Maendeleo ya haraka ya jiji la Arusha a.k.a Geneva ya Afrika ni mfano wakuigwa

Maendeleo ya haraka ya jiji la Arusha a.k.a Geneva ya Afrika ni mfano wakuigwa

christeve88

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2018
Posts
3,333
Reaction score
5,490
Kwanza poleni kwa matokeo ya Stars ya jana huo ndo mpira nao wakija kwetu tutawapiga tu hamna namna.

Nikiri nina zaidi ya mwaka na nusu tangu niondoke Arusha , sasa nipo Arusha nimeshangazwa na maendeleo makubwa ya makazi na miondombinu mizuri na yakupendeza.

Ni ukweli usiopinga Arusha imebadilika sana na kama uliondoka Arusha miaka kadhaa iliyopita ukija sasa ujue kuna eneo lipya sasa linatwa Morombo huko ndiko mji ulipohamia sasa, na hii ndo kariako ya Arusha, Kwa waliowahi kufika huko watakuwa mashahidi Mbuzi inaliwa sana huku na watu hawalali.

Nimefanikiwa kufika kata ya Muriet kupitia njia ya Ungalimited Uswahilini hadi Dampo, aisee barabara imepigwa lami safi ikichagizwa na taa za barabarani yaani ni raha tupu unaweza dhania haupo bongo.

Nikapita eneo la kwa Pateli nakuta wamama wanachota maji mabomba yakutosha nakumbuka mara ya mwisho naondoka huku kiasi cha mwaka mmoja na nusu ulipita hapakuwa na maji kiasi hiki kulikuwa na bomba moja tu la kijiji.

Umeme nao umezagaa kila kona Muriet na unazidi kuchanja mbuga kuelekea kwenye makazi mapaya huko kando ya barabara mpya na ya kisasa ya East Afrika inayoanzia Ngaramtoni kama sikosei hadi USA RIVER. Barabara imeshatandikwa lami ya kiwangi cha Ulaya nanipana kweli. Sasa ikifunguliwa naona Arusha itapaa sana na jiji la Arusha litapanuka kwa kasi ya 4G.
Kinachovutia zaidi ukiwa kwenye hiyo barabara unalifaidi jiji la Arusha maana majengo yote marefu ya mjini yanaonekana bila chenga.
 
Arusha ikiwa Geneva ya africa mombasa itakuwa nini?
Mbona unawivu mkuu hayo maneno sio ya yangu ni ya Raisi mstaafu wa Marekani Clinton. Alafu usijefika stend ya Arusha ukadhani umefka Arusha mkuu. Arusha imejengwa pembezoni huko hifadhini huko nenda Duluti, Mount Meru, Ngorongoro huko ukajionee majengo ya Nyota tano na uzuri wa Arusha
 
Nilipita na mzungu flan kwenye ile barabara mpya kuanzia ngulelo mpaka tengeru akanambia panafanana sana na Rio Di Janeiro. Kweli Arusha inapendeza
Hiyo barabara ni shida na bado hawajaweka ukoka wakiweka patakuwa balaa tupu. Sema hii ya mianzini kupanda juu ndo kama sijaelewa maana wamepiga lami kipande kidogo tu alafu wakaacha
na nimesikia mwenge ndo ulizindua.
 
Hiyo barabara ni shida na bado hawajaweka ukoka wakiweka patakuwa balaa tupu. Sema hii ya mianzini kupanda juu ndo kama sijaelewa maana wamepiga lami kipande kidogo tu alafu wakaacha
na nimesikia mwenge ndo ulizindua.

Haha hapo ni mgogoro wa mpaka kati ya arusha jiji na arusha vijijin
Lami imepigwa na arusha vijijini ila kipande ambacho hakina lami ni mita 200 za jiji la arusha....
Hiyo ni moja ya changamoto za mpaka kati ya jiji na vijijini
 
S
Haha hapo ni mgogoro wa mpaka kati ya arusha jiji na arusha vijijin
Lami imepigwa na arusha vijijini ila kipande ambacho hakina lami ni mita 200 za jiji la arusha....
Hiyo ni moja ya changamoto za mpaka kati ya jiji na vijijini
Achana na hicho kipande yaani hiyo lami yenyewe ukipanda juu kidogo kama kilometer moja unakuta vumbi
 
Chagueni upinzani. Majimbo yote ambayo CCM imepita hakuna maendeleo kama hayo. Nenda Moshi barabara za lami mpaka vijijini. Angalia Tabora, singida Rukwa Ruvuma yaani barabara ni vumbi tupuù. Nenda Iringa kwa Msigwa barabara unateleza tuuu
 
Back
Top Bottom