Kweli kabisa, viongozi wa cdm wasituone hamnazo eti kisa tunaikubali cdm basi watafanya mambo kihuni tuendelee kuwasupport. Wanampa nafasi Lowassa toka uchochoroni, kisha anapanda jukwaani hata kuongea hawezi zaidi ya kutegemea umaarufu wa chama kutimiza ndoto zake za kuwa rais, kwa hiyo cdm kimekuwa ni chama cha kutimizia ndoto za wanaccm, kisha wakikosa madaraka wanarudi zao ccm! Katika mazingira hayo kiongozi ameshakaa zaidi ya miaka 15 madarakani na bado analazimisha kuendelea kukaa madarakani eti bila yeye chama kitakufa! Mbowe akae pembeni ili kuiacha cdm kubaki na sifa ya taasisi na sio kundi la wahuni.
Huelewi Political calculations
Hakika unakaosea mkuu, Mheshimiwa Mbowe hachangishi bali vijana mahiri wa chama mahiri ndo wameamua kujichanga baada ya kupata dodoso kua hataki kugombea tena wakati bado anahitajika sana hasa kwa wakati huu wa UDIKTETA wa baba Jeska.Huu ni ubabe umetumika
Mbowe apunguze udkteta
Kwanini achangishe Wakati yeye ni bilionea?
Big Noooo sir, bado tuanimani kubwa sana kwa huyu mheshimiwa hasa kw wakati huu.Leo tunajadili ubabe wa Mh Mbowe
Hata picha yako uliyoweka inaonyesha tu wewe ni Mbabe kaka yeye, Mwache MBOWE MAANA BADO TUNAMHITAJISANA.Mbowe wenu huyo hapoView attachment 1269855
MwanaCCM huwezi kuona jema la CDMExactly nafikiri ni muda mwafaka chama kinahitaji fikra mpya na mwelekeo mpya maana mpaka sasa uongozi uko frustrated na umepoteza mwelekeo wa kukitoa chama hapa kilipo kwenda hatua nyingine.
Mbowe ni shujaaBig Noooo sir, bado tuanimani kubwa sana kwa huyu mheshimiwa hasa kw wakati huu.
Kumbuka ka si busara zake alizorithi kwa babake Nyerere leo tungekua barabarani tukidai kitu HAKI.
Mpika majungu nakuonea huruma sana.Mwache Mbwe aitwe MboweHamna cha political calcutions zaidi ya hongo waliyopewa viongozi wa cdm. Cdm ilikuwa inasifika kwa viongozi wanaoweza kujenga hoja jukwaani, sio huyo mgonjwa mliyemlia hela zake huku akiwa hawezi kuongea hata dakika tano. Ile haikuwa political calculations bali mlicheza kamari, sasa ukicheza kamari ukaliwa inabidi ukae pembeni na huu ni wakati sahihi wa Mbowe kupisha kiroho safi. Huyo Lowassa toka amekuja cdm aliongeza matawi mangapi ya cdm nchini? Mnaleta matapeli kwenye chama, kisha mnalazimisha kuendelea kuwa viongozi ili muendelee kula hela za matapeli wengine wa kisiasa.
Ni jukumu la wenye chama chao kuamua.Siyo blah blah mitandaoniAngepumzika tu, kashakaa muda mrefu aliyoyafanya yanatosha awaachie na wengine
Upo sawa sana, kuna watu humu naona wamekunywa maji ya bendera wanabaki kubwawaja tu.Mbowe ni shujaa
Shujaa akimbii vita.Mandela angeachia Mapambano kabla uhuru ungepatikana?Angepumzika tu, kashakaa muda mrefu aliyoyafanya yanatosha awaachie na wengine
Mpika majungu nakuonea huruma sana.Mwache Mbwe aitwe Mbowe
Shujaa akimbii vita.Mandela angeachia Mapambano kabla uhuru ungepatikana?
Mbowe ccm haina dau la kumnunua km hao wengine
Wapi wanacdm wamelalamikia uenyekiti Wa mbowe nyie mnawashwa nn,mungu wenu mbona ameanza dalili za kukaa zaidi amlioni hiloInawezekana kweli ccm kama chama hakina hela ya kumnunua Mbowe, kwenye hili unaweza kuwa uko sahihi. Lakini ujio wa mwanaccm Lowassa na kupewa nafasi ya juu kabisa ya nchi kupitia cdm huu utetezi wako unakosa nguvu. Hiyo ni sawa na kusema ww ni muislamu dhabiti na hakuna mtu anaweza kukulisha nyama ya nguruwe, lakini mchuzi wake unaweza kunywa kwakuwa utakuwa umekunywa kwa hiari yako! Kama Mbowe aliweza kumpokea Lowassa ccm itamshindwa vipi? Nilikuwa namuamini sana Mbowe kama mlinzi halisi wa cdm taasisi, lakini baada ya blunder ya Lowassa, namuona ni tapeli kama matapeli wengine, hata kama kweli mchango wa Mbowe umeifanya cdm kuwa taasisi kubwa ya kisasa hapa nchini.
Nadhani ni muda sahihi sasa wa Mbowe kupisha nafasi hiyo na kukaliwa na mtu mwingine ili taasisi isonge mbele, miaka 15 inatosha. Kama kisingizio ni kitisho cha ccm ndani ya cdm sio kweli maana Lowassa pia alikuja kwa mwendo kasi na kujua siri zote za chama, na sasa bado Sumaye yupo cdm, hapo kuna siri gani ya kutoifikia hiyo ccm?
Ccm wanamuogopa Sana mbowe kuliko Mungu
Kama wanachama wake awajalalamika sio shidaMkuu uko serious au unapiga propaganda? Vitega uchumi au Miradi mingapi ya Mbowe imeharibiwa tena kwa hujuma za wazi, ni mara ngapi Mbowe kakaa jela na hakuna lolote limefanyika? Leo hii Mbowe na viongozi lukuki wa cdm wana kesi tena za kubambikiwa na wanaweza kufungwa kwa maagizo toka juu, na hakuna lolote litafanyika, hapo hofu ya ccm kwa Mbowe inatoka wapi? Viongozi kibao kuanzia Lowassa, wabunge mpaka madiwani wamerubuniwa na kwenda/ kurudi ccm, hiyo hofu ya ccm itoke wapi kwenye mazingira hayo? Wapinzani wamezuiwa kufanya mikutano na bado wametii, na hivi sasa box la kura linabakwa kimacho macho na hakuna lolote Mbowe kazuia, hiyo hofu ya ccm unaionea wapi kwa Mbowe? Huko bungeni wabunge wa upinzani akiwepo Mbowe, wanadhalilishwa na kufanyiwa uhayawani wote, kama wangekuwa na hofu na Mbowe hayo yangefanyika tena mbele ya macho yake, na yeye akiwa ndio mhanga mkuu?
Nadhani wanacdm tuwe wakweli tu, kwa sasa ni bora kuwa na mwenyekiti mpya ili kuipa cdm haiba na hamasa mpya kama taasisi. Isitoshe Mbowe kashafanya mambo makubwa tena ya kupigiwa mfano ndani ya miaka 15 yake kama mwenyekiti. Na kwa hapo alipofikia na umri wake si vibaya akakaa pembeni, kwani mazuri yake yanaweza kuharibika kwa kushindwa kukubaliana na kanuni ya wakati ukuta. Mbowe kuendelea kuwa mwenyekiti wa cdm sio kwa ubora tena, bali kwa mazoea. Nayasema haya kwa nia njema ya taasisi ya cdm, na sina tofauti yoyote binafsi na Mbowe kwani wala hanifahamu.