Watz kwa uongo mmezidi sasa. Kwanza Californium does not occur naturally. Maana yake ni man made. Californium inapatikana kwa process inaitwa paricle bombardement of Plutonium ambayo ni very expensive na inahitaji utaalam wa juu sn kwa sababu kwanza hayo madini yana mionzi ( radioactive) na inaweza kusababisha madhara makubwa kwa binaadam kiafya.
So far ni sehemu mbili tu duniani zinazalisha Californium ambazo ni Oak Ridge National Laboratory Marekani na Research Institute of Atomic Reactors, Dimitrovgrad huko Urusi. Kwa mwaka ni nusu gram tu ya Californium huzalishwa dunia nzima hivyo kufanya kuwa na scramble ya kuyapata kutokana na kuwa adimu kupita kiasi.
Hivyo basi huu upotoshaji wako wa kusema yanapatikana Nigeria ni uzushi na uzandiki wenye mlengo wa ukurupukaji na upotoshaji.