Amrish Puri
JF-Expert Member
- Dec 11, 2016
- 274
- 379
hapo kwenye kusajir gari itumike kwa ajili ya uber mbona nilijaribu wanasema usajir wangu una shida tatizo nini hasa
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
niliijaribu nikiwa iringa nikaambiwa "sorry,this service is not yet available in your area" nikatoka ndukii[emoji125] [emoji125]Habari kama hii wa mikoani wanaugulia ndani kwa ndani.
Ukilogin inakuandikiajeMbona inanikatalia sasa hivi kulog in jamaan kwa no yangu nimeunstall app nimeinstall tena bado tu tatizo ni hilo
Hongera kutumia huduma za Uber, waambie na wengine tafadhali wajiungeJuzi hapa nimetumia UBER kutoka buguruni hadi kkoo mida ya saa nne usiku hivi. Dereva alikuwa kadada flani karembo around 26yrs ana kaPasso kananukia vizurii.Njiani full story aisee,hadi sikutamani kushuka.
Akawa ananiambia yeye anafanya kazi ya Uber part time, akiwa anatoka kazini kwake ndo anapiga trips kadhaa then anarudi nyumbani.
Cha kushangaza nauli ikasoma buku tano tu
Naomba nije pmUkilogin inakuandikiaje
Sawa mkuuNaomba nije pm
Nimeshakupm mkuuSawa mkuu
[emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3]Naomba nije pm
Asante kwa maswali yako MkuuNinachoomba uber,wafanye uwezekano:
1:Wakumkodishia gari,mtu aliyeko Dar,wakati nikiwa nje ya Dar.Kwa mfano naweza kusafari nje ya Dar,lakini familia yangu,mke ,watoto,baba,mama na wngineo wako Dar.
2.Uber iweke njia ya kuweza kupata gari anayotaka mteja.Kwa mfano mteja anataka Toyota wish,iwe inajionyesha kabla ya kuita gari.
Una nini eti shemela[emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3]
Check mkuuSawa mkuu
Mkuu asante sana ubarikiwe sana sana nimefanikiwakusema ukwlei madereva taxi wajipange sana... gari zao chafu
zinanuka sana
wana lugha mbaya haijawahi tokea
Ni kweli usafiri wa UBER ni rahisi ukilinganisha na Taxis nyingine. Mfano kutoka Ubungo kwenda Airport kwa UBER ni 15,000; Taxis nyingine ni 25,000 mpaka 40,000 kutegemeana na unavyojua kuomba punguzo. Toka Ubungo mpaka Bottle majengo pacha ni 12,000 Taxis nyingine hapo ni 30,000 hiviHabari wanaJamiiforums, Je umeshawahi kutumia usafiri wa Uber?
Kama bado soma hapa na bila shaka utashawishika kuujaribu.
Na kizuri zaidi utapata punguzo la tsh 6200, pale utumiapo Uber kwa mara ya kwanza.
Endapo safari yako ya kwanza itakuwa fupi,na nauli ikawa chini ya 6200 basi utakuwa umepata nafasi ya kusafiri buree bila gharama yoyote.Na ikiwa zaidi utalipa kile kinachoongezeka hapo kwenye 6200 tu.
Uber ni nini?
Uber ni application ya simu inayokuwezesha kupata usafiri wa bei ya chini na salama katika sehemu nyingi za mkoa wa Dar-es-Salaam, kwa kupitia simu yako ya mkononi. Usafiri huu ni wa kutumia magari madogo yanayoweza kubeba kuanzia mtu mmoja hadi watu wanne.
Kujisajili na Uber
Nenda Google playstore, search 'Uber' utaiona ina icon nyeusi, download kisha ifungue.
Fanya usajili kwa kutumia namba yako ya simu na email; pia utachagua neno la siri.
Kupata punguzo la Tsh6200 katika trip yako ya kwanza
Jinsi ya kutumia Uber kuita usafiri.
- Nenda Menu kwa kubonyeza mistari mitatu iliyoko juu kushoto,Kisha bonyezaPayments,kisha bonyeza Add promo code , andika tzaba17
- Utaona maandishi ya kijani yakionyesha kwamba utapata punguzo la tsh6200 katika trip yako ya kwanza.
- Nitatoa mfano, safari yako ya kwanzi ni kutoka posta hadi magomeni,na gharama yake ni shilingi 7200,basi utalipa sh1000 tu kutokana na hilo punguzo,lakini katika safari ya pili utalipa nauli kamili.
Malipo ya usafiri
- Fungua app ya Uber, hakikisha umewasha GPS, itakuletea maandishi 'where to'.Hapo utajaza unapotaka kwenda,mfano 'Magomeni Mapipa'.
- Itakuonyesha kiasi cha nauli inayokadiriwa, na utabonyeza 'Request uberX'
- Hapo hapo,itakuonyesha jina na namba ya gari la dereva atakayekufata hapo hapo ulipo, na ndani ya dk5 atakuwa kashafika.
Umuhimu wa kutumia Uber
- Ukifika 'destination' yako dereva atabonyeza 'Stop trip' kwenye application iliyoko kwenye simu yake, na hapo hapo itaonyesha nauli kwenye simu yako na kwenye simu ya dereva
- Unaweza kulipa kwa Cash(Taslimu) au kwa kutumia Kadi ya benki gharama ikawa inakatwa moja kwa moja
Jaribu Uber leo, uone teknolojia inavyorahisisha mambo; na kupunguza gharama.
- Ni gharama nafuu zaidi ukilinganisha na taxi za kawaida, kwa sababu bei inahesabiwa na mashine yenyewe kulingana na umbali wa sehemu unayoenda, na sio derevaa kujipangia bei kubwa.
- Ni salama zaidi, hasahasa usiku, kwasababu dereva wa uber anakuwa amesajiliwa na endapo itatokea tatizo lolote mfano kusahau kitu kwenye gari, dereva anaweza kupatikana kwa haraka.
- Inakusaidia kuokoa muda; mfano upo sehemu ambapo hamna taxi,bajaji wala bodaboda, unaweza kuita usafiri na ukakufata hapohapo kwa kutumia app hii.
- Ni usafiri bora; magari ya Uber,yanakaguliwa kabla ya kuruhusiwa kutoa huduma, hivyo inakuepusha na kupanda magari mabovu.
Nakaribisha maswali kuhusiana na usafiri huu
Karibu sana, tafadhali wafahamishe na wengine watumie UberMkuu asante sana ubarikiwe sana sana nimefanikiwa
Hongera sana kutumia UBER mkuuNi kweli usafiri wa UBER ni rahisi ukilinganisha na Taxis nyingine. Mfano kutoka Ubungo kwenda Airport kwa UBER ni 15,000; Taxis nyingine ni 25,000 mpaka 40,000 kutegemeana na unavyojua kuomba punguzo. Toka Ubungo mpaka Bottle majengo pacha ni 12,000 Taxis nyingine hapo ni 30,000 hivi