Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 24,665
- 25,388
Ilifahamika na kuonekana bayana tangu mwanzo, kwamba kiongozi mpya wa chadema hana maono wala mipango madhubuti ya kuendesha chama kwa mipango mikakati maalumu ya kiuchumi na kujitegemea kama vyama vingine vya siasa,
Tazama sasa,
Maelezo marefu kwa muda mrefu kumbe dhumuni na agenda ilikua ni kuomba kuchangiwa pesa za matumizi binafsi, ya kifamilia na za kuongoza chama, dah!.
Sasa ataomba kuchangiwa pesa mpaka lini na wananchi ambao mara zote wanaitwa maskini?
Lini ataweza kujitegemea yeye mwenyewe binafsi bila kuchangiwa? Lini chadema itaanza kujitegemea bila kukopa au kuchangiwa na wananchi maskini na kwa mipango ipi?
Ni mTanzania wa wapi atathubutu kuchagua kiongozi na chama cha siasa asiewewza hata kujitegemea kiuchumi yeye binafsi na chama chake? Huu si utapeli wa wazi kabisa kisiasa ndugu zangu?
Bilashaka yoyote,
waTanzania watakua wameona dhahiri shahiri njaa na mahitaji ya hao matapeli wa kisiasa ilivyowazonga. kiongozi hana hata kumi chakavu. Sasa akipewa uongozi si lazima ashibe kwanza ndio awafikirie wenye njaa wengine na kwa huyu kiongozi mpya wa chadema anaweza kuwasahau kabisa.
Tume huru ya Taifa ya uchaguzi na mfumo mzima wa uchaguzi Tanzania, ambao upo kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi, hauna matatizo hata kidogo, lakini mtoa maelezo wa chadema anajaribu kueleza kana kwamba kuna matatizo makubwa kitu ambacho si kweli.
Uchaguzi mkuu wa kihistoria Tanzania, utafanyika october 2025 bila shinikizo la mpiga kelele au mvuta bangi yeyote na hakuna mabadiliko wala ya sheria wala ratiba ya uchaguzi mkuu na hakuna mleta fujo atakae fanya lolote.
Ni muhimu sana kama chama cha siasa mkajikita kwenye agenda yenu ya kuomba kuchangiwa pesa za pocketi money na za kuendeshea chama chenu kutoka kwa wananchi mnao waita maskini, lakini sio kuhadaa waTanzania kwa kuwapotosha kwa dosari au kasoro za uchaguzi zisizo kuwepo kwenye uchaguzi Tanzania.
sasa nimeamini njaa haina mbabe,
njaa haina adabu na kuombaomba ni uaraibu wa aibu na fedheha sana

Mungu Ibariki Tanzania