Madudu ya Mkataba wa Bandari yazidi kuonekana. Rais alisaini kwa niaba ya Serikali ya Dubai pia

Madudu ya Mkataba wa Bandari yazidi kuonekana. Rais alisaini kwa niaba ya Serikali ya Dubai pia

Imetokea kwa bahati mbaya au ilikuwa imepangwa na waarabu DPW kwa ujanja wao au ni uvivu wa wanasheria wetu kusoma kilichoandikwa kwa makini, na ni nani hasa aliandaa andiko hili. —-AND—.

View attachment 2686950.
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

CHOMBO CHA NGUVU KAMILI

MIMI SAMIA SULUHU HASSAN, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, KWA HAPA NAMRUDISHA NA KUMWEZESHA, Mhe. PROF. MAKAME MNYAA MBARAWA (Mb) Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Akiwa mjini Dodoma, Tzania, kutia saini kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Dubai Kuhusu ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kwa ajili ya maendeleo. na kuboresha utendaji wa bandari za bahari na maziwa nchini Tanzania.

Imefanyika Dodoma, Tanzania siku hii...... Elfu Mbili Ishirini na Mbili tarehe 3 Oktoba, mwaka

srow: H.E. SAMIA SULUHU HASSAN RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
KWqm
Imetokea kwa bahati mbaya au ilikuwa imepangwa na waarabu DPW kwa ujanja wao au ni uvivu wa wanasheria wetu kusoma kilichoandikwa kwa makini, na ni nani hasa aliandaa andiko hili. —-AND—.

View attachment 2686950

D P World yawezekana ni watanzania wameamua kupitia mlango wa nyuma ili wapige pesa ndefu.

Kwa kuwa bunge haramu limeupitisha, basi jaji mkuu aunde tume kuchunguza huu mkataba.
Huyo Jaji mkuu ataanzia wapi ilihali kaongezewa muda wa kumalizia kulamba asali aliyoisaza?
 
kwahiyo dubai hawakusaini au vipi? tuliingia mkataba na nani sasa?
Mhe. PROF. MAKAME MNYAA MBARAWA (Mb) Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Akiwa mjini Dodoma, Tzania, kutia saini kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Dubai Kuhusu ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kwa ajili ya maendeleo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ufafànuzi upi zaidi kijana kwani mkataba unasainiwa baina ya nchi zipi?
Huu mkataba ndiyo umthibitisha Serikalini tuna watu wenye upeo na uelewa mdogo kwa kiwango gani!!

Hata wanaoushabikia ni wale wenye uelewa suni kama akina Musukuma na Kibajaji.

Yaani mtu anaandaa document ya kusaini Rais lakini ina makosa mengi kupindukia.
 
Usikute maana UVCCM wote wanafanyaga wanatoka makumbusho kumbe hata gate la kuingili wala lamkutokea hawayajui!
uvccm ya miaka hii inaundwa na vijana hovyo kabisa. Akili yao muda wote inawaza uteuzi tu kupitia njia ya U CHAWA.

Siku hizi hawana tena mawazo mbadala! Hawawezi kuikosoa serikali yao pale inapokengeuka!! Wao muda wote ni kusifia tu.
 
Imetokea kwa bahati mbaya au ilikuwa imepangwa na waarabu DPW kwa ujanja wao au ni uvivu wa wanasheria wetu kusoma kilichoandikwa kwa makini, na ni nani hasa aliandaa andiko hili. —-AND—.

View attachment 2686950.
EeeeenHeeeee!

Lakini wao watasema hapo hakuna tatizo lolote!
Nchi imefikia kiwango cha ujinga wa kutisha sana.

Ndio akina mawakili , akina Hamza hao.
 
Kuna Uzi nimesoma mdau mmoja kasema hii ishu ya bandari ni kikundi kidogo Cha mafisadi wanataka kujimilikisha bandari Kwa njia ya dp world inawezekana ni kweli maana haiwezekani rais wetu anasaini pande zote mbili Kwa kweli nikichekesho
Amesaini na jicho kubwa pamoja na ile miwani yake yenye magnification x 4000 .lakin akasaini ujinga
 

Mmekazana sana na mambo yasiyo na kichwa wala miguu kwenye huo mkataba kama sehemu ya matatizo.

Pitia article 18 ya ‘VCLT 1969’ hizo signature ndani ya huo mkataba hazina nguvu zozote za kisheria pekee yake, bila ya ratification.

Nguvu ya kisheria kwenye treaty inakuja baada ya ratification ya bunge. Vinginevyo mikataba yote ya baadae terms zake ambazo zipo kwenye treaty azitambuliki mahakamani kama ratification aikufanyika.

Kwanza nchi ingeweza ata ikana hiyo treaty (IGA) yenyewe ata kama raisi mwenyewe angekuwa ndio la sign; provided katika muda huo bunge lilikuwa bado alijaridhia.

Yaani watu mmekezana na upotoshaji badala ya kuwabana hawa watu tujue huko mbele ni kipi hawa wakezaji wanatoa, wanarudisha vipi investment yao na win situation kwetu ina sura gani katika hiyo mikataba. Hayo mambo hawajifikia bado au ndio wanajadiliana kwa sasa nyuma ya pazia.

Lakini wapotoshaji mmekazana na mambo yasiyo ya kichwa wala miguu; kuivuruga serikali matokeo yake tunaweza ata kuwatoa umakini kwenye future negotiations ambazo huko sasa wakiingia kichwa kichwa ndio nchi inaenda tandikwa kweli.
Hata hiyi isiyo na nguvu inafaa kukosewa?
 
Huu mkataba ndiyo umthibitisha Serikalini tuna watu wenye upeo na uelewa mdogo kwa kiwango gani!!

Hata wanaoushabikia ni wale wenye uelewa suni kama akina Musukuma na Kibajaji.

Yaani mtu anaandaa document ya kusaini Rais lakini ina makosa mengi kupindukia.
sana tena, uwezo wako ni mkubwa sana, lakini cha ajabu wenye uwezo mdogo ndiyo wanakuongoza!

Kazi ya Mungu haina makosa.
 
Ignorance is the highest order of foolishness .

Shida yenu mnatabia ya kufikiria vitu vichwani kwenu halafu mnadhani that’s how the world works.

Ata mkipewa sheria husika zinazotumika kuandaa hizo treaty na article husika juu ya hoja zenu huo muda wa kusoma amna, halafu mnakadhana na mambo yenu ya uzwazwa.

Nimekutafutia link nyepesi kuelewa mantiki ya hao signatories kwenye hiyo IGA na legal implications bila ya ratification ni zero; ili treaty iwe na nguvu za kisheria lazima iwe ratified na mamlaka husika ambayo ni bunge kwa Tanzania.

Shida yenu ni kulishwa ujinga na kudhani dunia nzima inameza hizo porojo za wanasheria wenu uchwara.
 
Back
Top Bottom