Uchaguzi 2020 Maendeleo yapi CHADEMA wataleta tofauti na ya chama kilichopo madarakani?

Uchaguzi 2020 Maendeleo yapi CHADEMA wataleta tofauti na ya chama kilichopo madarakani?

Hziyech22

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2019
Posts
15,351
Reaction score
21,362
Kuna mambo inabidi ifike hatua muwe mnaongozwa na akili badala ya mapenzi ya vyama au mihemko isiyo na faida siasa sio Kama ushabiki wa mpira siasa inagusa maisha yetu.

Kuna mambo nimeona hapa wakiaminishana eti akiingia Tundu Lissu na CHADEMA kiujumla ndio watakuwa na maisha Bora hiv Nani kakudanganya mwanasiasa yoyote atakuletea chakula,hela mfukoni?

Vijana wamejengewa matarajio makubwa hasa na CHADEMA lakini Kuna mambo ya kujiuliza

1. Je, demokrasia wanayodai CHADEMA Ni kwa manufaa ya Watanzania au kwaajili yao?

Tukija tukiangalia kwenye chama Chao demokrasia ipo? Kama haipo unaamini vipi watakupa wakiwa madarakani?

2. Maendeleo yapi CHADEMA wataleta tofauti na chama kilichopo au zaidi ya chama kilichopo?

Tukiangalia kwenye chama Chao maendeleo gani wameleta kwa watanzania?

Tokea nimfuatilie Tundu Lissu sijawahi kumuona akijitolea kusaidia mwananchi yoyote wa kawaida kupitia taaluma ya uanasheria aliyonayo zaidi anaitumia kwaajili ya chama chake Je unaamini hivi atawasaidia watanzania akiwa madarakani?

Tukija kwa chama chake Cha CHADEMA chama kimekuwa kikiomba kuchangiwa na watanzania pesa pale kikiwa na shida mfano mzuri Lissu wakati amepata majeraha ya kupigwa risasi lakini pia hata kwenye mikutano yao lakini sijawahi kuona CHADEMA wakiamasisha uchangiwaji wa fedha kwaajili ya maendeleo ya wananchi mfano mzuri sijaona wakiamasisha uchangiwaji wa fedha kwaajili ya ujenzi wa shule au kutumia ile ya weakness ya Magu kutakataa wanabukoba kupewa chakula Cha bure baada ya mazao yao kuharibika wao CHADEMA wangeitumia kwenye uchangiwaji na wakisaidiana na wanatz kuwachangia wanabukoba lkn Hilo alikutokea Je unakiamini vipi hiki chama kikishika madaraka kitakuwa na msaada kwa wanatz?

Ngojea nishie hapa maana ninahoja nyingi Sana hayo mambo machache niliyoandika tafakarini vizuri.
 
Watanzania wengi bado wanamawazo ya kusema..(Umeula)

Wengi hawatambui kwamba, mtu ukipata nafasi katika kitengo Fulani, ni kwenda kutumika tena Kwa uaminifu Kwa ajiri ya wengine Kwa kuwa nafasi hiyo angeliweza kuipata mtu mwingine yeyote!!

Kwa hiyo jibu lako ni hili, wataenda kushibisha matumbo Yao tu,

Wewe jibidiishe kutafuta Kula yako na Mungu akusaidie!!

Na ndiyo maana ni ujinga wa Hali ya juu kwenda kuandamana ili mtu aingie pale anapopatamani na mwisho wa siku ninyi mnakuwa walemavu na Wafu halafu Yeye anakwenda kushibisha tumbo lake na kwenda kuwekeza ulaya Kwa ajiri yake na vitoto na vijukuu vyake

Ujinga sipendi
 
Lissu kiujumla hana hoja nzito pamoja na CHADEMA kwa ujumla watanzania sasa hivi wana akili wanachuja mbivu na mbichi kuongoza nchi si rahisi kama wanavyofikiri.

Magufuli ameshaonyesha ni kitu gani anafanya sasa wao hata hawajulikani wanataka kufanya nini maana kampeni zao ni kumsema Magufuli ambaye tayari anachakuonyesha wananchi kafanya nini.

Sasa Lissu anawaonyesha kitu gani alichofanya ? hapo watasema inatakiwa ifanye serikali ni uongo mtupu, wao tayari ni sehemu ya serikali mbunge anapewa hela za jimbo kina Mdee wanazila tu wanaweza kushawishi watu wakachanga kwa matumizi ya Mbowe lakini wanashidwa kushawishi watu wachangie maendeleo.

Sasa wakiingia cha kwanza lazima waondoe uchovu walioupata kwakujilmbikizia mapesa na hazina za nchi mpaka miaka mitano inaisha hakuna walichokifanya Magufuli ameshaanza kufanya sasa anaendelea CDM hata kuanza bado hata kuonyesha mfano tu kuwa wana nia ya kuwasaidia watu hakuna
sasa wanini hao waendelee kupiga tu kelele
 
lissu kiujumla hana hoja nzito pamoja na chadema kwa ujumla watanzania sasahivi wana akili wanachuja mbivu na mbichi kuongoza nchi si rahisi kama wanavyofikiri magufuli ameshaonyesha ni kitu gani anafanya sasa wao hata hawajulikani wanataka kufanya nini maana kampeni zao ni kumsema magufuli ambaye tayari anachakuonyesha wananchi kafanya nini sasa lissu anawaonyesha kitu gani alichofanya ? hapo watasema inatakiwa ifanye serikali ni uongo mtupu, wao tayari ni sehemu ya serikali mbunge anapewa hela za jimbo kina mdee wanazila tu wanaweza kushawishi watu wakachanga kwa matumizi ya mbowe lakini wanashidwa kushawishi watu wachangie maendeleo sasa wakiingia chakwanza lazima waondoe uchovu walioupata kwakujilmbikizia mapesa na hazina za nchi mpaka miaka mitano inaisha hakuna walichokifanya magufuli ameshaanza kufanya sasa anaendelea cdm hata kuanza bado hata kuonyesha mfano tu kuwa wana nia ya kuwasaidia watu hakuna
sasa wanini hao waendelee kupiga tu kelele
Kubambika kesi watu nidyo uongozi?
 
Tokea nimfuatilie Tundu lisu sijawahi kumuona akijitolea kusaidia mwanainchi yoyote wa kawaida kupitia taaluma ya uanasheria aliyonayo zaidi anaitumia kwaajili ya chama chake Je unaamini hivi atawasaidia watanzania akiwa madarakani?
Kama hujui jambo, kaa kimya au uliza uelezwe..

JE, LISSU ALIINGIAJE CHADEMA?

Tundu Lissu alijiunga CHADEMA mwaka 2004.

Mwaka 2003, Lissu alikwenda Tarime kwenye masuala ya madini. Akakutana na Mh. Chacha Wangwe akiwa Diwani wa Tarime akiwa na kesi kumi za jinai. Mh. Wangwe akamwambia Lissu kuwa wanataka kumfunga. Lissu akamwambia aondoe hofu hawataweza.

Mh. Freeman Mbowe akampigia simu Mh. Lissu kumuomba amtetee Mh. Wangwe kwenye hizo kesi zilizokuwa zikifunguliwa kila uchao. Lissu akakubali na akafanya kazi yake kwa weledi wa hali ya juu. Mh. Lissu akasaidia pia kushinda kesi za wananchi wanyonge 366 katika kipindi cha miezi minne tu. Hawa ni wananchi waliokuwa wakiishi pembezoni mwa migodi kabla ya kuswekwa ndani kwa kosa la kuvamia migodi hiyo. Lissu aliwatetea BURE wananchi hawa mafukara na baada ya ushindi wa kesi hizo akatamka-"Uwekezaji umegeuka kuwa unyama Tanzania".

Lissu akaonekana ni mtu asiye na uzalendo na taifa lake kwa kuwasema vibaya wawekezaji ambao serikali ya ccm ilikuwa ikidai walikuwa wakiliingizia taifa mapato makubwa. Hata hivyo, kwa wananchi hao wanyonge, Lissu alionekana ni Mfalme.
Baadae Mh. Mbowe akampigia Lissu na kumuomba asaidie kutafuta wanasheria wengine waingie CHADEMA kama yeye. Lissu akamshangaza Mh. Mbowe kwani bila kupepesa macho, Lissu akasema yeye ni mwanachama wa NCCR MAGEUZI! Mh. Mbowe alistaajabu sana kwani aliamini Lissu ni mwanachama wa CHADEMA. Hivyo, Lissu akamwambia Mh. Mbowe "kama unataka nijiunge nanyi basi najiunga" ndivyo Lissu alivyojiunga CHADEMA.

Tundu Lissu aliendelea na jitihada zake kuwasaidia wananchi waliokuwa wakinyanyasika migodini huku akiacha wateja wenye fedha nyingi Dar Es Salaam.

Kwa Lissu, hakuna kitu kinamuuma moyoni mwake kama akiona mnyonge ana haki lakini anaonewa. Lissu kamwe hawezi kukaa kimya kuona hali hiyo ikiendelea.
 
Maendeleo hayo ni

1. Katiba mpya itakayoweka taasisi Huru zinazofanya kazi kwa Uhuru bila kuingiliwa na mtu yeyote. Mf. Mahakama, Bunge na Serikali

2. Maendeleo ya kweli ya watu kutokana na sekta binafsi kuwa injini ya kuendesha taifa. Hili litaongeza ajira za watu na kuboresha sana maisha ya watu

3. Mfumo bora wa kodi utakaoruhusu biashara kukua, kustawi na kuwa imara kwa kipindi chore.

4. Mfumo bora wa Elimu utakaofanya vijana wetu waweze kuajiliwa ndani na nje ya Tanzania

5. Mfumo bora wa afya hasa Bima ya afya, utakaowezesha watanzania wote kupata huduma bora za afya.

5. Mfumo bora wa miundombinu na mipango miji utakaopanga upya miji yetu na kuifanya iwe mizuri na misafi.

7. Mfumo bora wa pensheni utakaowezesha wastaafu na watu wanaoacha kazi kuishi vizuri bila mawazo
 
jamani kitu muhimu mjue kuongoza nchi siyo kama unavyoongoza familia yako kunamijitu mingine imepinda usipoipeleka kikatili unashangaa inakupanda kichwani

hakuna jipya ambalo lissu anaweza kulifanya na nchi bila kulipa kodi hatpata hata y kulipa mishahara ukilegeza sana kodi umekwisha na mambo ya kufanya ki nchi ni mengi miaka mitano ni michache asitegemee anaweza kumaliza tatizo lakia mtu asiwadanganye
 
Moja ya mambo watakayoyafanya ni kuyaasisi, na kubadilidha mfumo wa elimu ya kukaririsha watu ili iwakomboe Watanzania toka akili mgando kama ulizo nazo wewe mleta mada.
 
Shida ya JF kuna vitoto vingi sana vya 1995-2000 reasoning yao ni ndogo mnooo.

Yaani wewe Domo ahakuharibu akili kabisa.

Yeye analinda maslahi yake, sasa wewe kajambanani unalinda nini.

Ishtoshe watu wanazungumzia haki za raia wewe unaketa habari za CHADEMA.

Hii mentality ndio wanayo CCM wanapambana kuzuia watu na na CHADEMA badala ya kutatua matatizo ya watu.

- Watu wanauliwa na kupigwa risasi

- Watu wanahitaji masoko ya chai, mbaazi, korosho

- Pesa za pension

- Utu na Uhuru wa watu

- Biashara

- Ajira

Maliza masomo halafu hata kufungua YouTube channel hutaweza huku ukiwa unaona Abdallah Bulembo na familia yake wakiteuliwa kwenda kuka 200M na wakati huo wakikwambia JIAJIRI.

Na kama hilo halitoshi utashuhudia msemaji wa Serikali ana vyeo viwili na katibu wa wizara huku akikwambia wewe unaefanyishwa interviews uwanja wa taifa, uchumi umekuwa kwa kasi mnooo.

Sasa wewe takataka unaenuKA maziwa na kukaa kwenye TV ya shemeji kuangalia Wasafi TV huwezi kujua.
Hapa naona umenijibu kishabiki najua umeweka ushabiki wa Chadema ila nimekuuliza hivo vitu ulivyolist hapo chadema ndio itatatua? Mbona Hilo swali limekuwa Ni gumu kunijibu
 
Back
Top Bottom