Ule mpango uliokuwa umemnasa Mbowe, na kwa pamoja CHADEMA ulipo vurugika kwa mteja kupoteza raslimali muhimu iliyokuwa imapangwa aiwasilishe na kujisalimisha kwa Samia na Genge lake; ilibidi haraka haraka mafundi watengeneze mitego ya kuikwamisha CHADEMA Mpya, chini ya uongozi mpya haraka iwezekanavyo ili mipango ya Genge kuendelea kuishikilia serikali isivurugike.
Kwanza waliwategemea wapinzani wa ndani ya chama (wa upande wa Mbowe) kwamba watakivuruga chama na kukisambaratisha. Ilipoonekana hili haliwezekani wakawatumia hao hao kwa mbinu ya kujiondoa ndani ya chama, ikitegemewa kuwa CHADEMA itatikisika kwa wingi wa wanachama watakaoondoka ndani ya chama. Hili nalo liliposhindikana kuitikisa CHADEMA wakaona wawawezeshe waliojiondoa kwa kuwapeleka CHAUMMA kwa kelele nyingi za kuwatishia waliobaki ndani ya CHADEMA kukosa kushiriki kwenye uchaguzi. Kizingiti hiki pia kimeshindwa kuizuia CHADEMA kuendelea kuwa chama chenye matumaini kwa wananchi.
Wengi wa watu walio tkwa, kupotezwa na kuuawa ni watu waliojitambulisha kuwa karibu na CHADEMA. Kwa hiyo hii nayo ilikuwa ni mbinu ya kuwatisha watu wasijihusishe na chama hicho.
Kwa upande wa serikali, kupitia kwa Msajiri wa Vyama vya siasa, naye hakubaki nyuma kutekeleza mipango ya kuidhoofisha CHADEMA; kwa mfano, kwa kutowatambua viongozi wa chama walioteuliwa katika nafasi mbalimbali za uongozi; na kama hili halitoshi CHADEMA wakaambiwa hawatashiriki katika chaguzi mbalimbali tokea sasa hadi 2030; kwa sabau tu ya kukataa kusaini kikaratasi cha yanayoitwa maadili ya uchaguzi
Yoote haya yameonekana kushindwa kukidhibiti CHADEMA, ambacho sifa zake zinazidi kuenea miongoni mwa wananchi
Lakini, kilicho watisha zaidi Genge na Samia mwenyewe, ni hii Kampeni ya "NO REFORM, NO ELECTION". Wamejaribu kila mbinu kuwahadaa wananchi kwamba marekebisho yaliyofanywa kwa kupitisha sheria "Feki" ya kuunda "Tume Huru "FEKI"" yanatosha kuufanya uchaguzi kuwa wa HAKI. Kinacho washinda kujieleza kwa wananchi ni swali rahisi: Kuna ugumu gani wa kutengeneza Kanuni mpya zitakazo hakikisha uchaguzi utakuwa HURU na wa HAKI? Hawana jibu la swali hili rahisi kabisa!
Badala ya kujibu hilo swali na kufanya maandalizi ya kutengeneza kanuni za uchaguzi, wameona kitu rahisi kwao ni kuendelea kuivuruga CHADEMA ili isiweze kuendelea na mipango yake ya kuwaongoza wananchi kukataa uchaguzi usiokuwa HURU na HAKI.
Kwa hiyo wakageuzia mbinu zao kuwazushia kesi za uongo viongozi na kuwaweka ndani; wakitegemea kuwa ile Kampeni ya "NO REFORM, NO ELECTION" itakufa. Badala ya kufa, Kameni ndonkwanza inapamba moto, kwa viongozi walio baki kufanya kazi nzuri sana ya kuelezea uchafu wa chaguzi zote zifanywazo na CCM.
Sasa wameamua CHADEMA isimamishwe kufanya shughuli za chama, kwa kuibua kesi ya waZanzibari.
Na huko mahakamani, wanahakikisha kwamba kesi zinapigwa danadana na wala haionyeshi zitapita haraka kuiachia muda CHADEMA iendelee na shughuli zake za kisiasa
Hizi zote ni mbinu tu, zinazotengenezwa, ili kuiachia njia wazi CCM
Sasa katika hali ya namna hii waTanzania wafanye kitu gani kuhakikisha kwamba HAKI yao ya kuwachagua viongozi wanaowataka wao inlindwa?
"NO REFORM, NO ELECTION" ni lazima iendelee kwa nguvu zaidi.
Mwl
Kalamu, well said...
Hata hivyo, kumbuka kuwa, katika mipango ya Mungu aliye juu mbinguni, kwake huwa hakuna kuwahi wala kuchelewa....
Kwake kila kitu huenda kwa mipangilio iliyopangwa na kupangika huko juu japo kwa binadamu sisi huona kama ni majanga, bahati mbaya, haiwezekani, laana nk
Kila kitu kinachotokea sasa kina maana na kusudi lake....
KUSUDI #1: Kwa wenye HAKI, nyakati za giza, mateso, dhuluma kuzidi na kukosa matumaini, huwa ni ishara ya wokovu na ukombozi. Hapo ndipo Mungu hutokea na kuonesha uwezo na nguvu zake kuwa na watu wake....
KUSUDI #2: Kwa hayawani hawa, waabudu miungu, walozi na wachawi wanaongoza dola sasa - CCM...
Mungu amewaruhusu kwa muda wafanye uovu na dhuluma zao huku wakijidanganya nafsi zao kuwa wako salama. The FACT is that, they are not safe, rather they are killing themselves with their bare hands through their actions...
Pamoja na uovu wao, Mungu hawachukii bali anawapenda sana ndiyo maana ujumbe wa kuwaasa kurudi ktk mstari na kutenda haki na kuacha dhuluma, unasikika masikioni mwao kama ngurumo ya radi, Lakini wamefanya mioyo yao migumu....
Na kwa sababu hawataki kutii, basi wamechagua mauti yao wenyewe kwa hiari zao. Hivyo kufumba na kufumbua na ktk mazingira wasiyoyatarajia kabisa watapoteza kila mamlaka waliyonayo inawapa jeuri ya kutenda watendayo na watapewa watu wengine....
Hapo ndipo kitakapokuwa kilio na kusaga meno, kwa sababu:
For every action there is an equal and opposite reaction...
Kaka tulieni. Kila mtu afanye kile anachoweza kufanya kwa sasa. Tundu Lissu yuko salama, in no time from now, atakuwa huru nje na lazima taifa lote litakaa mezani kusikilizana. Hii haitawezekana bila Mwenyekiti wa CHADEMA kuwepo kwenye mazungumzo hayo...
Na niwatie moyo kuwa, CHADEMA iko salama na imara more than before..
Lakini kubwa kabisa na la muhimu kuliko yote ni hili: Kwa miezi mitatu iliyobaki kabla ya tarehe ya uchaguzi mkuu, na kwa kuwa tunaanza mchakato wa kufanya ELECTORAL REFORMS, uchaguzi mwaka huu haiwezekani ukafanyika. Uchaguzi mkuu utafanyika aidha mwaka kesho 2026 au 2027...
Vipi wanaochukua form za kugombea ubunge, udiwani nk? Vipi CCM walishateua mgombea u - Rais?
JIBU: Don't mind them. They are playing a mind game. Their action & process has no effect at all and it doesn't justify anything. Wanaweza kukaa nazo hizo fomu mpaka wakati uliokubalika na Bwana utakapofika, au kama pesa zao zitawauma, warudishe makaratasi hayo. Bwana asema...
Everything is written on the board. Heri yule mwenye akili za kusoma na kuelewa...
Asante