Maelezo ya Polisi kuhusu Panya Road hayaeleweki. Kwanini wanaua na siyo kukamata? Je, ni yale yale ya akina Zombe yanajirudia?

Kama wanaouawa ni panyaroad, ni sawa tu, maana wanapokea sawasawana matendo yao.

Fikiria familia zile zilizopoteza ndugu zao wasio na hatia. Fikiria waliojeruhiwa bila hatia.

Kama una ndugu yako ana mwelekeo wa upanyaroad, mkanye mapema sana.
 
Sawa mtetezi wa panyarodi
 
Tatizo siyo panya road, tatizo ni je hao waliouawa ni panya road? Na ni wapi walipouawa, na hizo risasi zilipigwa wapi, mbona wananchi hawakuzisikia? Tuambiane ukweli tu, maana watu wanapotea ovyo na magari yao hayaonekani, mashuhuda wanatuambia wananchi walisimamishwa na polisi kabla ya kupotea. Hatuwaamini polisi....Mtuambie hao panya road walikuwa wapi mkawaua, sikatai kama ni kweli hawastahili kuishi, lakini tuambieni ukweli polisi wetu.
 
Kama unaona hakuna haja ya kutumia bunduki kwa panga, hao raia wanaovamiwa unadhani hawana hayo mapanga?? Hawajui kutumia mapanga??

Kama raia wanayo mapanga na wanajua kuyatumia mbona wameshindwa kuwadhibiti Hao vijana?

Unataka mtu anayeua ashughulikiwe kwa fimbo sio???

Nenda wewe sasa kapambane nao kwa panga na fimbo huku ukipiga kelele wananchi wakusikie alafu usisahau nakavideo uje kutuonesha, Polisi na bunduki zao wakae pembeni.

Wakiachwa mnapiga kelele, wakishughulikiwa mnapiga kelele.
 
Pongezi kwa jeshi letu la police Safi Sana uweni wote na ww pia inaonekana ni mfuasi wa panya road unastahili pu pu puuu
 
Kama wanaouawa ni panyaroad, ni sawa tu, maana wanapokea sawasawana matendo yao.

Fikiria familia zile zilizopoteza ndugu zao wasio na hatia. Fikiria waliojeruhiwa bila hatia.

Kama una ndugu yako ana mwelekeo wa upanyaroad, mkanye mapema sana.
Jaribu uwakamate wewe. We unafaidika nao tunakujua. Subiri wakukamate wewe ili uwape ushirikiano
ushirikiano
 
Mkuu, na mimi shaka yangu ipo hapo. Je, waliwauwa walipowakamatia, au walienda kuwauwia sehemu nyingine? Isije kuwa hiyo kamata wanaijua wao polisi pekee!
 
Halafu yanatokea mapumbavu yanawatetea Tena hao vibaka na wauaji
Itoshe kusema una kichwa kigumu mno, nani katetea panya rodi? watu wanataka kujua hao wanaouawa ni panya rodi kweli? waliwakuta mtaa upi wakawaua? iweje walishindwa kuwakamata siku zote na intelijensia yao hadi walivyoua ndio wawakamate na kuwaua? hata mi nafurahi kusikia panya rodi wameuawa
 
Vitendo vya polisi vijadiliwe na kupimwa kwa kulingana na PGO yao hapo tutawaweza lakini mkiwa mnawakosoa kwa kutumia harakati za kisisa hamuwawezi kamwe maana wana mbinu nyingi ijapokuwa sio zote zinaingia akilini.

PGO is the only guidance that should always be referred to whenever criticizing some misbehaviors. that inflicts the public. welfare.
 

Suala la muda mazee hao wanaowauwa sio wenyewe halisi wale sio wazembe kias iko pnya halisi huuwAwa na wa2 maana ndo 2naish nao , uhalif wa baadae unaweza zidi wa uko south ,suluhisho vijana wapewe mitaj na kujaliwa
 
Okay vizur,Sasa Kama unataka kujua maelezo yote hayo nenda pale central polisi, au pale makao makuu ya polisi ,

Utapewa maelezo yote,maana ni haki yako kikatiba huwezi kunyimwa kupewa maelezo ya operation zote kuhusu hao panyalodi , wenzio Jana wameenda wamepewa maelezo na yamewatosheleza vizuri kabisa
 
Tatizo Kuna comments humu ni za panya road wenyewe na wazazi wao wanaonufaika na huu uporaji. Kwahiyo lazima walalamike tuu.
Nakubaliana na wewe hawa wauawe tuu hadi waishe au waache.
 
Narudia Tena humu Kuna comments za panya roads na wazazi wanaonufaika na huu uporaji. Watawatetea tuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…