Maelezo kwa ufupi juu ya clip ikionyesha wanajeshi katili wakiua raia

Cha ajabu ni kwamba kuna watu fulani walianza kumfuatilia Amjad ambae ni huyo muuaji, wakamfuatilia hadi wakagundua alikuwa anatumia mtandao wa kijamii, wakamuuliza kile amefanya anajisikiaje, jamaa akasema anajivunia na hajutii alichofanya. Baadae akapotea kabisa kwenye social media baada ya kugundua amefahamika, na akatoa vitisho. Baada ya clip kuvuja akakamatwa.

Kuna watu ni katili aisee.
 
Duuh ila yeye si yupo kutekeleza maagizo anayopewa na wakuu wake maana yake huenda serikali imemficha tu kupooza umma ila uhalisia kuna God father nyuma yake /yao
 
Toka utawala wa JKN
 
Duuh ila yeye si yupo kutekeleza maagizo anayopewa na wakuu wake maana yake huenda serikali imemficha tu kupooza umma ila uhalisia kuna God father nyuma yake /yao
Sahihi hawezi fanya kitu kama kile pasipo order maalumu toka juu, ukizingatia alikuwa na wenzake, ni tukio liliandaliwa na wakubwa makusudi.
 
Nchi gani kuna demokrasia duniani ?
 
Serikali zote duniani ni za kinyama gusa maslahi ya mapapa wa nchi ndio utajua moto haulambwi
Ni sawa lakini kuna nchi unaweza ongea mambo fulani ukabaki salama, kuna nchi ukimsema kiongozi hata kama ni ukweli, probability yako kuendelea kupumua masaa 72 yajayo ni 1/1000.

Siwezi kukubishia hata Snowden alikimbia US baada ya kutoa siri nzito, lakini kwa level waliopo America na Ulaya bado sana kwa nchi zingine nyingi kufika walipo katika free of speech na democracy.
 
Nchi za Ulaya na America wamejitahidi kwenye demokrasia.
Demokrasia gani waliyo jitahidi marekani Assange tu mpaka leo anaishi kama digi digi.

Hao ulaya unyama walio fanyia babu na bibi zako ni kwamba umesahau au hujui historia ?

Unyama anao fanya marekani hapo middle east kwa kushirikiana na dikteta mwenzake Israel huoni ?

Mauaji ya Marekani Vietnam unayafahamu ?
 

Hawa ndio FaizaFoxy umwambii kitu kuhusu Mwarabu, ndugu katika Imani.

Cc: MK254
 
Hizi nchi zilizopo mashariki ya kati mpaka huko uarabuni sijui zina watu wa aina gani. Kuua kwao ni kama kunywa chai.
Hapa tunawaonea. Haya yapo hata Afrika. Ni vile hizi zimevuja. Kusema kweli Afrika na Asia kuna mambo ya hovyo sana kutokana na haki za binadamu kutokua ishu pande hizo.
 
Hakuna nchi yenye hizo taka taka democracy na free speech kama propaganda ulizo lishwa na vyombo vyao vya habari nawe ukaaamini.

Futa mawazo ya free speech dunia hii ya kibepari, bepari hana huruma na anaye fichua maovu yake.
 
Hapa tunawaonea. Haya yapo hata Afrika. Ni vile hizi zimevuja. Kusema kweli Afrika na Asia kuna mambo ya hovyo sana kutokana na haki za binadamu kutokua ishu pande hizo.
Haya mambo yapo dunia kote sio Afrika,sio Asia, sio ulaya wala sio Amerika.

Serikali za dunia zimejaa damu za watu
 
Ndio demokrasia haiwezi zuia watu kuchinjwa hovyo
Kama haiwezi basi siyo demokrasia bali demokrasia bandia. Nimeishi nchi za Scandinavia zenye demokrasia ya kweli na jambo kama hili haliwezi kutokea.
 
Halafu kuna watu wanadiss western countries.
Kudadeki hakuna kitu sipendi kama kuuana bila hatia.
Kwangu ni mara 100 huo ushoga wanaoupromote western ila sio kuuana kama kuku.
Kuzikana kama mnyama aliekufa kwa ugonjwa, sote nchi moja, race moja lakini unaua na kumchoma moto, Really!!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…