Maelezo ya kina kuhusu Uber. Usafiri salama na wa bei ya chini kwa mtanzania

Maelezo ya kina kuhusu Uber. Usafiri salama na wa bei ya chini kwa mtanzania

Nimekuuliza inachukua muda gani kwa mtu kupata usajili UBER hujajibu mpaka sasa. Wewe ni msemaji wa UBER au raia tu?
Huduma ya kusajili madreva wapya imesimamishwa kwa sasa mkuu; mpaka December.Samahani kwa kuchelewa kukujibu.
 
Teknolojia inaenda mbele, tusibaki nyuma wadau. Epuka kulipa gharama kubwa,Tumia Uber, ni rahisi,nafuu na salama.
Mhe salama ? Hoja yangu ni kuhusu uwekezaji uber kwa maana wamiliki wa magari kwa kutumia soko la uber.
Ni wazi kwamba hivi karibuni magari mengi sana yanasajiliwa hapo kwenu mengi zaidi yakiwa mapya kabisa yaliyonunuliwa specific kwa ajili hiyo tu.

Na ili kutumia vizuri rasilimali za wadau wenu (wawekezaji/wamiliki na maderva) (wengi wetu wanakopa BANK )na kuleta TIJA kwa wadau woote na kwa muda woote.

SWALI :
1. Je haitatokea siku service supply ikazidi customer demand ? hatimae HASARA kwa wawekejazi ? na hatimaye nyie
2.Ni mikakati gani mlionalo ili wakati woote kuweza ku-balance soko ? najua kuna matangazo
3. Statistics zenu zinaonyeshaje mwelekeo wa soko lenu in near future 1 to 2 yrs ahead ?
4. Vipi kwa kujilinganisha na wenzetu wa miji mingine ya africa iliyotutangulia kama Nairobi, Harare, S. Africa ili kujua sisi tunaelekea wapi ?

Natanguliza shukran na nitafurahi sana kama ajibu yataambatana na DATA za kuthibitisha ili kuleta imani na kuwekeza kwa nguvu kubwa zaidi.
 
Mko vizuri kuna Sikh nilikuwa Kawe pale Tanganyika pekaz nilijaribu, wako fasta nikakuta taxi ziko online zote zipo tayari ndani ya dakika 1 tu nauli kutoka Kawe beach to Kariakoo market 12500/= only,, nilipenda hiyo huduma na wanakupigia simu wenyewe,, kwa sasa nipo home Mbeya, sijui huduma mtaleta lini mikoani?
 
Class D mkuu kwa gari za usafirishaji kama uber haiwezekani maana ile ni Tax...unatakiwa uwe na leseni daraja C3
 
Class D mkuu kwa gari za usafirishaji kama uber haiwezekani maana ile ni Tax...unatakiwa uwe na leseni daraja C3
Iyo c3 naweza nikaipata haina shida ila waswas wangu upo kwenye abiria na kama kwel kuna maslah maana kuna mtu anataka kunipa gari ila yeye hesabu ni 20000 kwa siku je na mim ntabak na kitu nikikomaa mkuu em nielekeze kwa experince yako uliyovyofanya kaz
 
Gari iwe na cc ndogo, iwe na ac, hapo utapiga kazi Tsh 20,000 kwa siku ndogo mkuu... mimi hesabu yangu ilikua Tsh 30,000 na nilikua nalipa na pesa yangu kidogo napata bila shida....komaa chukua kazi iyo
 
Gari iwe na cc ndogo, iwe na ac, hapo utapiga kazi Tsh 20,000 kwa siku ndogo mkuu... mimi hesabu yangu ilikua Tsh 30,000 na nilikua nalipa na pesa yangu kidogo napata bila shida....komaa chukua kazi iyo

K sawa mkuu ahsante ngoja nianze kufanya mchakato wa iyo leseni nione kma ntapata nianze kaz kaka
 
Application yao inakua shida kufanya kazi kwenye Windows phone
nifanyeje kuipata wakuu. Ikifika muda wa kuweka code hua sizipati.
 
Wakuu nataka kuingiza gari langu kwenye biashara ya Uber napenda kujua kama kuna mtu yeyote mwenye kujua jinsi faida inavyopatikana it's like ni how much par month

Thank you
 
Jaribu kuwafuta wenyewe.....nadhan tovut yao INA contact zao
 
Back
Top Bottom