Kiukweli kufuatia kauli za kishujaa anazotoa Rais Magufuli kwa wahanga mbali mbali wa majanga ya asili basi itoshe kusema tu kuwa Rais Magufuli hana utu kabisa!
Hivi Rais Magufuli amewahi kuona huko duniani jinsi watu wanavyoshikamana kwenye majanga? Amewahi kuona majanga kama yale ya nchi ya Haiti au majanga ya moto kule Australia? Yani kwa jinsi anavyoongea kwa watu mbalimbali wanaokumbwa na majanga ni tuna Rais wa ajabu kweli kweli asiye na utu.
Watu 21 wamekufa huko Lindi kwa kusombwa na mafuriko halafu yeye anatoka na kusema acha "wafurikwe sawasawa" Ni kuwakejeli au? Kwa hili kweli hapana. Tutampinga wazi wazi kingozi wa aina hii ambaye anaonyesha ukatili wa wazi wazi dhidi ya watu wake wanaokumbwa na majanga!
Watu walikufa Kagera kutokana na majanga serikali ikachangisha fedha kupeleka kwenye miradi na kuwaacha watu wakiwa "wakiwa" huku ikiwaambia eti serikali haikuleta tetemeko!
Mimi niulize wale wataalam wa sayansi ya binadamu, ki biologia hii imekaaje?
Mwisho ninawashangaa sana wale wote wanaounga mkono ukosefu huu wa ubinadamu uliokithiri!
Haya ni matokeo ya kutesa na kupiga watoto.
Mtoto ukimlea kwa kumtesa na kumpiga, hilo linamkaa kichwani hata kwenye subconscious, anakuwa mnyonge, lakini na yeye siku akipata kuwa mkubwa/nafasi/cheo, anaona ni zamu yake kulipiza.
Kuna wachache wanaweza kuona historia yao ya kupigwa inawafanya wawe na huruma zaidi kwa wenzao, wengi wanakuwa wanaona kupigana na kunyanyasana ni sawa tu.
Ni haki ya mwenye nguvu kumsimanga na kumpiga mnyonge.
Ndiyo maana utasikia kauli hizi si mara moja tu kwa Magufuli, ni pattern.
Aliwasengenya waliopata tetemeko Kagera, alisema atawapiga mpaka shangazi za wapinzani wake, aliwasema watu wanaofeli katika nchi isiyo na mifumo kuwa ni vilaza, sasa anawasengenya watu waliopatwa na maafa.
Hii kitu Wajerumani wanaita schadenfreude. Ni mtu kufurahia maafa ya mwenzako, mara nyingi kwa wewe kujiona bora zaidi.
Kisaikolojia kwa undani kabisa inaonesha mtu hajipendi mwenyewe, ana machungu fulani na maisha, na hivyo, hawezi kupenda wengine.
Atawazodoa, atawasimanga, atawanyanyasa.
Matatizo haya si ya Magufuli pekee. Watanzania wengi wana matatizo haya.
Na ndiyo maana wengi wanamuelewa na kumshabikia sana Magufuli.
Maisha ya mtu hayana thamani sana katika jamii ya watu masikini.
Ukiyapa thamani sana, watu wanakushangaa wewe unayetaka kuyapa maisha ya mtu thamani.
Hawamshangai huyu anayeshusha thamani ya maisha ya mtu.
After all, kufa ni jambo rahisi sana katika jamii ya watu masikini, sasa ukishangaa rais anasheherekea watu kufa, watu masikini wengine watakushangaa wewe, unashangaa nini wakati hilo ni jambo la kawaida sana kwao?