Madini aliyotema Rais Magufuli kwa waathirika wa mafuriko huko Lindi

Kwanza kabisa nikupongeze Rais wangu kwa majukumu mazito maana kuongoza nchi sio lelema, inahitaji afya ya akili, afya ya mwili na afya zote.

Lakini pia nafurahishwa sana pale unapoamsha akili za watanzania kwa kusema maneno mazima mazima bila kumung'unya. Ijapokuwa inauma lakini "msema kweli mpenzi wa mungu"

Ulipotoa kauli kuhusiana na mafuriko kama kawaida yako bila kumung'unya maneno baadhi ya watu walikuwa na muitikio hasi, lakini kwangu mimi naona unawaambia mambo mawili

1. Wajifunze kufikiri kabla ya kutenda, waangalie faida na hasara kwa muda mrefu na muda mfupi wanapotaka kufanya maamuzi.

2. Wajifunze kuweka akiba ya dharura.

Sisi tuta-ukumbuka Daima uongozi uliotukuka chini ya Dkt: John Pombe Joseph Magufuli

Zingatia: Wakati unataka kutoka usisahau kutuachia katiba imara kabisa maana hatujui ajaye kama atakuwa mzalendo kama wewe.

Nawasilisha
 
1581504017682.png
1581504035051.png
We FaizaFoxy umejificha wapi? ....... wenzio tuna'furikwa' hukuuu!
 
Nnacho mpendea Mr pezidaa ni mkweli muda wote, hajui kumung'unya maneno. Wa Tz wanapenda kudanganywa ili mradi kuifurahisha nafsi. Btw anko ashawaambia kuwa yeye si mwanasiasa kitambo Sana. Km unabisha kajenge bondeni!
 
Haya ndiyo madini ya ukweli aliyotema Rais Magufuli kwa waathirika wa mafuriko huko Lindi kama alivyonukuliwa

-----
Watanzania tumejenga kwenye mikondo ya maji haizibi, mvua ikija kuwachukua mnapiga kelele ni mafuriko, mnajifurika wenyewe, mlima upo hutaki kujenga unakwenda kujenga kwenye mabonde

Nilimtuma Waziri Mkuu na ametoa maelekezo waliojenga mabondeni wahame Serikali haitohangaika na aliyejipeleka kwenye bonde mwenyewe eti ishughulikie kumlisha, uwe wa Chato uwe wa wapi, huo ndio msimamo, acheni kujenga kwenye mabonde

Tuzitumie hizi mvua kama fursa, badala ya kulalamika, tuyatumie maji yaliyoletwa na Mungu kulima, tumekalia kulalamika mafuriko mafuriko na hatulimi, maji yakipotea tuanze kulalamika njaa, Mungu atashangaa alituletea maji hatukuyatumia, kila Mtanzania pale alipo afanye kazi

Wakiwa wanafurikwa uko wewe lima kunde,viazi, wakitoka kwenye mafuriko waje wale chakula chako kwa kuwatwanga fedha, kuna Wasukuma wameenda Lindi na Ng'ombe maji yamewachukua mabondeni, hakuna cha kusaidiwa uliyafuata mwenyewe mabonde ngoja yakubondoe ili ujifunze vizuri
Tafadhali rejea hiyo hotuba na rekebisha kilichosemwa, hususan hapo nilipokuwekea nyekundu. Rais kasema. ..

" Kuna baadhi ya Watanzania wamejenga kwenye mikondo ya maji na mikondo ya maji haizibwi..."

Sasa wewe kwanini maneno mengine hukuyaweka? Huo ni ushenzi.

Nimemsikikiza Rais na Rais ameonhea vizuri na iutoa into la mvuankubwa zinazotarajiwa. Landa hutazami haki ya hewa wewe.

Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.

Rais yupo sahihi Kwa hili. Naunga mkono Kwa kuwa mikali maana watani zangu wa Rufiji wanangoja "hedikopta" zikawaokoe.

Wewe huwajui Warufiji, tuulize sisi jirani zetu hao. Hao toka wazee wao wawahadithie kuwa wakati wa mafuriko enzi za Nyerere zilienda helicopter kuwaokoa watu, basi kila mmoja na yeye ikitokea mafuriko anangoja helicopter iksmuokoe ili baadae akawakoge wenzake kuwa kapanda "hedikopta" kama babu yake!

Cheza na Warufiji wewe.
 
Haya ndiyo madini ya ukweli aliyotema Rais Magufuli kwa waathirika wa mafuriko huko Lindi kama alivyonukuliwa

-----
Watanzania tumejenga kwenye mikondo ya maji haizibi, mvua ikija kuwachukua mnapiga kelele ni mafuriko, mnajifurika wenyewe, mlima upo hutaki kujenga unakwenda kujenga kwenye mabonde

Nilimtuma Waziri Mkuu na ametoa maelekezo waliojenga mabondeni wahame Serikali haitohangaika na aliyejipeleka kwenye bonde mwenyewe eti ishughulikie kumlisha, uwe wa Chato uwe wa wapi, huo ndio msimamo, acheni kujenga kwenye mabonde

Tuzitumie hizi mvua kama fursa, badala ya kulalamika, tuyatumie maji yaliyoletwa na Mungu kulima, tumekalia kulalamika mafuriko mafuriko na hatulimi, maji yakipotea tuanze kulalamika njaa, Mungu atashangaa alituletea maji hatukuyatumia, kila Mtanzania pale alipo afanye kazi

Wakiwa wanafurikwa uko wewe lima kunde,viazi, wakitoka kwenye mafuriko waje wale chakula chako kwa kuwatwanga fedha, kuna Wasukuma wameenda Lindi na Ng'ombe maji yamewachukua mabondeni, hakuna cha kusaidiwa uliyafuata mwenyewe mabonde ngoja yakubondoe ili ujifunze vizuri
Hili jitu lipuuzi sana
 
Mimi nimekuelewa, na in fact haya siyo "madini" ama la, kama ni madini, basi ni aidha moramu ama kokoto za kujengea choo. Kamwe hayawezi kuwa almas ama dhahabu ama any other precious metals...

Nadhani, Mr President Pombe, lengo lake ilikuwa ni kutoa ujumbe wa athari za mafuriko na tahadhari za kuchukua kwa pande zote wananchi na serikali ambayo ndiyo yenye jukumu la kupanga na kugawa ardhi kwa matumizi mbalimbali nchini kote. Unfortunately, kama kawaida yake akawa mentally disturbed akiwa kwenye podium na kutapika nyongo hii...

Bahati mbaya ni kuwa, Bwana Magufuli hana maarifa, busara wala ujuzi wa kutumia lugha ktk kuwasilisha ujumbe kwa hadhira ya watu mbalimbali hususani walio ktk nyakati za taabu na shida kama sasa....

Kwa hiyo, kwa kukosa hekima, busara na maarifa = UJUZI ktk kutumia lugha kuwasiliana na watu, ndiyo kajikuta anashikwa na mihemko isiyo na sababu na kujikuta anajiropokea tu huku akitumia lugha ya kuudhi na kukera.....

By the way, hata ktk nchi za wenzetu zilizoendelea, majanga kama haya yanawapata na huwezi kuona viongozi wa serikali zao wanawa kejeli wananchi wao waathirika kama kwa Rais wetu huyu wa ajabu kabisa....

Kuna mji mmoja huko Australia nadhani, mafuriko yameleta athari ya kutisha kiasi kwamba kaya takribani 70,000 ama zaidi nyumba zao zimeingiliwa na maji na huduma kama za umeme, maji nk zimekatika kabisa...

Angekuwa ndiyo Magufuli Rais huko na atoe kauli kama hizi, sina hakika kama angebaki salama mpaka leo!!!

This guy's leadership is a disaster....
 
Alichosema kina ukweli lakini mmmh! nahisi angepunguza ukali wa maneno, angewakumbusha tu wajifunze kuzingatia katazo la kuishi mabondeni.
Hakuna ukweli wowote wa alichosema. Tuko mamilioni ya watu, tunawezaje wote tukaishi milimani!!? Hiyo milima ni mingapi hadi nchi nzima tuishi huko.
Kuna tatizo kichwani kwa mkuu, nami nawahimiza Watanzania wenzangu Oktoba tokeni kwa wingi mmwadhibu mtu huyu asiyetumia kinywa chake kwa staha anapozungumzia maswahibu ya Wananchi.
 
There is such a thing as blaming the victim.

Mtu anyimwe fursa za elimu sawa kwa wote, anyimwe mitaji, haya, anajikakamua afanye ufugaji bila wa kumshika mkono, anakutana na mafuriko huko, kwa sababu nchi haina mifumo, napo rais wake amtukane kwa kukutana na mafuriko.
On the other side of the same coin you get "playing the victim" to get undeserved sympathy.

Sasa sijui kama hao waliopata maafa walinyimwa fursa za kuwafanya wasiishi kwenye ile hali hatarishi, au walionywa na bado wakaendelea kukaidi maonyo waliyopewa hadi maafa yalipotokea!
 
Kwanza kabisa nikupongeze Rais wangu kwa majukumu mazito maana kuongoza nchi sio lelema, inahitaji afya ya akili, afya ya mwili na afya zote.

Lakini pia nafurahishwa sana pale unapoamsha akili za watanzania kwa kusema maneno mazima mazima bila kumung'unya. Ijapokuwa inauma lakini "msema kweli mpenzi wa mungu"

Ulipotoa kauli kuhusiana na mafuriko kama kawaida yako bila kumung'unya maneno baadhi ya watu walikuwa na muitikio hasi, lakini kwangu mimi naona unawaambia mambo mawili

1. Wajifunze kufikiri kabla ya kutenda, waangalie faida na hasara kwa muda mrefu na muda mfupi wanapotaka kufanya maamuzi.

2. Wajifunze kuweka akiba ya dharura.

Sisi tuta-ukumbuka Daima uongozi uliotukuka chini ya Dkt: John Pombe Joseph Magufuli

Zingatia: Wakati unataka kutoka usisahau kutuachia katiba imara kabisa maana hatujui ajaye kama atakuwa mzalendo kama wewe.

Nawasilisha
Mkuu muwe mnatumia akili . hivi inaingia skilini unawanyima misada wananchi wako wakati wa maafa afu siku nyingine unasaidia Msumbiji, Zimbabwe kwenye maafa mengine ?
 
Hakuna ukweli wowote wa alichosema. Tuko mamilioni ya watu, tunawezaje wote tukaishi milimani!!? Hiyo milima ni mingapi hadi nchi nzima tuishi huko.
Kuna tatizo kichwani kwa mkuu, nami nawahimiza Watanzania wenzangu Oktoba tokeni kwa wingi mmwadhibu mtu huyu asiyetumia kinywa chake kwa staha anapozungumzia maswahibu ya Wananchi.
WaTz watamuadhibu kwa tume ipi ?! [emoji87][emoji56]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanza kabisa nikupongeze Rais wangu kwa majukumu mazito maana kuongoza nchi sio lelema, inahitaji afya ya akili, afya ya mwili na afya zote.

Lakini pia nafurahishwa sana pale unapoamsha akili za watanzania kwa kusema maneno mazima mazima bila kumung'unya. Ijapokuwa inauma lakini "msema kweli mpenzi wa mungu"

Ulipotoa kauli kuhusiana na mafuriko kama kawaida yako bila kumung'unya maneno baadhi ya watu walikuwa na muitikio hasi, lakini kwangu mimi naona unawaambia mambo mawili

1. Wajifunze kufikiri kabla ya kutenda, waangalie faida na hasara kwa muda mrefu na muda mfupi wanapotaka kufanya maamuzi.

2. Wajifunze kuweka akiba ya dharura.

Sisi tuta-ukumbuka Daima uongozi uliotukuka chini ya Dkt: John Pombe Joseph Magufuli

Zingatia: Wakati unataka kutoka usisahau kutuachia katiba imara kabisa maana hatujui ajaye kama atakuwa mzalendo kama wewe.

Nawasilisha
Huwa Ni kawaida kwa watu wasiotumia akili kama wewe kuwa na tabia ya kudhani kila anayefikwa na janga basi amejitakia. Hii pia Ni hulka ya watu makatili wasiokuwa na chembe ya huruma moyoni.
Kwao mateso ya watu huwa Ni faraja kwa nafsi zao, hawajuti.
Ukitaka uthibitisho, tazama vifo vya Moshi, na comment ya Rais kuhusu Mchungaji muhusika!!!
 
On the other side of the same coin you get "playing the victim" to get undeserved sympathy.

Sasa sijui kama hao waliopata maafa walinyimwa fursa za kuwafanya wasiishi kwenye ile hali hatarishi, au walionywa na bado wakaendelea kukaidi maonyo waliyopewa hadi maafa yalipotokea!
Kuna watu hawana hata mawasiliano na serikali huko.

Ndiyo maana, nasisitiza mifumo kwanza kabla ya lawama.

Mpe mtu nafasi za ajira, halafu asipotaka kuchukua hizo nafasi za ajira na kwenda mabondeni, hapo unaweza kumlaumu.

Mpe nafasi za elimu, mpe nafasi, muingize kwenye uchumi rasmi, akikataa, unaweza kumlaumu.

Sasa mtu hujampa nafasi ya elimu ya kueleweka, hujampa nafasi ya ajira, mikopo hamna, kika akikutana na ofisa wa serikali anaombwa rushwa, kwa nini asiamue kwenda machakani huko akapambane kivyake bila elimu wala stadi?

Na akipatwa na mafuriko huko kwa sababu hakuna mifumo hata ya kukataza watu wasiende huko, serikali inatakiwa kusema kwa tone ya kuasa, si kusengenya kama muimba taarabu anamchamba mwenzake.

Serikali ina wajibu wa kuwaelimisha wananchi wake, haina wajibu wa kuwasengenya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom