Maendeleo ya haraka ya jiji la Arusha a.k.a Geneva ya Afrika ni mfano wakuigwa

Arusha inapaa ...

Screenshot_20181013-163622.jpg
Screenshot_20181013-163700.jpg
 
Mbona unawivu mkuu hayo maneno sio ya yangu ni ya Raisi mstaafu wa Marekani Clinton. Alafu usijefika stend ya Arusha ukadhani umefka Arusha mkuu. Arusha imejengwa pembezoni huko hifadhini huko nenda Duluti, Mount Meru, Ngorongoro huko ukajionee majengo ya Nyota tano na uzuri wa Arusha
Kumbe Bill Clinton ndie aliesema maneno ambayo kimsingi hayana uhalisia, arusha haina airport ya kutua Boeing ya magufuli, arusha gharama ya maisha iko juu kwa sababu ya uwepo wa maeneo mengi ya kitalii.
.
Angesema arusha the goma of africa hapo sawa
 
Katikati ya barabara mpya ya Sakina-Tengeru ni kinyaa tupu...nyasi zile za porini zimeota kabisa .yani jiji linashindwa hata kupanda maua..?? Arusha imezungukwa na mito kila kona
 
Kwanza poleni kwa matokeo ya Stars ya jana huo ndo mpira nao wakija kwetu tutawapiga tu hamna namna.

Nikiri nina zaidi ya mwaka na nusu tangu niondoke Arusha , sasa nipo Arusha nimeshangazwa na maendeleo makubwa ya makazi na miondombinu mizuri na yakupendeza.

Ni ukweli usiopinga Arusha imebadilika sana na kama uliondoka Arusha miaka kadhaa iliyopita ukija sasa ujue kuna eneo lipya sasa linatwa Morombo huko ndiko mji ulipohamia sasa, na hii ndo kariako ya Arusha, Kwa waliowahi kufika huko watakuwa mashahidi Mbuzi inaliwa sana huku na watu hawalali.

Nimefanikiwa kufika kata ya Muriet kupitia njia ya Ungalimited Uswahilini hadi Dampo, aisee barabara imepigwa lami safi ikichagizwa na taa za barabarani yaani ni raha tupu unaweza dhania haupo bongo.

Nikapita eneo la kwa Pateli nakuta wamama wanachota maji mabomba yakutosha nakumbuka mara ya mwisho naondoka huku kiasi cha mwaka mmoja na nusu ulipita hapakuwa na maji kiasi hiki kulikuwa na bomba moja tu la kijiji.

Umeme nao umezagaa kila kona Muriet na unazidi kuchanja mbuga kuelekea kwenye makazi mapaya huko kando ya barabara mpya na ya kisasa ya East Afrika inayoanzia Ngaramtoni kama sikosei hadi USA RIVER. Barabara imeshatandikwa lami ya kiwangi cha Ulaya nanipana kweli. Sasa ikifunguliwa naona Arusha itapaa sana na jiji la Arusha litapanuka kwa kasi ya 4G.
Kinachovutia zaidi ukiwa kwenye hiyo barabara unalifaidi jiji la Arusha maana majengo yote marefu ya mjini yanaonekana bila chenga.

Miji mingi kwa sasa imebadilika hapa Tz, japo utamaduni wetu wa kutojali mazingira unatuangusha. Yani barabara mpyaaaa, lakini, uzuri utabaki kwenye hiyo barabara tu, makazi na shughuli zingine bado zinachukiza miji yetu. Hakuna bustani za kutosha, pia unakuta barabara zina sehemu ya maua ama nyasi au miti, si watumiaji wala mamlaka husika wanaojali. Hapo usisahau mabanda ya maduka yasiyopangwa, mama ntilie n.k, duka linaanzia ndani ,vitu vinapangwa hadi barabarani. Yani unaingia mjini utasema pamepigwa mabomu.
 
Leo BBC walikuwa na programme ya innovation. Nimeiogopa Arusha. Watu wamegundua jinsi ya kukausha matunda na mboga kwa kutumia majiko au drier zinazoendeshwa na solar, wameweza kugundua jinsi ya kutengeneza mafuta ya parachichi na yanakuwa as pure as coconut oil!!!! Big up Wajasiria mali wa Arusha and they were speaking in fluent English not colloquial one. Big up wana Arusha.
 
Kwanza poleni kwa matokeo ya Stars ya jana huo ndo mpira nao wakija kwetu tutawapiga tu hamna namna.

Nikiri nina zaidi ya mwaka na nusu tangu niondoke Arusha , sasa nipo Arusha nimeshangazwa na maendeleo makubwa ya makazi na miondombinu mizuri na yakupendeza.

Ni ukweli usiopinga Arusha imebadilika sana na kama uliondoka Arusha miaka kadhaa iliyopita ukija sasa ujue kuna eneo lipya sasa linatwa Morombo huko ndiko mji ulipohamia sasa, na hii ndo kariako ya Arusha, Kwa waliowahi kufika huko watakuwa mashahidi Mbuzi inaliwa sana huku na watu hawalali.

Nimefanikiwa kufika kata ya Muriet kupitia njia ya Ungalimited Uswahilini hadi Dampo, aisee barabara imepigwa lami safi ikichagizwa na taa za barabarani yaani ni raha tupu unaweza dhania haupo bongo.

Nikapita eneo la kwa Pateli nakuta wamama wanachota maji mabomba yakutosha nakumbuka mara ya mwisho naondoka huku kiasi cha mwaka mmoja na nusu ulipita hapakuwa na maji kiasi hiki kulikuwa na bomba moja tu la kijiji.

Umeme nao umezagaa kila kona Muriet na unazidi kuchanja mbuga kuelekea kwenye makazi mapaya huko kando ya barabara mpya na ya kisasa ya East Afrika inayoanzia Ngaramtoni kama sikosei hadi USA RIVER. Barabara imeshatandikwa lami ya kiwangi cha Ulaya nanipana kweli. Sasa ikifunguliwa naona Arusha itapaa sana na jiji la Arusha litapanuka kwa kasi ya 4G.
Kinachovutia zaidi ukiwa kwenye hiyo barabara unalifaidi jiji la Arusha maana majengo yote marefu ya mjini yanaonekana bila chenga.
Lakini kumbuka Tanzanite za magumashi hazipo tena, wamebakia watalii tu
 
Leo BBC walikuwa na programme ya innovation. Nimeiogopa Arusha. Watu wamegundua jinsi ya kukausha matunda na mboga kwa kutumia majiko au drier zinazoendeshwa na solar, wameweza kugundua jinsi ya kutengeneza mafuta ya parachichi na yanakuwa as pure as coconut oil!!!! Big up Wajasiria mali wa Arusha and they were speaking in fluent English not colloquial one. Big up wana Arusha.
Kwa hyo kuspeak fluent English kwako ni big deal?
 
Big deal sababu sasa hivi watu wangapi wanaweza kwenda kuongea kwenye chombo kama BBC bila mkalimani? Watu hawajiamini ila hawa vijana wa Arusha wanaweza kuongea ngeri, ung'ee bila shida. Kama umeona wivu kafie mbali ndiyo maana maofisini na vitengo vingi tumejaza watu wa Kenya na Uganda mpaka watoto wetu wanafundishwa na hao watu kisa, mnaona kuonge ung'e ni aibu kumbe wavivu.
 
Nadhani una wivu tu.

Hiyo ni sifa ya nyongeza.... Kwanini usimsifie Mtanzania mwenzako kamaanaweza kutengeneza kitu na akakielezea kwa lugha ya kimataifa?
We nae ndyo wale wale wanaoumwa ugonjwa wa colonial mindset disorder ....angeongea kichina wala msingeshoboka kiivi!
 
Back
Top Bottom