JOVITUS KAMUGISHA
Member
- Mar 13, 2013
- 5
- 5
Mwezi uliopita, nilichapisha makala kuhusu Kupanga ni Kuchagua na Kuchagua ni Kupanga. Nashukuru sana kwa wasomaji wangu ambao wamekuwa chachu ya kuandika machapisho haya na mengine mengi. Ningependa kuzungumzia ukuaji katika maendeleo ya jamii.
Moja ya changamoto kubwa tunayokabiliana nayo ni kutofahamu kuwa maendeleo binafsi hayamaanishi ubinafsi au kujiona bora kuliko wengine. Kufanikiwa ni kujenga njia kwa ajili ya wengine pia kufanikiwa - hii ni tafsiri sahihi ya ukuaji, kujiondoa kutoka hali moja na kufikia nyingine, na jinsi ambavyo unagusa maisha ya watu wanaokuzunguka.
Ninachoamini ni kuwa, hakuna mtu anayeweza kufanikiwa peke yake, au kufika safari. Mfano mzuri ni kwa tunaotumia vyombo vya usafiri- kila mmoja anamtegemea mwenzake kuanzia dereva hadi chombo cha usafiri pamoja na wasafiri. Kwa kipindi hiki inabidi tuondokane na fikra ya changu ni changu, katafute chako kwingine kwa maana hakuna aliyeweza kufika safari bila ya msaada wa mtu mwingine.
Ule usemi wa "Kidole kimoja hakivunji chawa" una umuhimu mkubwa katika maisha yetu ya kila siku. Ni muhimu kila mtu kutambua kwamba ukuaji binafsi unategemea pia jinsi jamii inayokuzunguka inavyokuunga mkono, na pia jinsi unavyochangia maendeleo chanya ya jamii hiyo.
Ni mambo gani muhimu ya kuzingatia ili kufikia hatua bora zaidi ya maendeleo ya jamii, kuanzia kwa mtu binafsi?
Kwa Watanzania wengi na waafrika, tuna kasumba ya kuwa na umimi- ingawa ni hali ya kawaida kwa wanadamu kujifikiria wao peke yako, ila mambo yote yanategemea. Ni ukweli usiopingika kuwa hakuna mtu aliyekosa kabisa mpaka akashindwa kuwa msaada kwa mwingine na pia hakuna mtu aliyekamilika kwa asilimia zote
Ni muhimu kujikita katika elimu inayojenga jamii inayokua na jamii ijayo- Mkazo wa kipekee katika elimu ya kujikomboa kutoka katika ujinga, maradhi na umasikini kwa kukisaidia kizazi kinachokua na kijacho katika kufikia malengo yake, kwa kusaidia jamii hii changa na ijayo, tunaweza kutengeneza jamii inayokua katika hali chanya, yenye kupembua na kupambanua mambo kiyakinifu. Si hivyo tu, pia kuacha au kupunguza tabia zisizosaidia maendeleo yetu, kujihusisha zaidi katika shughuli za kimaendeleo, na kuwa na viongozi wawajibikaji ambao wanatilia maanani maendeleo ya jamii nzima.
Mwisho, ni muhimu kujiuliza: BILA JAMII, UBINAFSI UNA FAIDA GANI?

- Kuwa chachu ya mabadiliko kwa wengine. Hakuna njia rahisi ya kufikia malengo yako bila kushirikiana na jamii. Kushirikiana na wengine kunakupa fursa ya kukua kielimu, kifikra, kiuwezo na kijamii.
- Hakikisha unashirikiana na watu sahihi. Kufanikiwa kwako kunategemea sana watu unaowazunguka, iwe kwenye biashara, mahusiano au ofisini.
- Kuwa tayari kusikiliza na kukubali mawazo mapya, lakini pia usiwe mwepesi wa kuyakataa au kuyakubali bila kufanya uchambuzi sahihi.
- Saidia wengine kuvuka vikwazo, hata kama wewe bado unakabiliwa na changamoto. Kusaidia wengine kunachangia pia katika mafanikio yako binafsi- na si lazima uliowasaidia wakulipe kwa mema uliyowafanyia.
- Jifunze kutokana na makosa yako na ya wengine. Makosa yako yasiwe kizuizi cha wewe kushindwa kuanza safari au kuthubutu kufanya kitu ambacho ni sahihi. Makosa ya wengine yawe kwako kama ukumbusho kwako kuwa njia ipi ni sahihi na njia ipi hutakiwi kupita- usingoje kung’atwa na nyoka ndipo ushtuke
- Endelea kujifunza kutoka kwa wengine na kuweka akili yako wazi kwa mambo mapya yanayohusu teknolojia, siasa na mambo mengine. Tafakari ukweli na uongo kwa umakini.
- Kujenga na kudumisha mahusiano mazuri na jamii na kushiriki katika shughuli za kijamii. Mahusiano ya kijamii yanachangia sana katika ustawi wa mtu binafsi na jamii kwa ujumla.
- Kuwekeza katika elimu na mafunzo ya ufundi ili kuongeza ujuzi na uwezo wa kujiajiri au kupata ajira bora. Elimu ni ufunguo wa maendeleo binafsi na maendeleo ya jamii.
- Kujenga tabia ya kujitolea na kushiriki katika miradi, makongamano na programu za kujitolea za kijamii. Kujitolea kunaweza kuleta mabadiliko makubwa katika jamii na kukuza uelewa wa kina wa mahitaji ya jamii. Pia inampa nafasi mtu kujifunza zaidi.
- Kufanya kazi kwa bidii na kwa uadilifu katika majukumu yetu ya kila siku. Uadilifu na kujituma katika kazi zetu kunachochea maendeleo binafsi na kuchangia katika maendeleo ya jamii.
- Kukuza utamaduni wa kuheshimu na kuthamini tofauti za kitamaduni, kijinsia, na kijamii katika jamii. Kuheshimu na kuthamini tofauti kunachochea umoja na maendeleo endelevu ya jamii.