Pre GE2025 Kumekucha: Madiwani Arusha waomba Paul Makonda agombee Ubunge jimbo la Arusha Mjini

Pre GE2025 Kumekucha: Madiwani Arusha waomba Paul Makonda agombee Ubunge jimbo la Arusha Mjini

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Greatest Of All Time

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2017
Posts
23,620
Reaction score
52,790
Baraza la Madiwani mkoani Arusha kwa pamoja limeridhia na kumuomba Mkuu wa Mkoa huo, Paul Makonda kugombea ubunge kwa jimbo la Arusha Mjini.

Je uamuzi huu wa madiwani wa jimbo hilo ni kwambaa wamekosa imani na Mbunge wa sasa anayemaliza muda wake, Mrisho Mashaka Gambo?

Soma zaidi: Pre GE2025 - Mrisho Gambo: Nitaenda kuwajibu nini wananchi wa Arusha. Jiji kama Arusha linakosaje stendi?
IMG_5422.jpeg
 
Baraza la Madiwani mkoani Arusha kwa pamoja limeridhia na kumuomba Mkuu wa Mkoa huo, Paul Makonda kugombea ubunge kwa jimbo la Arusha Mjini.

Je uamuzi huu wa madiwani wa jimbo hilo ni kwambaa wamekosa imani na Mbunge wa sasa anayemaliza muda wake, Mrisho Mashaka Gambo?

Tupe maoni yako
View attachment 3248208
Masikini Gambo kasalitiwa waziwazi...
 
Madiwani wa Baraza la Halmashauri katika Jiji la Arusha wamemuomba Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda agombee ubunge katika Jimbo la Arusha Mjini kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika October mwaka huu 2025.

Madiwani hao akiwemo Naibu Meya wa Jiji la Arusha Abraham Mollel na Diwani wa Kara ya Themi Lobora Petro wakiongea kwenye kikao maalumu cha Madiwani cha kujadili bajeti wamesema kuwa kwa namna Makondq anavyogusa Watu muda ukifika anatakiwa achukue fomu.

“Tunakaa na Watu wanasema kwa namna unavyogusa Watu, sisi tunakaa na Wananchi na wanazungumza mengi dhidi yako ikikupendeza vuta fomu, tuko nyuma yako chukua haya maneno endelea kutafakari wewe ni muombaji” —-Abraham Mollel, Naibu Meya Jiji la Arusha

Hata hivyo Mkuu huyo wa Mkoa Paul Makonda hakujibu chochote baada ya hoja hizo za Madiwani lakini awali wakati anaongea na Madiwani hao katika kikao hicho cha bajeti alitoa maagizo kwa Mkuu wa Wilaya kufuatilia tuhuma za baadhi ya Watumishi wanaodaiwa kufanya upigaji wa fedha Tsh. million 200.

 
Hahaha hata KIGAMBONI waliwahi kumuomba agombee.

Kila anakokwenda anaombwa yeye tu. Alipokuwa Bench Hakuombwa na yeyote.

Rushwa ni zaidi ya oxygeni Tanzania, tunahitaji rushwa zaidi ili kupata japo kiasi kidogo kutoka kwa watawala kupunguza ukali wa maisha.
 
Kwani ubunge na ukuu wa mkoa upi unyama?
Ubunge unyama sana na una maposho na marupu rupu mengi na ana nafasi pia ya kuukwaa unaibu au uwaziri kabisa , ukuu wa mkoa ni uchawa na anacho faidi mkuu wa mkoa ni kuweka wenzie ndan kwa saa 24 na kupigiwa saluti na maaskari tu. Ila hakuna lolote huko kwenye ukuu wa mkoa zaidi ya kulewa misifa tu akiwa mbele ya maafande na kuwaamrisha
 
Back
Top Bottom