Madini aliyotema Rais Magufuli kwa waathirika wa mafuriko huko Lindi

Madini aliyotema Rais Magufuli kwa waathirika wa mafuriko huko Lindi

G Sam

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2013
Posts
11,795
Reaction score
36,704
Haya ndiyo madini ya ukweli aliyotema Rais Magufuli kwa waathirika wa mafuriko huko Lindi kama alivyonukuliwa

6F787761-81E7-46D5-92B4-A0C9EE3C3BB2.jpeg


-----
Watanzania tumejenga kwenye mikondo ya maji haizibi, mvua ikija kuwachukua mnapiga kelele ni mafuriko, mnajifurika wenyewe, mlima upo hutaki kujenga unakwenda kujenga kwenye mabonde

Nilimtuma Waziri Mkuu na ametoa maelekezo waliojenga mabondeni wahame Serikali haitohangaika na aliyejipeleka kwenye bonde mwenyewe eti ishughulikie kumlisha, uwe wa Chato uwe wa wapi, huo ndio msimamo, acheni kujenga kwenye mabonde

Tuzitumie hizi mvua kama fursa, badala ya kulalamika, tuyatumie maji yaliyoletwa na Mungu kulima, tumekalia kulalamika mafuriko mafuriko na hatulimi, maji yakipotea tuanze kulalamika njaa, Mungu atashangaa alituletea maji hatukuyatumia, kila Mtanzania pale alipo afanye kazi

Wakiwa wanafurikwa uko wewe lima kunde,viazi, wakitoka kwenye mafuriko waje wale chakula chako kwa kuwatwanga fedha, kuna Wasukuma wameenda Lindi na Ng'ombe maji yamewachukua mabondeni, hakuna cha kusaidiwa uliyafuata mwenyewe mabonde ngoja yakubondoe ili ujifunze vizuri
 
Naomba akumbushwe yeye kama rais ni mfariji mkuu.
Hilo la muhimu sana, achague na achambue ya kuyatoa kinywani ni vile wananchi most of them hawana utambuzi(ashakum si matusi)(layman) "mostly" ndio maana kauli kama hizi zinapita softly.

Kwa jamii na mahala ambapo jamii(wananchi) wanauelewa wa upembuzi, hizo kauli zina'impact kubwa na mbaya sana.
Mungu mbariki rais wetu
 
Hivi jiografia ya lindi ina mabonde kweli au? Maana swala la mafuriko mara nyingi huzikumba sehemu za tambarare..

Sent using Jamii Forums mobile app
Niliwahi kusikia mahali kuwa maana ya neno Lindi ni Bonde, sasa sijui ni kweli??

Hata haivyo kama umewahi kusafiri kwenda lindi, ukiwa unaukaribia mji unakuwa kama unashuka bondeni, mjiwenyewe upo bondeni.

Ndio maana makao makuu mapya ya mkoa wamejenga huko juu mlimani kuepuka matukio kama hayo ya mafuriko.
 
Back
Top Bottom