Madini aliyotema Rais Magufuli kwa waathirika wa mafuriko huko Lindi

Madini aliyotema Rais Magufuli kwa waathirika wa mafuriko huko Lindi

Nategemea Rais wa wanyonge atasema Mwanza hakuahidi moto uliosababishwa na umeme kuunga vibanda vya machinga hivyo wapambane na hali zao!Au kwasababu Mwanza ni nyumbani hivyo atawapa maneno ya faraja kama tulivyoshuhudia kwenye bomoa bomoa?
 
Nasoma historia ya dikteta Franscisco Franco wa Uhispania, baba yake alikuwa mlevi aliyewatesa sana watoto wake.

Historia ya Stalin nayo ni hivyo hivyo.

Hitler na Idi Amin, Stalin wote walikataliwa na jamii kwa namna moja ama nyingine.
Hawakuwa na kisomo cha kupanda ngazi.Hitler hakuweza kuingia art school, Idi Amin hakuweza kuwa officer mwenye elimu, Stalin hakuweza kumaliza seminary.

Ukisoma maisha ya Franco katika kitabu "Franco" cha Professor Paul Preston utaona baba yake alivyokuwa mlevi na anawapigapiga watoto, mpaka akaikimbia familia.

Ukisoma maisha ya Stalin katika kitabu cha Professor Stephen Kotkin "Stalin, Paradoxes of Power 1878- 1928" utaona yaleyale yamejirudia.

Madikteta wengi wanakuwa kama wanalipiza visasi hivi kwa mambo ambayo hayakwenda vizuri maishani mwao.
 
Haya ndiyo madini ya ukweli aliyotema Rais Magufuli kwa waathirika wa mafuriko huko Lindi kama alivyonukuliwa

View attachment 1355631

-----
Watanzania tumejenga kwenye mikondo ya maji haizibi, mvua ikija kuwachukua mnapiga kelele ni mafuriko, mnajifurika wenyewe, mlima upo hutaki kujenga unakwenda kujenga kwenye mabonde

Nilimtuma Waziri Mkuu na ametoa maelekezo waliojenga mabondeni wahame Serikali haitohangaika na aliyejipeleka kwenye bonde mwenyewe eti ishughulikie kumlisha, uwe wa Chato uwe wa wapi, huo ndio msimamo, acheni kujenga kwenye mabonde

Tuzitumie hizi mvua kama fursa, badala ya kulalamika, tuyatumie maji yaliyoletwa na Mungu kulima, tumekalia kulalamika mafuriko mafuriko na hatulimi, maji yakipotea tuanze kulalamika njaa, Mungu atashangaa alituletea maji hatukuyatumia, kila Mtanzania pale alipo afanye kazi

Wakiwa wanafurikwa uko wewe lima kunde,viazi, wakitoka kwenye mafuriko waje wale chakula chako kwa kuwatwanga fedha, kuna Wasukuma wameenda Lindi na Ng'ombe maji yamewachukua mabondeni, hakuna cha kusaidiwa uliyafuata mwenyewe mabonde ngoja yakubondoe ili ujifunze vizuri
Yy ameshiba hawez wakumbuka wenye njaa na matatizo yao
 
February 16, 2020
Nyasa, Ruvuma
Tanzania

Kata ya Linga, Nyasa wakumbwa na mafuriko

Wananchi wa kata ya Linga wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma waomba msaada wa serikali kufuatia mazao yao kuharibiwa na mafuriko



Source: RUVUMA TV
 
Mbona alitoa mabilion ya msaada kwenye maafa ya kivuko Mwanza?
Kwani ni yy Rais 'aliye tuma" kivuko kile kiue watu?
Rais wa nchi anapotoa misaada ya maafa kutokana na eneo analo toka anapoteza uhalali wa kuchaguliwa tena
Amekuwa akikejeli watz wanapo pata matatizo ISIPOKUWA tu kama hayo matatizo yametokea kanda anayo toka
Anyimwe kura Oktoba 2020
 
February 16, 2020
Muhoro, Rufiji
Tanzania

Mafuriko Rufiji Pwani

Wananchi wa Muhoro Rufiji mkoa wa Pwani waiomba serikali msaada wa kibinadamu na pia kuwajengea daraja kufuatia mafuriko makubwa ya maji. Hayo walimueleza Naibu Waziri wa Nishati Mh. Subira Mgalu alipopita eneo hilo kuangalia mradi wa umeme vijijini REA na ndipo alipolazimika pia kusikiliza kilio chao cha mafuriko .



Source: ITV Tanzania
 
Sikio la kufa halisikii dawa ,mi sioni kama kakosea kuongea ukweli huo ,Sisi watanzania ni wagumu sana kufata maelekezo hata kama yana malengo mema kwetu suala la kutojenga kwny mikondo ya maji kila mwaka linaongelewa lakini wananchi wanapuuzia tuu,ebu ona hata hapa Dar watu wanaambiwa wahame kwenye mabonde wanahama kwa muda baadae wanarudi tena ,sasa Tunataka serikali ifanyaje ,au viongozi waanze kutumia maneno gani zaidi ili tuelewe,Maana kuambiwa ukweli watz wanakasirika,Hapo hamna kosa kauli ngumu hutolewa kwa watu wagumu kuelewa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu Rais wetu kama anasoma jamii forum atajifunza mavitu. Humu anafundishwa bure kwa bundle kiduchu.

Kama ningekuwa na uwezo ningemuacha Rais aendelee kujiharibia ukubaliwaji wake kwa jamii.

Ili nishinde uchaguzi mkuu kiu laini, hapa ni sawa na kujipaka mavi!

Mpeni heko aseme zaidi.wapiga kura wanaona . hawatafurahia Rais kushangilia vifo bin majanga ya wenzi wao!

Siyo civilian wote wanajua jografia ya Lindi.

Mgonjwa wa malaria unamuacha afe eti "uliwafata mbu mwenyewe" seriously?
Km ni kweli Siyo akili hii, Nadhani mabeberu wameharibu akili yake, ili akose umaarufu.
 
Back
Top Bottom