Maelfu wamchangia Mbowe katika kampeni ya #MwambaTuvushe ya kumrejesha madarakani CHADEMA

Maelfu wamchangia Mbowe katika kampeni ya #MwambaTuvushe ya kumrejesha madarakani CHADEMA

Vijana wa Chadema Mkoa wa Dar es Salaam wameanzisha kampeni kubwa ya kutaka Freeman Mbowe achukue fomu kwa mara nyingine ya kugombea Uenyekiti CHADEMA.

Kampeni hiyo yenye kauli mbiu #MwambaTuvushe imeungwa mkono na maelfu ya watu ambao wanachanga pesa zao kwa kiwango cha kuanzia mia tano ili kutimiza shilingi milioni 1 ya kuchukulia fomu ya uenyekiti.

Vijana hao wa CHADEMA wameapa kumchukulia fomu na kuzijaza kisha kwenda kumlazimisha kiongozi huyo kuzitia sahihi na baada ya hapo wazirejeshe.

Vijana hao wameamua kuanza kampeni hiyo kabambe baada ya Tetesi kuvuma kwamba Mwenyekiti huyo wa CHADEMA ameamua kutogombea tena nafasi hiyo.

Wafuasi hao wa CHADEMA wametishia kukesha nyumbani kwa Mwenyekiti huyo na kumzuia kwenda popote mpaka atakapokubali kusaini fomu hizo za kugombea Uenyekiti.

Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr Vincent Mashinji alipuliza rasmi kipenga cha uchaguzi mkuu juzi na kutangaza uchaguzi mkuu wa kumpata Mwenyekiti mpya wa chama hicho utakuwa December 18.

=====
Michango ya wadau
Ukinipa majina ya hao vijana wa CHADEMA, nikaangalia majina yao ya ukoo, nitachangia kueleza sababu yao ni nini.
 
Huu ni ubabe umetumika

Mbowe apunguze udkteta

Kwanini achangishe Wakati yeye ni bilionea?
Hutaweza tenganisha siasa hizi na ukabila. Usidanganywe, hapo ni suala la chama chetu. Ubaya sasa kitabaki kuwa cha mkoa mmoja maana nionavyo, Arusha haitawakubalia tena.
 
Ni jambo jema, lakini huyu ndugu ameumizwa sana na utawala kisa tu ni hicho cheo. Natamani angepumzika kupisha mwingine lakini huyu aliyetangaza nia nahisi harufu ya kijani. Hakuna jinsi, SISIEM waendelee kulala na viatu sharti Mbowe awe mwenyekiti, tena napendekeza hadi hapo atakapoona hawezi hata kutembea.
Subili Mbowe arudi madarakani ndo utaelewa ubaya wa kuungwa mkono kikabila. Next Bunge tunakuwa na ACT kama chama kikuu cha upinzani. Ruzuku zitakuwa haba. Ni aibu chama kinachobadili makatibu wakuu lakini siyo mwenyekiti.
 
Hutaweza tenganisha siasa hizi na ukabila. Usidanganywe, hapo ni suala la chama chetu. Ubaya sasa kitabaki kuwa cha mkoa mmoja maana nionavyo, Arusha haitawakubalia tena.
Majina yao ni KONDE BOY huyu Msuk -kma Boy
 
Hata mimi niko tayar! Mbowe amenifunza mengi sana kwenye maisha kupitia ukomavu wake kwenye siasa. ANASTAHILI HESHIMA KUBWA SANA,URAIS,UBUNGE WALA UWENYEKITI HAVIMTOSHI KUMPA HESHIMA ANAYOSTAHILI. MBOWE UNASTAHILI HESHIMA TUU MBINGU NA ARDHI VINAFAHAMU HILI HUJAVIKANYAGA BURE.
Naona sasa Tundu Lissu hana wafuasi tena. Hakuna anayemuunga mkono?
 
Acha porojo wewe

Fanyeni kampeni mtakavyo, ila ukweli ni kuwa muda wa Mbowe kuendelea kuwa mwenyekiti wa cdm umeisha. Ni suala la yeye kuishi tu kwenye demokrasia anayohubiri. Kama una maslahi binafsi na Mbowe na sio maslahi na chama ni lazima umtetee Mbowe kuendelea kuwa mwenyekiti wa cdm. Ni wachache sana ukiacha wenye maslahi na Mbowe ndio wanalazimisha Mbowe aendelee kuwa mwenyekiti. Ni vyema tukailinda cdm kama taasisi na sio kumlinda Mbowe kuwa mwenyekiti. Mimi kama mimi msimamo wangu uko wazi, ni cdm damu kama taasisi na sio cdm mtetezi wa kiongozi, tena kiongozi mwenyewe akiwa amekaa madarakani muda wa kutosha.

Huu mchezo wa kuendelea kulazimisha Mbowe awe mwenyekiti utaigharimu sana cdm. Fanyeni siasa za bei rahisi bila kuangalia madhara yake huko mbeleni. Hili kosa mnalolazimisha hapa ndio tulipiga kelele na kulaani Lowasa kupewa nafasi adhimu ya kugombea urais, tulisema wazi Lowassa hawezi siasa na kaja cdm kusaka madaraka tu na akiyakosa ataharibu haiba ya chama. Na kweli amekosa madaraka, kibaya zaidi karudi ccm. Ni kama aliigeuza cdm kama kondomu. Kosa lile muhusika namba moja ni huyo Mbowe, na bado analazimisha kuwa mwenyekiti. Nasisitiza Mbowe kuendelea kuwa mwenyekiti wa cdm ni kosa kubwa sana la kiufundi cdm wanaenda kulifanya.
 
vijana elf kumi? wanazunguka nchi nzima kuchangisha milioni moja ya form ya mtu bilionare? duh? nisitie neno tena.

Huyu mleta mada ni mfaidiki binafsi wa cheo cha Mbowe, ndio maana hajali ustawi wa chama kama taasisi, bali anajali nafasi ya Mbowe ili aendelee kuwa kwenye mlo. Naamini cdm ni taasisi na inapaswa kuongozwa kitaasisi. Sioni shida yoyote ya Mbowe kukaa pembeni kuruhusu sura mpya, kwani kama ni mazuri kashayafanya sana, na kimsingi ni kama kafikia mwisho wa ubora wake.

Hamna kitu kinanifedhesha kama kiongozi kukaa madarakani kwenye nafasi moja zaidi ya miaka 10, huku Mbowe akiwa na miaka 15 kwenye nafasi hiyo. Kama alishindwa kuaanda succession plan hilo ni kosa lake. Lakini kwenye demokrasia ya kweli, Mbowe hastahili tena kuendelea kuwa mwenyekiti wa cdm kwa sababu zozote zile. Msimamo wangu huu siwezi kuuficha na uko wazi hapa jukwaani, kama nillivyokataa Lowassa kupewa nafasi ya kugombea urais kupitia cdm.
 

Attachments

  • FB_IMG_15715037856934869.jpg
    FB_IMG_15715037856934869.jpg
    43.3 KB · Views: 14
Ccm wamekuwa wakimpigia kampeni mbowe bila ya kujujia, walifanya hivyo wakati wa Lissu alipokuwa anagombea TLS
 
Ccm wengi ndio wanataka mbowe asiwe mwenyekiti ,ila chadema kama chama , chama kinamhitaji zaidi mbowe kuliko mbowe kukihitaji chama
 
Mimi kama mimi msimamo wangu uko wazi, ni cdm damu kama taasisi na sio cdm mtetezi wa kiongozi, tena kiongozi mwenyewe akiwa amekaa madarakani muda wa kutosha.
Ni haki yako kuwa na msimamo huo, na kwa kuwa wewe ni mpenda demokrasia, acha mchakato wa wazi na haki ufanyike, mradi tu isije ikafanyika kama Magufuli anavyotaka kulazimisha watu wafanye anavyotaka yeye.
Huu mchezo wa kuendelea kulazimisha Mbowe awe mwenyekiti utaigharimu sana cdm. Fanyeni siasa za bei rahisi bila kuangalia madhara yake huko mbeleni.
Huku kulazimishana kumetoka wapi? Kama kupo, hilo ndio la kupigia kelele wakati huu, ili uchaguzi wa Mwenyekiti uwe wa haki, bila kujali Mbowe kakaa muda gani kwenye kiti hicho. Wengi wakimchagua kwa haki, nadhani hata wewe hutakuwa na pingamizi hapo.
 
Huo ndio upinzani unaojiita chama Cha demokrasia na maendeleo. Aibu Sana.
 
Ni haki yako kuwa na msimamo huo, na kwa kuwa wewe ni mpenda demokrasia, acha mchakato wa wazi na haki ufanyike, mradi tu isije ikafanyika kama Magufuli anavyotaka kulazimisha watu wafanye anavyotaka yeye.

Huku kulazimishana kumetoka wapi? Kama kupo, hilo ndio la kupigia kelele wakati huu, ili uchaguzi wa Mwenyekiti uwe wa haki, bila kujali Mbowe kakaa muda gani kwenye kiti hicho. Wengi wakimchagua kwa haki, nadhani hata wewe hutakuwa na pingamizi hapo.


Mkuu kiongozi akishakaa zaidi ya miaka 15 kwenye taasisi zetu huku Afrika, ni nadra sana kupita tena kwenye uchaguzi kwa haki. Sisemi hakutakuwa na haki kwenye uchaguzi, lakini sitegemei hiyo haki kwenye huo uchaguzi, hasa kutokana na uzoefu wangu kwa viongozi wa muda mrefu hivyo. Hivi unaelewa nini unaposikia vijana maelfu wamchangia Mbowe kuchukua fomu, ni kweli Mbowe hana hiyo hela ya kuchukua fomu?

Bado nasisitiza hata akishinda kwa haki kama itakuwepo, miaka 15 inatosha sana kwa mtu kukaa madarakani. Hata akishinda kwa haki sioni akiwa na wazo au hamasa mpya zaidi ya alizokuwa nazo huko nyuma. Kitendo tu cha kumpokea Lowassa, na kumpa nafasi adhimu ya kugombea urais dakika za mwisho bila maandalizi sahihi na sasa karejea ccm, ile peke yake ilipaswa kwa kiongozi makini kustep down.
 
Back
Top Bottom