Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nimetumia iko poa sana no Leo asbhJaribu kutumia Uber leo ujionee teknolojia inavyokua na kurahisisha mambo
Hongera sana mkuu,endelea kutumia UberNimetumia iko poa sana no Leo asbh
Uber ni the best kwakweli madriver tax wa kawaida wanakuangalia kwanza umevaaje unaenda wapi ndo anakupa bei,bora kutumia Uber
Juzi hapa nimetumia UBER kutoka buguruni hadi kkoo mida ya saa nne usiku hivi. Dereva alikuwa kadada flani karembo around 26yrs ana kaPasso kananukia vizurii.Njiani full story aisee,hadi sikutamani kushuka.
Akawa ananiambia yeye anafanya kazi ya Uber part time, akiwa anatoka kazini kwake ndo anapiga trips kadhaa then anarudi nyumbani.
Cha kushangaza nauli ikasoma buku tano tu
Ubber naipenda sana hasa kwa wafanyabiashara ni ngumu kuchorewa mchezo wa kuibiwa....nipo nairob naitumia mno na bei ni poa nikiwa dar pia naitumia inarahisisha mambo.....mpaka umigie dereva wako akudanganye woi hiyo dereva yupo karib na ulipo muda wote
Nimetumia iko poa sana no Leo asbh
Uber imerahisisha sana maisha yangu
Nimetoka Ubungo stendi hadi Karume usiku wa saa saba kwa elfu nane
Ni kweli usafiri wa UBER ni rahisi ukilinganisha na Taxis nyingine. Mfano kutoka Ubungo kwenda Airport kwa UBER ni 15,000; Taxis nyingine ni 25,000 mpaka 40,000 kutegemeana na unavyojua kuomba punguzo. Toka Ubungo mpaka Bottle majengo pacha ni 12,000 Taxis nyingine hapo ni 30,000 hivi
je kama mhalifu akiforge imei number na akasajiii lain kwa kitambulisho feki....hamuoni kwamba dereva atakuwa kwenye risk....add more security features pleaseKuhusu usalama wako;
Mkuu ili mteja atumie usafiri wa Uber lazima awe amejisajili kwa kutumia namba yake ya Simu, hivyo ni vigumu mtu kufanya uhalifu akijua namba yake ya simu imesajiliwa. Vilevile uber wana taarifa mbalimbali kama IMEI namba ya simu husika, hii inaweza kusaidia kumtrace mteja anapofanya uhalifu kama kuiba gari la dereva wa uber.
Kuhusu kujiunga na Uber kama una gari na dereva; hii unaweza ukafika ofisi za Uber, Viva towers Posta, ukapata maelezo zaidi
Duuuh aisee tumefika mbali kiasi hususani kwny ubunifu wa matumizi ya technologyHabari wanaJamiiforums, baada ya kuona watu wanasambaza tricks za uongo kuhusu usafiri wa Uber nimeshawishika kuelezea kwa kina kuhusu usafiri huu.
Uber ni nini?
Uber ni application inayokuwezesha kupata usafiri wa bei ya chini na salama katika sehemu nyingi za mkoa wa Dar-es-Salaam, kwa kupitia simu yako ya mkononi. Usafiri huu ni wa kutumia magari madogo yanayoweza kubeba kuanzia mtu mmoja hadi watu wanne.
Kujisajili na Uber
Nenda playstore, search 'Uber' utaiona ina icon nyeusi, download kisha ifungue.
Fanya usajili kwa kutumia namba yako ya simu, email na pia utachagua neno la siri.
Kupata punguzo la Tsh6200 katika trip yako ya kwanza
- Nenda Menu kwa kubonyeza mistari mitatu iliyoko juu kushoto,Kisha bonyezaPayments,kisha bonyeza Add promo code , andika tzaba17
- Utaona maandishi ya kijani yakionyesha kwamba utapata punguzo la tsh6200 katika trip yako ya kwanza.
- Nitatoa mfano, safari yako ya kwanza ni kutoka posta hadi magomeni,na gharama yake ni shilingi 7200,basi utalipa sh1000 tu kutokana na hilo punguzo,lakini katika safari ya pili utalipa nauli kamili.
Zingatia
Unaweza kujisajili mara moja tu kwa kutumia hiyo promotion code, ukirudia kujisajili kwa namba nyingine kama baadhi ya watu wanavyopotosha mitandaoni, akaunti yako ya uber itafungiwa na hutaweza tena kutumia huduma za uber
Jinsi ya kutumia Uber kuita usafiri.
Malipo ya usafiri
- Fungua app ya Uber, hakikisha umewasha GPS, itakuletea maandishi 'where to'.Hapo utajaza unapotaka kwenda,mfano 'Magomeni Mapipa'.
- Itakuonyesha kiasi cha nauli inayokadiriwa, na utabonyeza 'Request uberX'
- Hapo hapo,itakuonyesha jina na namba ya gari la dereva atakayekufata hapo hapo ulipo, na ndani ya dk5 atakuwa kashafika.
Umuhimu wa kutumia Uber
- Ukifika 'destination' yako dereva atabonyeza 'Stop trip' kwenye application iliyoko kwenye simu yake, na hapo hapo itaonyesha nauli kwenye simu yako na kwenye simu ya dereva
- Unaweza kulipa kwa Cash(Taslimu) au kwa kutuma Kadi ya benki
- Ni gharama nafuu zaidi ukilinganisha na taxi za kawaida, kwa sababu bei inahesabiwa na mashine yenyewe kulingana na umbali wa sehemu unayoenda, na sio derevaa kujipangia bei kubwa
- Ni salama zaidi, hasahasa usiku, kwasababu dereva wa uber anakuwa amesajiliwa na endapo itatokea tatizo lolote mfano kusahau kitu kwenye gari, dereva anaweza kupatikana kwa haraka
- Inakusaidia kuokoa muda; mfano upo sehemu ambapo hamna taxi,bajaji wala bodaboda, unaweza kuita usafiri na ukakufata hapohapo kwa kutumia app hii.
Asante sana kwa kukumbushia hayo mawili mkuu.Mkuu umesahau haya:-
1. Ukiita gari halafu usiitumie(ukaingia mitini) utachajiwa 3,000/=, yaani account yako itawekewa deni hilo. Siku nyingine ukiita gari inakupa nauli ya kawaida na ile penalt ya 3,000/=. Kama unatoka Mwenge to Ubungo 2,500/= bili itakuja 5,500/=
2. Ushindani unakuja sasa, naona kuna nyingine imeanzishwa inaitwa Taxify, uber boresheni zaidi huyu asiwapiku.
Maeneo ya ndanindani bado ni changamoto,magari hayako mengi sana.Vp huku kwa mtogole nikiita ndani ya dk5 inakua imefika?
App ya uber kwa ajili ya windows phone ipo mkuu.Nenda hapa Get Uber - Microsoft Storekwa siye wa windows phone tunafanyaje kuipata hiyo app?
Ni sahihi kabisa kuwa charged 57000.Nauli ya Uber hukokotolewa kwa kutumia Umbali uliotembea(km) na Dakika ulizotumia katika safari yako.Kwahiyo automatically dereva akibonyeza start trip program inaanza kuhesabu muda; pale mliposimama kwa dk45,app iliongezea charges kwenye nauli ya awaliHivi UBER wana waiting charges?
Nakumbuka tulitoka kimara baruti tukaenda mlimani city tukamwambia atusubiri tufuatilie kitu chap chap then baada ya hapo tutamrudia atupeleke kariakoo. Kwa bahati mbaya tukapoteza muda mule ndani kama dk 45 hivi bila kutegemea tukamrudia akatupeleka kariakoo kupitia ubungo mataa na alipotufikisha kariakoo akadai Tshs 57000 ambayo ndio iliyokuwa ikimwonyesha kwenye app yake thou mim kwa mahesabu ya app yangu uki sum up route zote nilikuwa napata chini ya Tshs 57000
Nakushauri siku nyingine kama unahitaji kukaa sehemu muda mrefu,mwambie dereva aStop trip then kwenye safari inayofata ita usafiri upya.Ukimwambia asubiri gharama inakuwa kubwa sanaHivi UBER wana waiting charges?
Nakumbuka tulitoka kimara baruti tukaenda mlimani city tukamwambia atusubiri tufuatilie kitu chap chap then baada ya hapo tutamrudia atupeleke kariakoo. Kwa bahati mbaya tukapoteza muda mule ndani kama dk 45 hivi bila kutegemea tukamrudia akatupeleka kariakoo kupitia ubungo mataa na alipotufikisha kariakoo akadai Tshs 57000 ambayo ndio iliyokuwa ikimwonyesha kwenye app yake thou mim kwa mahesabu ya app yangu uki sum up route zote nilikuwa napata chini ya Tshs 57000