Usimwamini sana mtu anaesema nakula nyasi kwa sababu nalazimishwa. Kama ingekuwa wanasema kweli kipigo wanachotembeza kwa wananchi, kwa mfano wakiandamana, kingekuwa sio cha kuua mtu, na hata usingeona jeshi la Polisi mara zote likilalamikiwa kutumia nguvu kupita kiasi. Ungeona wakizuia watu kiungwana. Ingekuwa picha za victims wa Police Tanzania bado zinawekwa Google na kwingine ningekuonyesha hapa uniambie kuwa hao victims waliumizwa hivyo na watu wanaofanya wasiyotaka kuyafanya, hao rafiki zako.
Polisi wetu ni wanyama wabaya kuliko fisi wa mwituni. Kuna mwanamke alitumiwa video clip ya mumewe FFU akipiga mtu, alidai talaka! Alisema hawazii siku mume wake akiamua kumpiga itakuwaje kila akifikiria ile video. Na kosa la mtu huyo aliepigwa ilikuwa kuandamana tu.