Maendeleo ya mtu yana uzuri asilimia 30 tu zinazobakia asilmia 70 ni uchafu mtupu ambao hubaki siri yake maisha

Maendeleo ya mtu yana uzuri asilimia 30 tu zinazobakia asilmia 70 ni uchafu mtupu ambao hubaki siri yake maisha

Pesa tunatafta kwa haki na aman ndo tulichojaaliwa hiki asilimia 30% ....

Lakini zaidi ya hapo ni utapeli, ukahaba, magendo, madawa n.k ambavyo ni sehemu ya 70% ya utajili!

Huo ndo ukweli!
Mfano!
Kuna kelele za bandari! Wanaohusika wataendelea kuwa matajiri hadi vizazi vyao kwa pesa ya kunyonga!

Huu siyo upambanaji kama wetu Bali ni uhalamia!
Usikariri wewe
 
Siyo kwa ubaya lakini!

Naomba kuwatia moyo wenye uwezo mdogo kama mimi wa ugali na dagaa na tembele!

Ukweli ni kwamba sisi tuko bora kuliko hao wanaoonrkana wamefanikiwa!

Tunachofanya ni halali, tunachochuma ni jasho la haki tunagawana na familia maisha yanasonga!

Wanaoonekana wamefanikiwa sana wala siyo wa kuwaonea gere! Wengi wao ni wa kuwahurumia kwa upande mwingine!

Uhalali wa mali zao walizochuma kwa wema ni 30% tu...hizo zingine ni uchafu mtupu, ufisadi, umalaya, ukahaba, wizi, magendo hata ushirikina ni sehemu ya 70% ya mali zao!

1. Wapo wafanya biashara wakubwa wanaishi kwa nguvu za waganga tu, wanalala chini, hawavai chupi ..nguo moja au marufuku zingine!

2. Kuna wanasiasa tunawatamani Leo kisa wamelamba uteuzi, lakini yaliyowahi kuwakuta kabla ya kuteuliwa ukisimuliwa utabakia mdomo wazi! Uchawi, kuchapika na mengine mengi wamepitia wrngine walikwapuamo na magonjwa!

Kiufupi wengi waliofanikiwa sana tusichekelee juu juu kwa mali walizo nazo laiti kama tungejua chimbuko la mali zao tungewapiga marufuku hata kutoa sadaka misikitini na kanisani!

Machoni tunawaaeshimu sana sana! Lakini mafanikio yao yana ufusika kwa 70%

Sisi ni bora kuliko wao hata kama tumefulia lakini familillah siku zinasonga kwa aman ya 30%!

Tukiamua wote tuifanye ile asilimia 70% dunia itatikisika, amani itapotea, nch itatikisika!

Hivyo 30% ya aman ni bora kuliko 70% yao isiyojulikana!

Mungu anatupigania!
🤣🤣🤣🤣Acha kujifariji maskini wewe....nani havai chupi. Acha fikra za kimaskini na za kishirikina. Huo ni wivu wa kimaendeleo. Tafuta pesa na wewe....uchawi haupo. Labda useme ufisadi sawa...🤣Jamani eti analala chini. Ndo mnajidanganya ee
 
Kiufupi wengi waliofanikiwa sana tusichekelee juu juu kwa mali walizo nazo laiti kama tungejua chimbuko la mali zao tungewapiga marufuku hata kutoa sadaka misikitini na kanisani!
Ingawa sio wote lakini kuna Jamaa yangu alikuwa anaishi hapo Kariakoo mtaa wa mtambani. Alikuwa ni jambazi wa kimataifa lakini alikuwa anapendwa sana Msikitini ajabu.

Alikuwa mtoa sadaka na kulea watoto waliokosa mwelekeo mtaani.

Wazee walikuwa wanamwita Baba.
Nyumbani kwake watu hawakatiki.
 
MUNGU huyu huyu tunae muabudu ametoa Maelekezo(kwa aina yake) Namna gani ya ku'make Fortune alaf waumia Wake wanasema ooohh Money is dirty, Behind money there is evil nk. Hamuon kwamb mnamatatizo
Wana akili za kimaskini Sana,
Na vitabu vya dini vinasema kabisa
"Umaskini Ni laana"
"Mungu hafanyi maagano na maskini"
 
Wana akili za kimaskini Sana,
Na vitabu vya dini vinasema kabisa
"Umaskini Ni laana"
"Mungu hafanyi maagano na maskini"
Kumbuka pia bibilia imeandika Tajiri kuuona ufalme wa Mungu ni sawa na ngamia kupenya kwenye tundu la sindano!
Pia bibilia imeandika heri yao maskini wa roho....
 
Punguza negativity mtoa mada,
Struggle is real na watu wanafanikiwa

Ungekua uchawi Ni deal

Sumbawanga, kigoma na gambosh kungeongoza kimaendeleo

Na matajiri kibao nchi hii wangetokea maeneo hayo kuthibitisha kauli zako.
🤣Yaani watu wanaoamini uchawi ndo maskini
 
Siyo kwa ubaya lakini!

Naomba kuwatia moyo wenye uwezo mdogo kama mimi wa ugali na dagaa na tembele!

Ukweli ni kwamba sisi tuko bora kuliko hao wanaoonrkana wamefanikiwa!

Tunachofanya ni halali, tunachochuma ni jasho la haki tunagawana na familia maisha yanasonga!

Wanaoonekana wamefanikiwa sana wala siyo wa kuwaonea gere! Wengi wao ni wa kuwahurumia kwa upande mwingine!

Uhalali wa mali zao walizochuma kwa wema ni 30% tu...hizo zingine ni uchafu mtupu, ufisadi, umalaya, ukahaba, wizi, magendo hata ushirikina ni sehemu ya 70% ya mali zao!

1. Wapo wafanya biashara wakubwa wanaishi kwa nguvu za waganga tu, wanalala chini, hawavai chupi ..nguo moja au marufuku zingine!

2. Kuna wanasiasa tunawatamani Leo kisa wamelamba uteuzi, lakini yaliyowahi kuwakuta kabla ya kuteuliwa ukisimuliwa utabakia mdomo wazi! Uchawi, kuchapika na mengine mengi wamepitia wrngine walikwapuamo na magonjwa!

Kiufupi wengi waliofanikiwa sana tusichekelee juu juu kwa mali walizo nazo laiti kama tungejua chimbuko la mali zao tungewapiga marufuku hata kutoa sadaka misikitini na kanisani!

Machoni tunawaaeshimu sana sana! Lakini mafanikio yao yana ufusika kwa 70%

Sisi ni bora kuliko wao hata kama tumefulia lakini familillah siku zinasonga kwa aman ya 30%!

Tukiamua wote tuifanye ile asilimia 70% dunia itatikisika, amani itapotea, nch itatikisika!

Hivyo 30% ya aman ni bora kuliko 70% yao isiyojulikana!

Mungu anatupigania!
Najaribu kufungua code hivi.
Una maana kus wanasuasa wamepigwa mti japo wanavaa suruali?
Miaka ya nyuma kidogo kuna mchezaji walikuwa wanadai kocha anamsukumia mti ili apate namba.
Haya niliyasikia kijijini kwao anvyokuja home hushiri ndondo.
Nimejaribu tu kufungua code.
 
Katika hii mada kwa namna nilivyomuelewa mtoa mada anamaanisha 30% ya utajiri, sio kwamba wenye hiyo 30% ni maskini, no ila wameridhika na hiko wanachokipata na maisha yanasonga. Kitu ambacho hakitaki ni kuongeza 70% ambazo mara nyingi zinakuwa na makando kando kibao.
Kama we una hustle na unaamini umefanikiwa kwa uaminifu bila janja wala michezo michafu basi ujue huo utajiri wako ndio 30% yako ila ukitaka 70% itakulazimu kuingiza michezo michafu.
Kwa tafsiri ya haraka haraka maskini ni mtu anayeshindwa kukidhi mahitaji yake muhimu kama vile malazi, mavazi na chakula, nje ya hapo we sio maskini, ila ukitaka kuongeza luxuries za kuzidi na kibunda cha kutuna lazima kuna janja janja itakubidi uzicheze.
Can you imagine mtu asiye na luxuries hanywi pombe, hana ufahari wa kuendesha mipira mikali, kujenga mijumba kama hekalu au kula pisikali za mjini, unadhani huyu anaweza kujisumbua kufanya michezo michafu ili apate kibunda cha ziada asicho na matumizi nacho?
Na shida ya vibunda vya design hii havirithiki kizembe ukifa vinayeyuka hata uwe na mrithi genious vipi, atajikuta kinabaki kile cha halal labda naye umrithishe hiyo michezo michafu.
 
Najaribu kufungua code hivi.
Una maana kus wanasuasa wamepigwa mti japo wanavaa suruali?
Miaka ya nyuma kidogo kuna mchezaji walikuwa wanadai kocha anamsukumia mti ili apate namba.
Haya niliyasikia kijijini kwao anvyokuja home hushiri ndondo.
Nimejaribu tu kufungua code.
Watu laiti wangelijua kuna baadhi ya watu wamefika hapo kwa uchafu mwingi wangesikitika
 
Back
Top Bottom