Ule mpango uliokuwa umemnasa Mbowe, na kwa pamoja CHADEMA ulipo vurugika kwa mteja kupoteza raslimali muhimu iliyokuwa imapangwa aiwasilishe na kujisalimisha kwa Samia na Genge lake; ilibidi haraka haraka mafundi watengeneze mitego ya kuikwamisha CHADEMA Mpya, chini ya uongozi mpya haraka iwezekanavyo ili mipango ya Genge kuendelea kuishikilia serikali isivurugike.
Kwanza waliwategemea wapinzani wa ndani ya chama (wa upande wa Mbowe) kwamba watakivuruga chama na kukisambaratisha. Ilipoonekana hili haliwezekani wakawatumia hao hao kwa mbinu ya kujiondoa ndani ya chama, ikitegemewa kuwa CHADEMA itatikisika kwa wingi wa wanachama watakaoondoka ndani ya chama. Hili nalo liliposhindikana kuitikisa CHADEMA wakaona wawawezeshe waliojiondoa kwa kuwapeleka CHAUMMA kwa kelele nyingi za kuwatishia waliobaki ndani ya CHADEMA kukosa kushiriki kwenye uchaguzi. Kizingiti hiki pia kimeshindwa kuizuia CHADEMA kuendelea kuwa chama chenye matumaini kwa wananchi.
Wengi wa watu walio tkwa, kupotezwa na kuuawa ni watu waliojitambulisha kuwa karibu na CHADEMA. Kwa hiyo hii nayo ilikuwa ni mbinu ya kuwatisha watu wasijihusishe na chama hicho.
Kwa upande wa serikali, kupitia kwa Msajiri wa Vyama vya siasa, naye hakubaki nyuma kutekeleza mipango ya kuidhoofisha CHADEMA; kwa mfano, kwa kutowatambua viongozi wa chama walioteuliwa katika nafasi mbalimbali za uongozi; na kama hili halitoshi CHADEMA wakaambiwa hawatashiriki katika chaguzi mbalimbali tokea sasa hadi 2030; kwa sabau tu ya kukataa kusaini kikaratasi cha yanayoitwa maadili ya uchaguzi
Yoote haya yameonekana kushindwa kukidhibiti CHADEMA, ambacho sifa zake zinazidi kuenea miongoni mwa wananchi
Lakini, kilicho watisha zaidi Genge na Samia mwenyewe, ni hii Kampeni ya "NO REFORM, NO ELECTION". Wamejaribu kila mbinu kuwahadaa wananchi kwamba marekebisho yaliyofanywa kwa kupitisha sheria "Feki" ya kuunda "Tume Huru "FEKI"" yanatosha kuufanya uchaguzi kuwa wa HAKI. Kinacho washinda kujieleza kwa wananchi ni swali rahisi: Kuna ugumu gani wa kutengeneza Kanuni mpya zitakazo hakikisha uchaguzi utakuwa HURU na wa HAKI? Hawana jibu la swali hili rahisi kabisa!
Badala ya kujibu hilo swali na kufanya maandalizi ya kutengeneza kanuni za uchaguzi, wameona kitu rahisi kwao ni kuendelea kuivuruga CHADEMA ili isiweze kuendelea na mipango yake ya kuwaongoza wananchi kukataa uchaguzi usiokuwa HURU na HAKI.
Kwa hiyo wakageuzia mbinu zao kuwazushia kesi za uongo viongozi na kuwaweka ndani; wakitegemea kuwa ile Kampeni ya "NO REFORM, NO ELECTION" itakufa. Badala ya kufa, Kameni ndonkwanza inapamba moto, kwa viongozi walio baki kufanya kazi nzuri sana ya kuelezea uchafu wa chaguzi zote zifanywazo na CCM.
Sasa wameamua CHADEMA isimamishwe kufanya shughuli za chama, kwa kuibua kesi ya waZanzibari.
Na huko mahakamani, wanahakikisha kwamba kesi zinapigwa danadana na wala haionyeshi zitapita haraka kuiachia muda CHADEMA iendelee na shughuli zake za kisiasa
Hizi zote ni mbinu tu, zinazotengenezwa, ili kuiachia njia wazi CCM
Sasa katika hali ya namna hii waTanzania wafanye kitu gani kuhakikisha kwamba HAKI yao ya kuwachagua viongozi wanaowataka wao inlindwa?
"NO REFORM, NO ELECTION" ni lazima iendelee kwa nguvu zaidi.