Maelezo ya Polisi kuhusu Panya Road hayaeleweki. Kwanini wanaua na siyo kukamata? Je, ni yale yale ya akina Zombe yanajirudia?

Ni mara nyingi sana inatokea kuona polisi wetu wakisimama kwenye podium kuzungumza na waandishi wa habari, wanachozungumza mara nyingi ni "watuhumiwa walipigwa risasi na wakafa wakikimbizwa hospitali" Wakati huo huo hakuna ushahidi wa polisi kushambuliana na hao wanaowaita wahalifu, wananchi hawaoni na kuhakikisha kuwa kulikuwa na milio ya risasi.

Miaka ya nyuma, Zombe na wenzake walileta hadithi inayofanana na haya yanayoendelea....Kirahisi rahisi wafanyabiashara wakauawa, huku wakisingiziwa ni majambazi, hadi tume ilivyoundwa ikathibitisha kuwa wale ni wafanyabiashara waliopelekwa Mabwe pande na kuuliwa huko.

Sasa haya leo yameshamiri, polisi wanatatua matatizo yao kwa kuua, kwa nini wasiwashike? Kweli kuna asiye na akili akataka kupigana na panga na polisi walio na silaha kali? Katika kipindi cha wiki 3, watu/wananchi 19 wameshapoteza maisha mikononi mwa polisi. Maelezo yao polisi wetu hayaeleweki. Yaani ya kuunga unga tu!

Nani leo hii atawaamini polisi wanaoua watu wasio na makosa? Kwanini wasiwakamate washukiwa wa ujambazi ili waweze kuwataja wauaji wengine? Na mbona hawaonyeshi sehemu kulipokuwepo hayo mapambano? Wanaonyesha mapanga yenye damu (Polisi wanajua ukweli kuwa wanadanganya)

Polisi wetu hamna credibility, mnaua, mnatesa na kuumiza wananchi wasio na hatia. Hakuna anayewaamini kwa matendo yenu.
Ni deterence ambayo haipo kisheria mkuu.
 
Niliplomsikia Mhe. Amos Makala anasema kama kuna mzazi wake ataona kijana wake haonekani aende Polisi au Hospitali kuulizia, nikajua tayari kishaumana[emoji16] na kimsingi ndugu Makala alikuwa anamaanisha wakaulizie Mochwari[emoji23]
 
Ni mara nyingi sana inatokea kuona polisi wetu wakisimama kwenye podium kuzungumza na waandishi wa habari, wanachozungumza mara nyingi ni "watuhumiwa walipigwa risasi na wakafa wakikimbizwa hospitali" Wakati huo huo hakuna ushahidi wa polisi kushambuliana na hao wanaowaita wahalifu, wananchi hawaoni na kuhakikisha kuwa kulikuwa na milio ya risasi.

Miaka ya nyuma, Zombe na wenzake walileta hadithi inayofanana na haya yanayoendelea....Kirahisi rahisi wafanyabiashara wakauawa, huku wakisingiziwa ni majambazi, hadi tume ilivyoundwa ikathibitisha kuwa wale ni wafanyabiashara waliopelekwa Mabwe pande na kuuliwa huko.

Sasa haya leo yameshamiri, polisi wanatatua matatizo yao kwa kuua, kwa nini wasiwashike? Kweli kuna asiye na akili akataka kupigana na panga na polisi walio na silaha kali? Katika kipindi cha wiki 3, watu/wananchi 19 wameshapoteza maisha mikononi mwa polisi. Maelezo yao polisi wetu hayaeleweki. Yaani ya kuunga unga tu!

Nani leo hii atawaamini polisi wanaoua watu wasio na makosa? Kwanini wasiwakamate washukiwa wa ujambazi ili waweze kuwataja wauaji wengine? Na mbona hawaonyeshi sehemu kulipokuwepo hayo mapambano? Wanaonyesha mapanga yenye damu (Polisi wanajua ukweli kuwa wanadanganya)

Polisi wetu hamna credibility, mnaua, mnatesa na kuumiza wananchi wasio na hatia. Hakuna anayewaamini kwa matendo yenu.

Mzee wa Msoga kwa kuwafahamu aliunda tume ya Jaji Kipenka. Siyo hao waliomfuatia.
 
Tatizo la mwandishi wa hii mada ni wale wale wanaoishi ndani ya mageti. Hao panya road wamemuua msichana mwenye miaka 24 akiwa mbichi kabisa mwenye maisha marefu mbeleni.

Unapoandika hizi siasa za haki za binadamu ukumbuke kuwa mama wa binti huyo pengine anasoma hizi makala zako, jiulize unaziumiza vipi hisia zake!.

Hao madogo ni wauaji usipowawahi wanakuwahi wao wanakumaliza. Angalau kinachoendelea kinawapa akili kuwa serikali ipo kazini muda wote.
 
Tatizo siyo panya road, tatizo ni je hao waliouawa ni panya road? Na ni wapi walipouawa, na hizo risasi zilipigwa wapi, mbona wananchi hawakuzisikia? Tuambiane ukweli tu, maana watu wanapotea ovyo na magari yao hayaonekani, mashuhuda wanatuambia wananchi walisimamishwa na polisi kabla ya kupotea. Hatuwaamini polisi....Mtuambie hao panya road walikuwa wapi mkawaua, sikatai kama ni kweli hawastahili kuishi, lakini tuambieni ukweli polisi wetu.
Mmepewa majina. Na maiti zao zimechukuliwa na ndugu zao.
Ungesikia tu malalamiko, na wana haki ya kushtaki ili kujua ukweli.
 
Kwa vile panya road wanavunja nyumba za watu, wanaiba, wanajeruhi na wanauwa watu wasiokuwa na hatia basi acha na wao wauwawe tu.
Tena polisi ongezeni juhudi ya kuwaua hao Panya-road.

Kamateni na kuwaua pia wapiga debe, wavaa mlegezo, wanyoa panki, wavuta bangi na wajinga wengine wote
 
Hata kama polisi watawakamata panya road na kuwaweka nguvuni bado polisi haohao tu mtawalaumu kwamba wanaonea watu kwa chuki binafsi na mtawatetea panya roads kwakuwa your are their masters. Then watarudi uraiani na kuendeleza yaleyale kisha mnaibuka tena "polisi wameshindwa kazi!!" Shem on you! Kama kuna ndugu yako kauawa kimakosa akidhaniwa panya road, miili ipo mochwari, nenda kadai utoe na maelezo ya kwa nini unadhani kaonewa ili hao polisi wawajibike.
Msiwatetee tu huku mtandaoni wakati hakuna anayelalamika ndugu yake kauawa alikuwa hahusiki.
Msiwatishe polisi, mpaka sasa mbona hajitokezi tena!? Acheni hizo.
 
Tazama
images%20(68).jpg
 
Tena polisi ongezeni juhudi ya kuwaua hao Panya-road.

Kamateni na kuwaua pia wapiga debe, wavaa mlegezo, wanyoa panki, wavuta bangi na wajinga wengine wote
Hapa sisi tunazungumzia panya road, hao wengine umewaingizaje hapa?

Lkn pia kama na wao wanahusika katika matukio ya uhalifu wa kuvunja nyumba za raia wasiokuwa na hatia, kujeruhi, kuiba na kuuwa huku wakiwa wamejificha katika kimvuli cha upigaji debe, uvutaji bangi na ujinga mungine basi acha na wao wauwawe.
Maana kuna watu mchana ni wema wanashinda kweny mabasi wakipiga debe, usiku ni makatili wakivunja kujeruhi na kuuwa. So acha waangamizwe mpaka wakose kimvuli cha kujifichia.
 
Panya-road wengi waliokamatwa walipohojiwa waliangikiw ktk makundi hayo. Wauawe tu maana wao pia wameua mpk vikongwe.
Hapa nimekuelewa mkuu, mwanzo nilifikiri unawatetea hawa washenzi.
 
Tatizo ni je hao ni panya road? Polisi wa Tanzania wamedanganya mara ngapi?Ni nani asiyewajua polisi wetu, kuanzia kutekwa kwa MO Dewji, Roma na wengineo. Na zile maiti zilizookotwa kwenye viroba? Hapo bado kesi za kufoji wanazotengenezewa watu wengine wanaoikosoa serikali hizi za CCM.
Sina tatizo kama ni Panya road kweli, lakini tunaijua vizuri polisi yetu.
Kweli kabisa Polisi hawaaminiki hata kidogo usikute wanaouwawa Wala hata sio panyaroad basi tu Polisi hawana weledi hawana mbinu za uchunguzi yaani ni vurugu tu iko siku watanzania wataamka usingizini ndipo watakubali kuwa wengi wa wanouwawa Wala si majambazi mbona kabla hawajashikiwa bango hawakuwa na hizo operesheni?
 
Back
Top Bottom