Na ndiyo maana hata muhamad mwenyewe alikiri kuwa hajuwi atatendewa nini siku ya hukumu. Na wanaomfuata hajuwi watatendewa nini siku ya hukumu. Yaani unamfuata mtu ambaye hajui anaenda wapi.
muhammad atawakana wale wote wanaomwamini na kumfuata kwa sababu yeye mwenyewe anasema wazi katika
sura Al-Ahqaf 46:9,
... na wala mimi sifahamu kile nitakachotendewa wala kile ninyi mtakachotendewa. Mimi nafuata tu kile ninachofunuliwa.
Swali ni kwamba, je, kama mtu mwenyewe anakiri kuwa hajui hatima yake wala hatima ya wale wanaomfuata, je, kama ni kweli Mungu wa mbinguni ndiye aliyempatia quran, je, angekaa kimya kweli juu ya suala la HATIMA za wanadamu? Yaani jibu la mtu atakuwa wapi MILELE lingeachwa hewani tu hivihivi? Na kama Muhammad hajui hili na bado anataka watu wamfuate, je, ni hilohilo tu asilolijua au yapo na mengine asiyoyajua? Bila shaka hii inaashiria kuwa yako mengi asiyoyajua.