Madini aliyotema Rais Magufuli kwa waathirika wa mafuriko huko Lindi

Madini aliyotema Rais Magufuli kwa waathirika wa mafuriko huko Lindi

Mkuu muwe mnatumia akili . hivi inaingia skilini unawanyima misada wananchi wako wakati wa maafa afu siku nyingine unasaidia Msumbiji, Zimbabwe kwenye maafa mengine ?
Magufuli ni mtu mmoja ambaye katika saikolojia yake inawezekana kavurugwa huko nyuma.

Inakuwa kama kapigwapigwa alivyokuwa mdogo, hakupata mapenzi ya familia, sasa anaona kakimua kapata cheo, na yeye zamu yake kupiga watu.

Ndiyo maana kauli zake ni za kupigapiga, kusengenyasengenya, za ujingaujinga tu.

Mara atapiga wapinzani mpaka shangazi, mara anaita watu walioshindwa kufauku katuka nchi ambayo haina mifumo vilaza, mara anakaripia watendaji kuhusu lift kinyume na sera za serikali yake mwenyewe.

Ni mtu wa ovyo sana. Kapewa urais!

Hizi si za staha za kirais.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huo ndio ukweli, nani alikutuma ujenge mabondeni? Unaenda bonds la mto msimbazi mtu kajenga ukingoni kabisa mwa mto, anatumia milioni kadhaa huku akiona kabisa hapafai kukaa nyumba pale.

Haya maisha ukibembelezwa sana unakuwa mjinga.
 
Kuna vitu vinachekesha sana nimejaribu kufikiria hadi enzi za historia yetu kama nchi
 
Huo ndio ukweli, nani alikutuma ujenge mabondeni? Unaenda bonds la mto msimbazi mtu kajenga ukingoni kabisa mwa mto, anatumia milioni kadhaa huku akiona kabisa hapafai kukaa nyumba pale.

Haya maisha ukibembelezwa sana unakuwa mjinga.

..hata milimani kunaweza kutokea MUDSLIDE / MAPOROMOKO YA UDONGO.

..ukweli ni kwamba Jpm ana roho ya KIKATILI. hata walioathirika na tetemeko la ardhi badala ya kuwafariji aliwatolea lugha za MATUSI.

..suala la mafuriko lina sehemu mbili. Sehemu ya kwanza ni serikali kutokuweka MIUNDOMBINU ya kupitisha maji [ ya mvua na maji machafu ]. Sehemu ya pili ni wananchi waliojenga kimakosa mabondeni.

..
 
Hakuna ukweli wowote wa alichosema. Tuko mamilioni ya watu, tunawezaje wote tukaishi milimani!!? Hiyo milima ni mingapi hadi nchi nzima tuishi huko.
Kuna tatizo kichwani kwa mkuu, nami nawahimiza Watanzania wenzangu Oktoba tokeni kwa wingi mmwadhibu mtu huyu asiyetumia kinywa chake kwa staha anapozungumzia maswahibu ya Wananchi.
When it comes to people's life the stakes are too high to make it a political agenda.
There are hundred safe ways to prevent any political leader from being re-elected for a second term.

If you live in dangerous areas that are prone to floods, it is you who is going to lose big, you either lose your beloved ones or you lose your life. And there is no 100% guarantee the politician you hate the most won't be re-elected after your loss.

Ukikaa mabondeni anaekufa sio Mugufuli bali wewe na ndugu zako, maeneo yaliyo juu ni mengi sana kuliko mabondeni.
Kwani umefungwa na nati au umechomelewa na umeme hapo mabondeni kiasi cha kushindwa kwenda kuanzisha makazi maeneo mengine?
 
Unaniuliza mimi kwani mimi ndiye nimeleta habari za "kufunzwa na dunia" hapa?

Serikali ziache watu wafe kwa sababu wanafunzwa na dunia?

Kama hivyo kwa nini zinajenga hospitali?

Kwa nini zisiwaache watu wafe kwa magonjwa wafunzwe na duni?

Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa nimekuelewa,we are on two different pages though we are reading same book
 
Naomba akumbushwe yeye kama rais ni mfariji mkuu.
Hilo la muhimu sana, achague na achambue ya kuyatoa kinywani ni vile wananchi most of them hawana utambuzi(ashakum si matusi)(layman) "mostly" ndio maana kauli kama hizi zinapita softly.

Kwa jamii na mahala ambapo jamii(wananchi) wanauelewa wa upembuzi, hizo kauli zina'impact kubwa na mbaya sana.
Mungu mbariki rais wetu


Sio tu kufariji, ila hata kusema ukweli. Anachosema Rais ni kwamba hata iweje, mtu kwanza kupata hasara ya mafuriko ni yule atakuwa amejenga kwenye mkondo wa maji.
 
Haya ndiyo madini ya ukweli aliyotema Rais Magufuli kwa waathirika wa mafuriko huko Lindi kama alivyonukuliwa

-----
Watanzania tumejenga kwenye mikondo ya maji haizibi, mvua ikija kuwachukua mnapiga kelele ni mafuriko, mnajifurika wenyewe, mlima upo hutaki kujenga unakwenda kujenga kwenye mabonde

Nilimtuma Waziri Mkuu na ametoa maelekezo waliojenga mabondeni wahame Serikali haitohangaika na aliyejipeleka kwenye bonde mwenyewe eti ishughulikie kumlisha, uwe wa Chato uwe wa wapi, huo ndio msimamo, acheni kujenga kwenye mabonde

Tuzitumie hizi mvua kama fursa, badala ya kulalamika, tuyatumie maji yaliyoletwa na Mungu kulima, tumekalia kulalamika mafuriko mafuriko na hatulimi, maji yakipotea tuanze kulalamika njaa, Mungu atashangaa alituletea maji hatukuyatumia, kila Mtanzania pale alipo afanye kazi

Wakiwa wanafurikwa uko wewe lima kunde,viazi, wakitoka kwenye mafuriko waje wale chakula chako kwa kuwatwanga fedha, kuna Wasukuma wameenda Lindi na Ng'ombe maji yamewachukua mabondeni, hakuna cha kusaidiwa uliyafuata mwenyewe mabonde ngoja yakubondoe ili ujifunze vizuri

Ni kweli kabisa, maana hata Madaraja yaliyotengenezwa na serikali kwa fedha za walipa kodi, yalipobomolewa na mafuriko, serikali haikuchukua hatua maana hayo madaraja yalifuata maporomoko.
Pia kingo za mito zilipobomolewa na maji, na yale maji yakaelekea kwenye makazi ya watu, hizo kingo ndo zilifuata hayo maji.

NB:
Kauli kama hizi ndizo wanaccm wanazipenda na kuzipigia makofi bila kujua aliyezitoa hana muda nao na anawaona kama mizigo kwa serikali. Tujifunze na tuchukue hatua.
 
Naona udikteta wake unagain momentum ngoja avuke 2020 mtamjua vizuri.
NASIKIA YALE MAFURIKO LINDI YANA CONNECTION NA UKATAJI MITI ILI KUPISHA UJENZI WA BWAWA LA UMEME(Mwalimu NYERERE H.E.P) NA MBAYA ZAIDI ILIKAKATAZWA KUONESHWA HILI TUKIO LIVE NASIKIA NI BALAA KUBWA MNO ILA KUREPORT MWIKO.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwanini hayajatokea dodoma ambako hakuna misitu kabisa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ushahidi unao, wa watu kutokuwa na mawasiliano, kunyimwa yote hayo uliyoorodhesha?
Ushahidi gani unataka, unajua kipato cha wastani tu cha Mtanzania, GDP per capita, ni ushahidi tosha?

Hakiwezi kupanga bajeti ya mtu anayetakiwa kuishi kwa viwango vya utu wa dunia ya leo.

Yani GDP per capita ya Mtanzania haitoshi hata kununua bando ya internet kwa mwaka.

That is if huko mabondeni kuna mawasiliano ya kumuasa kuwa mvua zinakuja ondokeni mabondeni.

Sasa hapo mtu atafanyaje mawasiliano kiasi cha wewe umlaumu kwamba hajafanya mawasiliano?
 
Back
Top Bottom