Al Watani
JF-Expert Member
- Dec 28, 2014
- 22,714
- 34,545
Exactly nafikiri ni muda mwafaka chama kinahitaji fikra mpya na mwelekeo mpya maana mpaka sasa uongozi uko frustrated na umepoteza mwelekeo wa kukitoa chama hapa kilipo kwenda hatua nyingine.
Kweli kabisa, viongozi wa cdm wasituone hamnazo eti kisa tunaikubali cdm basi watafanya mambo kihuni tuendelee kuwasupport. Wanampa nafasi Lowassa toka uchochoroni, kisha anapanda jukwaani hata kuongea hawezi zaidi ya kutegemea umaarufu wa chama kutimiza ndoto zake za kuwa rais, kwa hiyo cdm kimekuwa ni chama cha kutimizia ndoto za wanaccm, kisha wakikosa madaraka wanarudi zao ccm! Katika mazingira hayo kiongozi ameshakaa zaidi ya miaka 15 madarakani na bado analazimisha kuendelea kukaa madarakani eti bila yeye chama kitakufa! Mbowe akae pembeni ili kuiacha cdm kubaki na sifa ya taasisi na sio kundi la wahuni.