100 others
JF-Expert Member
- Aug 5, 2017
- 4,766
- 16,191
- Thread starter
-
- #41
Huwezi linganisha uhuru wa kuongea uliopo US na North Korea, hapo napo utabisha.Hakuna nchi yenye hizo taka taka democracy na free speech kama propaganda ulizo lishwa na vyombo vyao vya habari nawe ukaaamini.
Futa mawazo ya free speech dunia hii ya kibepari, bepari hana huruma na anaye fichua maovu yake.
Watu wanauliwa toka 1948 utakuwa huo mchezo wa kuigiza?
Sasa western kwani hayo hawafanyi ?Halafu kuna watu wanadiss western countries.
Kudadeki hakuna kitu sipendi kama kuuana bila hatia.
Kwangu ni mara 100 huo ushoga wanaoupromote western ila sio kuuana kama kuku.
Kuzikana kama mnyama aliekufa kwa ugonjwa, sote nchi moja, race moja lakini unaua na kumchoma moto, Really!!?
Hii clip nimeiona kutoka kwenye uzi alioanzisha mdau anaitwa GoldDhahabu wenye kichwa cha habari Hawa wanajeshi katili ni wa wapi? .
View: https://streamable.com/ly7v6f
Kuna maelezo mengi tofauti na sehemu kubwa si sahihi.
Tukio linaonyesha raia ambao wamefungwa mikono na kuzibwa macho wakikokotwa na askari, pasipo raia hao kujua wanaelekea wapi au pengine wakifahamu wanaelekea mahala salama wanaangukia kwenye shimo lililoandaliwa tayari na kupigwa risasi vichwani, baada ya askari hao kumaliza kuwapiga risasi mmoja baada ya mwingine, askari hao wakiwa wameshatanguliza matairi ya gari kwenye shimo, wanawasha moto na kuteketeza miili hio.
Hili tukio lilitokea 16 April 2013 nchini Syria katika mji mkuu Damascus, askari wanao onekana kutekeleza unyama huo wanatokea kitengo cha intelijensia katika jeshi la Syria (Military Intelligence Directorate (Syria)), na specifically hao askari wapo katika kitengo kinachohusika na ukatili, utesaji na mauaji pasipo huruma. Yaani kwenye Syrian Military Intelligence kuna hiki kitengo kwa ajili ya utesaji, mauaji na ukatili wa kila aina unaoufahamu.
Syrian Military Intelligence ipo chini ya raisi, inaendeshwa na Bashar Al Assad mwenyewe, kitengo hiki kimekuwa kimetumika pia kwenye siasa hasa kuwakandamiza wale wanaotaka kuleta upinzani lazima cha moto utakiona.
Hii clip imevuja mwaka 2022, inasemekana kuna mtu alipata access ya laptop iliyokuwa na clip hii, akacopy na kuihifadhi, inasemekana ni askari wa Syria.
Aliyetambulika kwenye hii clip ni Major Amjad Yousef ambae anaonekana kuwapiga risasi raia hao pasipo huruma, askari huyu katili inasemekana amejiunga na jeshi mwaka 2004, baadae baada ya mafunzo akajiunga na branch 227 katika Syrian Intelligence Service kitengo maalumu kwa ajili ya utekaji, kutesa na kuua hasa wapinzani katika serikali ya Syria.
Kwa ufupi hao raia wanauliwa kikatili inasemekana hawana kosa, kilikuwa ni kipindi cha mapigano ambapo waasi walikuwa wanakaribia eneo hilo, hivyo askari hao walitaka kuonyesha mfano kwa yeyote ambae atajaribu kuwa upande wa uasi. Raia hao inasemekana waliishi karibu kabisa na eneo ambalo kulikuwa na upinzani.
Raia waliouawa wakati huo ni 41, waliouawa kwenye hilo shimo. Hata hivyo inasemekana waliouawa wengine ni wanakadiriwa 200 au 300 katika maeneo mengine
Baada ya clip kuvuja, Amjad alikamatwa na serikali ya Syria 2022, Amjad amekamatwa pasipo warrant na hajafikishwa mahakamani, wachambuzi wa mambo wanasema kukamatwa kwa Amjad ni kuzuia waliojihusisha na unyama huo waliopo ngazi za juu wasifahamike.
Serikali ya marekani ilitoa sanctions juu ya Amjad Yousef mnamo March mwaka huu 2023 , secreatry of state Anthony Blinken alisema vikwazo hivyo ni kwa ajili ya mauaji hayo yaliyofanyika.
Utofauti upo kwenye unafiki.Huwezi linganisha uhuru wa kuongea uliopo US na North Korea, hapo napo utabisha.
Nchi gani ?Kama haiwezi basi siyo demokrasia bali demokrasia bandia. Nimeishi nchi za Scandinavia zenye demokrasia ya kweli na jambo kama hili haliwezi kutokea.
Taqbir.Watu wanauliwa toka 1948 utakuwa huo mchezo wa kuigiza?
Una amani gani sasa wewe hapa bongo ? Unafikiri kuwa tahira na kondoo la CCM la kukubali kila kitu cha kipumbavu ndio amani au ushenzi ? PumbavuDini no kitu kibaya sana!!
Imani siasa dini madaraka.
So sad!
Ni Bora ccm itawale TU tuwe na amani kuliko wavuruge mambo tuingie huko!
Hai wanaokufa walizaliwa baada ya miezi Tisa tumboni Kuna wanafamilia wanawategemea!!
Hasta hapa Bongo hatujui ni wangapi waliokufa gizani bila kamera kunasa matukio kisa!siasa,imani dini!
Siasa ni imani,Dini,madaraka n.k imani zimeua wengi sana!!
Lakini wanazidiana, hilo lazima tukubali.Utofauti upo kwenye unafiki.
Mmoja ana uhakika hana hiyo free speech mwengine ana nafikiwa anayo huku uhakika hana.
Wanazidiana unafikiLakini wanazidiana, hilo lazima tukubali.
Maumivu hayo ndio wanayoyapata mnaowazushia ushoga na ufiraji humu JF kwa kutumia fake ID. Nao wana mioyo ya nyama, pia wana ndugu na jamaa wanaowaamini na kuwafuatilia. Acheni kudharirisha watu.πππHii clip iliniumiza, na sasa nimeumia zaidi kwa kufahamu kwamba waliouawa hawakuwa na hatia!
Amjad hastahili kuwa hai mpaka hivi sasa, na ingependeza zaidi endapo wangepatikana wote waliotekeleza ukatili huo katika clip.
Ungemuuliza Ben angekuambia. Duniani tunapita, haina maana ya kufanyiana ubaya. Sasa yupo wapi Jiwe? Atakuwa amekutana na Ben Sasa anamuuliza kuhusu Damu yake aliyoimwaga. Wanadamu tunajisahau Sana tukiwa na madaraka na uhai ila kuna siku ya kukutanika njia panda na siku ya hukumu ya Mungu.Hivi hawa washkaji wana familia kweli huko nyumbani yaani watoto au mke aseee !! Watu huwa wanasema kufanya kazi mochwari ni kipengele ila hii kazi ni ya moto asee naona bora hata anayenyonga wafungwa ana nafuu ! Hii kazi hata ukiiacha lazima upate Post Traumatic Disorder.
Hiki kitengo hata kwetu hapa kipo kweli ?
Nakujibu tu kwa staha... tumia akili.Maumivu hayo ndio wanayoyapata mnaowazushia ushoga na ufiraji humu JF kwa kutumia fake ID. Nao wana mioyo ya nyama, pia wana ndugu na jamaa wanaowaamini na kuwafuatilia. Acheni kudharirisha watu.πππ
We hata ukitukana ni sawa ila Maumivu ni yale yale. Kwa nchi za kiafrika bora uuliwe kuliko kusingiziwa u shoga. Fedheha kubwa sana katika jamii. Ebu badilikeni sister. Hamtendei haki wenzenu.Nakujibu tu kwa staha... tumia akili.
Unataka kufananisha udaku na watu wanaouawa kikatili? Uko timamu kweli?
JF watu wana stress sana, mtu anafananisha watu kupigwa risasi na udaku πNakujibu tu kwa staha... tumia akili.
Unataka kufananisha udaku na watu wanaouawa kikatili? Uko timamu kweli?
Ndo iwe kweli hicho tunachokiwaza kuhusu maisha baada ya kifo kiwe kweli na hakimu awepo kweli , isiwe mtu ukifa na biashara imeishia hapo !!Ungemuuliza Ben angekuambia. Duniani tunapita, haina maana ya kufanyiana ubaya. Sasa yupo wapi Jiwe? Atakuwa amekutana na Ben Sasa anamuuliza kuhusu Damu yake aliyoimwaga. Wanadamu tunajisahau Sana tukiwa na madaraka na uhai ila kuna siku ya kukutanika njia panda na siku ya hukumu ya Mungu.
Siku hiyo watu wataona aibu na kulia kilio cha hatari tokana na vitu vya hovyo wafanyavyo.
Kwa muda wangu wa kuishi Duniani, sina mashaka wala wasiwasi wa uwepo wa siku ya Hukumu na maisha baada ya kifo. Sasa mna potoshwa na kudanganywa na yule muovu na mawakala wake ili muamini hakuna hiko kitu. Ile siku ipo bro, ile jioni ipo kaka na ni dhahiri kabisa.Ndo iwe kweli hicho tunachokiwaza kuhusu maisha baada ya kifo kiwe kweli na hakimu awepo kweli , isiwe mtu ukifa na biashara imeishia hapo !!