Inachukua muda gani kwa mtu mwenye gari kusajiliwa na UBER ili atoe huduma hivyo kwani namfahamu jamaa yangu mmoja ni zaidi ya mwezi sasa tangu afike ofisini kwenu asajili gari yake UBER, hamjampa jibu mpaka sasaHongera sana kutumia UBER mkuu
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Inachukua muda gani kwa mtu mwenye gari kusajiliwa na UBER ili atoe huduma hivyo kwani namfahamu jamaa yangu mmoja ni zaidi ya mwezi sasa tangu afike ofisini kwenu asajili gari yake UBER, hamjampa jibu mpaka sasaHongera sana kutumia UBER mkuu
Mimi huwa namkodishia mtu. Mfano nipo kazini na nina mgonjwa Muhimbili anataka kurudi nyumbani, huwa nabadilisha pick up location na kuweka Muhimbili, halafu namlipa dereva kupitia MPESA. Nampa maelezo kwa simu. Kwa hiyo waweza fanya ukiwa popote.Ninachoomba uber,wafanye uwezekano:
1:Wakumkodishia gari,mtu aliyeko Dar,wakati nikiwa nje ya Dar.Kwa mfano naweza kusafari nje ya Dar,lakini familia yangu,mke ,watoto,baba,mama na wngineo wako Dar.
2.Uber iweke njia ya kuweza kupata gari anayotaka mteja.Kwa mfano mteja anataka Toyota wish,iwe inajionyesha kabla ya kuita gari.
Mara nyingi inakuwa ile ile au inaweza kuongezeka kidogo, kulingana na muda uliotumia kusafiri; mfano kukiwa na foleni sana basi nauli inaweza ikaongezeka kidogo; sio tofauti kubwa na ya mwanzoni. Mfano inaweza ikaonyesha 6000 na baadae ikawa 6800samahani sijaelewa hapo baada ya kufika(stop trip) itaonyesha nauli hii nauli ni tofauti na ile ya mwanzo inayoonekana kabla ya reqeust?
Rav 4 kilitime 3door mpya inafaa kuwa uber!?Habari wanaJamiiforums, baada ya kuona watu wanasambaza tricks za uongo kuhusu usafiri wa Uber nimeshawishika kuelezea kwa kina kuhusu usafiri huu.
Uber ni nini?
Uber ni application inayokuwezesha kupata usafiri wa bei ya chini na salama katika sehemu nyingi za mkoa wa Dar-es-Salaam, kwa kupitia simu yako ya mkononi. Usafiri huu ni wa kutumia magari madogo yanayoweza kubeba kuanzia mtu mmoja hadi watu wanne.
Kujisajili na Uber
Nenda playstore, search 'Uber' utaiona ina icon nyeusi, download kisha ifungue.
Fanya usajili kwa kutumia namba yako ya simu, email na pia utachagua neno la siri.
Kupata punguzo la Tsh6200 katika trip yako ya kwanza
- Nenda Menu kwa kubonyeza mistari mitatu iliyoko juu kushoto,Kisha bonyezaPayments,kisha bonyeza Add promo code , andika tzaba17
- Utaona maandishi ya kijani yakionyesha kwamba utapata punguzo la tsh6200 katika trip yako ya kwanza.
- Nitatoa mfano, safari yako ya kwanza ni kutoka posta hadi magomeni,na gharama yake ni shilingi 7200,basi utalipa sh1000 tu kutokana na hilo punguzo,lakini katika safari ya pili utalipa nauli kamili.
Zingatia
Unaweza kujisajili mara moja tu kwa kutumia hiyo promotion code, ukirudia kujisajili kwa namba nyingine kama baadhi ya watu wanavyopotosha mitandaoni, akaunti yako ya uber itafungiwa na hutaweza tena kutumia huduma za uber
Jinsi ya kutumia Uber kuita usafiri.
Malipo ya usafiri
- Fungua app ya Uber, hakikisha umewasha GPS, itakuletea maandishi 'where to'.Hapo utajaza unapotaka kwenda,mfano 'Magomeni Mapipa'.
- Itakuonyesha kiasi cha nauli inayokadiriwa, na utabonyeza 'Request uberX'
- Hapo hapo,itakuonyesha jina na namba ya gari la dereva atakayekufata hapo hapo ulipo, na ndani ya dk5 atakuwa kashafika.
Umuhimu wa kutumia Uber
- Ukifika 'destination' yako dereva atabonyeza 'Stop trip' kwenye application iliyoko kwenye simu yake, na hapo hapo itaonyesha nauli kwenye simu yako na kwenye simu ya dereva
- Unaweza kulipa kwa Cash(Taslimu) au kwa kutuma Kadi ya benki
- Ni gharama nafuu zaidi ukilinganisha na taxi za kawaida, kwa sababu bei inahesabiwa na mashine yenyewe kulingana na umbali wa sehemu unayoenda, na sio derevaa kujipangia bei kubwa
- Ni salama zaidi, hasahasa usiku, kwasababu dereva wa uber anakuwa amesajiliwa na endapo itatokea tatizo lolote mfano kusahau kitu kwenye gari, dereva anaweza kupatikana kwa haraka
- Inakusaidia kuokoa muda; mfano upo sehemu ambapo hamna taxi,bajaji wala bodaboda, unaweza kuita usafiri na ukakufata hapohapo kwa kutumia app hii.
Duuh elfu 25 nauli ya basi luxury la Dar to DomKutoka Ubungo hadi Airport kwa Uber ni kati ya 15,000 hadi 17,000. Ukilinganisha na Taxi ya kawaida ni 25000 hadi 35,000
Tumia Uber uepukane na gharama kubwa kama hizo mkuuDuuh elfu 25 nauli ya basi luxury la Dar to Dom
Inafaa mkuuRav 4 kilitime 3door mpya inafaa kuwa uber!?
Ubber naipenda sana hasa kwa wafanyabiashara ni ngumu kuchorewa mchezo wa kuibiwa....nipo nairob naitumia mno na bei ni poa nikiwa dar pia naitumia inarahisisha mambo.....mpaka umigie dereva wako akudanganye woi hiyo dereva yupo karib na ulipo muda wote
Hongera sana mkuu, kutumia UberUbber naipenda sana hasa kwa wafanyabiashara ni ngumu kuchorewa mchezo wa kuibiwa....nipo nairob naitumia mno na bei ni poa nikiwa dar pia naitumia inarahisisha mambo.....mpaka umigie dereva wako akudanganye woi hiyo dereva yupo karib na ulipo muda wote