza kulitafuna taifa; Nani wa kulaumiwa?

Madhara ya Utawala wa Awamu ya Tano yameanza kulitafuna taifa; Nani wa kulaumiwa?

Ndugu zanguni habari za asubuhi.

Ni shahiri dhahiri sasa tumeanza kuvuna tulichopanda.

Sio mkubwa wala mdogo. Mwenye cheo wala asiye na cheo, tajiri wala maskini sote tumeanza kuonja joto la Jiwe.

Hali ni tete. Sio polisi sio Raia. Sio mtuaji sio mteuliwa. Amani, Umoja, utulivu, heshima vimeanza kuteteleka.

Tatizo lilianzia Awamu ya tano. Ambapo utawala wa sheria, haki na kuzingatia misingi ya demokrasia, uwazi na usawa havikuzingatiwa kabisa.

Ni katika utawala wa awamu ya tano ndipo Tulishuhudia kwa kiwango kikubwa Mtanzania anayepigania haki au kuhamasisha umoja na maelewano alikuwa akipingwa na kupigwa hapa na pale. Dhulma ikawa kila mahali. Kwa matajiri na kwa Maskini.

Mimi binafsi naweza kuvilaum vyombo vyenye mamlaka na vilikuwa na uwezo wa kukinga yasitokee

Kwa mfano. Vyombo vya dola Polisi, Mahakama, Usalama na jeshi la nchi viliwezaje kuruhusu watu kuvunjiwa haki zao kwa maslahi ya wanasiasa wachache??

Kwa mfano umtufikirie kesi 147 zilizosemwa na Rais pamoja na Boss qa Takukuru kuwa zilibambikiwa na kusababisha uhasama mkubwa miongoni mwa jamii, kati ya jamii na polisi na hatimaye na serikali yao.

Mfano wa pili ni tukio baya kabisa kuwa kutoke ktk mfumo wa siasa zetu ambapo mwaka 2020 oktoba Uchaguzi ulivurugwa kuanzia mchakato wa utungwaji wa sheria ya uchaguzi na vyama vya siasa na hatimae mchakato wenyewe wa uchaguzi na hata upitishwaji wa wagombea. Najiuliza hili lilifanyika kwa faida ya nani? Usalama wetu tunaouamini kwa maslahi ya nchi hawa kuanticipate madhara ya matukio yale? Polisi je? vipi Mahakama?

Sasa tunaona madhara yake Tozo, maiamala, uhaba wa ajira, uchumi mbovu na sasa hali mbaya ya mufukoni mwa watu.

Tumeanza kuona watu wakipromote uhasama dhidi ya serikali yao. Tukio la Mauwaji ya juzi pale Salenda ni la kusikitisha. Tena likidaiwa kutekelezwa na Mtu anayedaiwa kuqa ni Kada wa chama cha mapinduzi. Hawa vijana wa Chama cha mapinduzi bila kumung'unya maneno walilelewa na kudekezwa vibaya chini ya mwamvuli wa MATAGA. Hili ni kundi kubwa lililokuwa linahisiwa kufanya uhalifu sehemu mbali mbali za nchi. Ilikuwa si ajabu Kutishiwa na vijana hawa kuwa watakupoteza au wanakwambia kabisa tutakubinya ukose mahali pa kwenda na hwakufanywa chochote na mtu yeyote. Sasa Chatu anamla aliyemfuga.

Sasa nini tufanye.

Tuepuke migogoro inayokwepeka. Mahakama zitende haki, Polisi watende haki. Wadhibiti uhalidu kweli kweli. Usalama wafanye kazi yao kweli kwelikweli. Wenye mamlaka tunawakumbusha tu kuwa Hali ikiwa mbaya nchi hii na wao hawataishi kwa amani.

Tumeona wale tuliowaita mabeberu sasa wanafungasha vilago. Matishio ya ugaidi kwa mujibu qa IGP sasa yameibuka tena.

Haya ni madhara ya utawala usiozingatia sheria, katiba na haki za binadamu.

Asalaam Ale ykum
Porojo nyingi hazisaidii , umakini zaidi unahitajika.
 
Maliza kutype kisha ukalipe kodi ya Jengo! Pumbavvv.... Mlizoea kumtupia lawama JPM sasa hakuna wa kumtupia lawama sio!? Kazi inaendelea! Hakuna miradi mipya,tozo kama zote,ufisadi,wizi,rushwa,ujambazi vimetamalaki! Na bado hapo... Kazi inaendelea! Mpaka mtubu na kuomba msamaha! SHAABASH!
Balaa sn
 
Magufuli hayupo kwa miezi mitano tu hayo madudu yote yametokea kwa miezi mitano tu? Hebu acha KUKURUPUKA!!!!
Watu mnashindwa ku kubali mlikuwa wrong dhidi ya Magufuli, sasa Magufuli hayupo na mlichotarajia hakiji ili kuendeleza u mbuni bado mna ji mbuni tu kichwa mchangani.
 
Wafanye nini sasa?
Ni kutafuta jinsi ya kutatua matatizo yaliyopo , tunaishi sasa , jana imepita iwe kwamtazamo wa ubaya au uzuri , imeshapita hiyo , tuangalie sasa kinafanyika nini ,mifumo isukwe kiutaalam ili kukidhi matakwa na mahitaji ya nchi na wananchi kwa ujumla .
 
Fursa hiyo tunayo? je wako tayari kujirekebisha?
 
JPM hayupo tena! Vipi amekwambia ulipe tozo? Lawama za BWM alizibeba Kikwete?.... Mlizoea kumtupia lawama JPM sasa hakuna wa kumtupia lawama sio!? Kazi inaendelea! Hakuna miradi mipya,tozo kama zote,ufisadi,wizi,rushwa,ujambazi vimetamalaki! Na bado hapo... Kazi inaendelea! Mpaka mtubu na kuomba msamaha! SHAABASH!
Ndio mana ukaambiwa shida zote hizi sababu ya utawala wake Magufuli. Mama anajitahidi tu kurekebisha hali. Hebu we fikiri no ajira mpya for 6yrs. mshahara alokuwa akilipa JK ndo huo huo mpk anakufa, hakuna kupanda madaraja, nk. Mamiradi makubwa kuliko uwezo wa bajeti, sasa Mama afanyeje!!!
 
Wenye fikra njema kama nyie watawaita Magaidi. Haya maccm bwana
 
Magufuli hayupo kwa miezi mitano tu hayo madudu yote yametokea kwa miezi mitano tu? Hebu acha KUKURUPUKA!!!!
Jipe mda tu baada ya miaka 10, 20 mtakuwa mnasema Magufuli. Hayo madudu yote in first place yametokea toka kitambo ndiyo maana kabla ya Magufuli 2015 tulizungusha mikono mabadiliko.

Nakumbuka watu kupigwa mabomu arusha, morogoro na Kikwete kurushiwa mawe mbeya na Mwinyi kuchapwa kibao kwa kadamnasi.
 
Hebu tuondolee upumbavu wako. Dhalimu magufuli alikuwa ni janga kubwa la Taifa na Mwenyezi Mungu ni mkubwa na hivyo akaamua kumnyakua baada ya sala na maombi mengi ya Watanzania waliofanyiwa maovu mbali mbali na yule dhalimu.

Extent and level of extremism haijawahi kufikia ile ye Magufuli. Jamaa aliwafanya nchi nzima kama misukule. Alitumia utisho ambao kila mwanadamu anauongopa- Execution.
 
Hebu tuondolee upumbavu wako. Dhalimu magufuli alikuwa ni janga kubwa la Taifa na Mwenyezi Mungu ni mkubwa na hivyo akaamua kumnyakua baada ya sala na maombi mengi ya Watanzania waliofanyiwa maovu mbali mbali na yule dhalimu.
Alikuwa janga ktk historia ya tanzania
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Back
Top Bottom