Maelezo ya Wenje yamenyooka zaidi kuliko tuhuma za Lissu! Huenda Mbowe bado ni mtu sahihi zaidi kuongoza CHADEMA

Wenje ameelezea hilo kwamba ni kawaida duniani kote kutumia watu maarafu au walio karibu na viongozi kushawishi kukwamua mambo yanapokwama, japo hili kweli ni tatizo la kimfumo lakini sio rushwa kama inavyoelezwa na Lissu kwa maana ya "pesa za Abdul".
 
Wenje ameelezea hilo kwamba ni kawaida duniani kote kutumia watu maarafu au walio karibu na viongozi kushawishi kukwamua mambo yanapokwama, japo hili kweli ni tatizo la kimfumo lakini sio rushwa kama inavyoelezwa na Lissu.
Wewe ulivyofikiria Kweli unaona ni kawaida?
Mada yako mbona kama ipo upande wako Mkuu?
 
Wenje anadai walimpelekea document abdul ili averify?

Abdul anaverify malipo ya serikali? Abdul anacheo gani serikalini?
Hili ni tatizo kutokana na mfumo dhaifu wa utendaji haki nchini na urasimu uliopitiliza, hii ndio inapelekea watu kujaribu kutumia "watu wanaowajua watu" lakini pia kwa maelezo ya Wenje Lissu alikuwa pamoja akitoa ushirikiano katika mchakato wote huo wa kumtumia Abdul kushawishi serikali imlipe madai yake halali.
 
Wenje ameelezea hilo kwamba ni kawaida duniani kote kutumia watu maarafu au walio karibu na viongozi kushawishi kukwamua mambo yanapokwama, japo hili kweli ni tatizo la kimfumo lakini sio rushwa kama inavyoelezwa na Lissu.
Dunia gani hiyo wewe unaishi, kuna kesi nyingi watoto wa queen uingereza wameingia matatizo kama hayo .Wahongaji walikuwa wanapitia kwao ila wazungu hawana ushenzi kama huo kwenye hongo. Abdul alijua njia ya kumpata lissu ni kupitia shida yake ya pesa......Hilo tatizo la lissu yalikuwa mazingira tu ya namna ya kumpata....Ndo maana watu wanatekwa...hapo angeweza ata kumteka, kingine ni kwamba lissu aliona usalama wake ni mkubwa nyumbani kuliko kwenda uko hotelini.....huyo Wenje muongo
 
Sahihi kabisa.
 
Huwa namfananisha na Kikwete, hawa ni wanasiasa na wanaifahamu siasa! Lisu ni mwanaharakati siyo mwanasiasa na hataki kujifunza siasa coz haipo damuni kama uhanarakati! Hana tofauti na marehemu Magufuli!
Kuna usahihi kwa kiasi kikubwa.
 
Umeshindwa hata kuandika muhtasari wa maelezo yake, japo kwa sentensi moja au mbili? Uandishi wako mbona wa mhemko sana?

Tutajadilije hapo sasa?
Team Mbowe ni wajinga na hawana hoja mkuu, wazoee tu hakuna namna!.
 
Wenje kajikanyaga kanyaga ovyo ovyo tu hajaeleza kile kinachodaiwa

Mara Abdul alisema Lissu tayari kashalipwa mara wakaenda kwa Lissu wakachukua nyaraka

Hapo kuna kitu behind the scenes tumefichwa.
 
Maelezo ya Lissu kama nimemuelewa vizuri ni haya:
1. Wenje aliongozana na Abdul kwenda nyumbani. Sijui kama alikuwa tayari na appointment na Wenje au la.
2. Alipofika Wenje akamtambulisha Abdul ambae Lissu alikuwa hamjui.
3. Wenje au Abdul wakamwambia Lissu kuna zawadi yake kama atapunguza makali dhidi ya serikali.
4. Ili kuthibitisha kuwa wana nia njema wakamtajia wengine ambao wamepewa zawadi. Ingawa haijasemwa lakini katika hao waliotajwa ni lazima Boss wake Lissu alikuwemo pamoja na wengine.
5. Lissu akawafurumusha na kuwaambia kuwa haongeki.

Inaelekea pia Lissu alishtaki kwa Boss wake lakini kwa mshangao akaona hamna hatua iliyochukuliwa dhidi ya Wenje. Ndio akajua kuwa kweli kuna wakubwa nyuma ya Wenje. Kwa vile alitoa hizo shutma kwenye Kamati Kuu ya chama chake kuna wenzake ambao nao walianza kukosa imani na uongozi wa chama. Halafu, hamadi, huyo huyo Wenje mtoa rushwa anatangaza nia ya kugombea nafasi ambayo Lissu ameishika. Lissu kwa kutambua kuwa Wenje ni mtu wa Boss na kujua uwezo wa Boss wa kucheza foul akajua kuwa kibarua chake kitaota nyasi. Ndio maana akaamua kushambulia nafasi ya Boss kwa sababu alijua hilo hawatalitegemea na attack is the best form of defence. Ndio maana tumefika hapa tulipo.

Amandla...
 
Pia na sisi tumemtazama na kumsikiliza vyema....

Kama umemwelewa na kumwamini Hezekia Wenje akiwawakilisha wenzake waliokula naye mlungula, nachelea kusema kuwa udadisi na ufahamu wako una kasoro...

Kwanini kabla hujaja na conclusion ya namna hii ukajipa nafasi ndogo tu kujiuliza maswali madogo na rahisi tu haya:

1. Tundu Lissu aliumia akiwa kazini. Ni kwanini unadhani serikali haitaki kulipa madai ya fedha za Tundu Lissu alizotumia kujitibu huku akiwa mbunge (mtumishi wa umma) ambaye yuko entitled na haki hiyo ya kutibiwa kwa gharama za serikali...?

2. Kumbe Wenje alimkopesha Tundu Lissu kwenye pesa hizo za matibabu. Na kumbe struggle ya Wenje na wenzake (akiwemo Freeman Mbowe aliyemtuma Wenje) hadi kuamua kujiuza kwa Rais Samia Suluhu Hassan kupitia kwa mwanae Abdul. Sasa kwanini naye anasema hilo leo? Je, Tundu Lissu anajua kuwa anadaiwa na Wenje? Shilingi ngapi..?

3. Hivi, malipo halali ya serikali hufanyika kwa njia wanayotumia Abdul na Wenje?

4. Na je, madai ya Tundu Lissu (fedha za kujitibu alizopaswa kulipiwa na serikali) ni halali au batili/ hayakidhi vigezo vya kulipwa na serikali...?

5. Kama madai yake ni halali kabisa, ni haki yake alipwe fedha hizo, huyu Abdul na Wenje wanaingia hapo kama kina nani? Walikwenda kufanya nini kwa Tundu Lissu? Wana influence gani serikalini?

6. Kama madai ya Tundu Lissu siyo halali, serikali imeshawahi kumjibu kwa maandishi kuwa hutalipwa fedha zako za madai ya matibabu yako kwa hayakidhi vigezo vya malipo 1, 2, 3, 4 nk...?

##Ukiweza kujibu maswali ndiyo utaelewa Hezekia Wenje na Genge lake ni wakweli kiasi gani...!
 
Ropo ropo sidhani kama zinakutosha unaweza mchagua huyo Jamaa.

Uzoefu unaonesha watu dizaini ya Lisu Huwa ni waharibifu kuliko kujenga.

Mbowe atakuwa mjinga sana kuacha chama Kwa mtu wa hivyo .
 
Nipe mfano wa kesi moja ya hao watoto wa malkia huko Uingereza kama lilivyokuwa suala la Wenje, Abdul na Lissu ikawasabishia hao watoto wa malkia kuingia katika matatizo.

Wewe unafikiria leo mama, shangazi au dada yake Lissu akiwa amestaafu anafuatilia mafao/pensheni yake halafu anazungushwa hatamfuata Lissu ili ampigie Waziri husika, Waziri mkuu au hata Rais??

Lissu alipokutana na Rais kuwasilisha madai yake Ubelgiji ulikuwa ni utaratibu sahihi au kwa sababu wanajuana kwa ukaribu na anaweza kumfikia Rais kwa urahisi??, kama ni kufuata utaratibu ilipaswa akomae na bunge na mahakama tu.
 
LISSU ALIJUA WAZI KUWA ANATEGWA NA YEYE AKAONA AWAUMBUE HUKU AKINUFAIKA NA NI KWELI LISSU YUKO MBELE YAO. NI MTU ALIYEONDOA UBONGO WAKE TU NDIYE ATAAMINI KUWA LISSU ALIJUA NA KUAMINI KUWA KUPITIA ABDUL ATAFANIKISHA KULIPWA MADAI YAKE.

WENJE KESHAFUNDISHWA NAMNA YA KUMNASUA ABDUL KWENYE SAKATA HILI NA HUENDA NI YEYE ALIYEWAITA NA KUWAANDAA HAO WANAOMHOJI.
 
Shida ya maelezo ya Lissu ni kuwa yanataka tuamini kuwa Wenje ni mjinga kiasi ya kwenda na mtu kama Abdul kumhonga mtu ambae msimamo wake dhidi ya rushwa na mambo ovyo unajulikana na kila mtu. Ili iaminike, itakuwa basi Wenje anajua kuwa tofauti na sura ambayo Lissu anayotuonyesha wote anahongeka. Hii nayo ni ngumu kuamini. Kitu pekee ambacho Wenje anastahili kuhukumiwa ni poor judgement. Kuto kufikiri optics za kiongozi wa juu wa Chadema kuwa karibu na mtoto wa Mwenyekiti wa CCM. Labda kama alikuwa anatumika kama mole ili apate siri za upande wa pili.

Amandla...
 
Wenje ameelezea hilo kwamba ni kawaida duniani kote kutumia watu maarafu au walio karibu na viongozi kushawishi kukwamua mambo yanapokwama, japo hili kweli ni tatizo la kimfumo lakini sio rushwa kama inavyoelezwa na Lissu.
Abdul aliwahi kuongoza ujumbe wa serekali Uganda.

Anayefikiri Abdul ni sawa na mimi na wewe anajidanganya sana.
 
Well said ndugu...

Haya ndiyo maelezo ya kufikirisha...

And from all angles, yana make sense kwa kiasi kikubwa...

Wenje ktk maelezo yake, obvious ni uongo uliojaribiwa vyema lakini kashindwa kuu - deliver kwa audience inavypaswa....

Na ni kwa sababu siku zote, kuusema uongo huku ukijua ni uongo, huwa ni mtihani mgumu sana...

Sijui kama Yoda atakuelewa hapa....
 
Wenje kasema ukweli akidhani ananyoosha but in reality ni Yuda fresh na lisu has nothing to loose except Truth ndio maana hakuogopa kumtaja hata Chair wake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…