Super Charged
JF-Expert Member
- Jan 12, 2020
- 947
- 1,710
Hongera kwa uchambuzi mzuri. Ila kumbuka Sheria au Sharia na Desturi nyingi zinazotumika katika Dini ya kiislam zilichukuliwa au kuendelezwa kutoka katika Dini ya Kiyahudi. Mengi unayoyaona yanafuatwa na kuzingatiwa na waislam yapo hivyo hivyo pia katika Dini ya Kiyahudi.
Na mengi ni yapo kama yalivyo kwenye Torati au Taurati ya Musa au yamenyumbulishwa kama walivyonyumbulisha waandishi wa sheria wa wakati ule na kupata sheria zaidi ya 600+++ kutokana na Torati.
Wakristo waliondokana na Sheria hizo kwa sababu nyingi zilikuwa mzigo mzito ambao walilazimishwa kuzitii watu wa chini huku waliozisimamia wakiishi kinafiki.
Ni kama Leo nchi ya Saudi Arabia ambayo inafuata Sharia Kali za kiislam na ni Suni na wananchi wanafuata.. lakini wanaozisimamia ambao ni utawala na familia ya kifalme ya Saudia wanaishi maisha ya kufuru na uchafu wa kila namna. Kila starehe Duniani unayoijua na usiyoijua wanafanya lakini kwao huko wanaonekana ni watakatifu mno maana ni descendants wa mtume.
Utaratibu na Sheria hizo ni nzuri kwa maana ya kuweka usawa kwa wote ingawa zinaweza kuleta changamoto kutokana na mazingira tofauti tofauti ya Ulimwenguni.
Zipo nchi za kiislam ambazo ukienda utashangaa hawafuati kabisa baadhi ya Sheria. Mf. Indonesia, Uturuki, Lebanon Kuna baadhi wanafuata Desturi zao badala ya sheria ya Dini.
Ila kwa ujumla ni nzuri sana Kila Dini ila jambo zuri la pekee ambalo Dini nyingine inaweza kujifunza.
Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
Uyahudi Ni Kabila Hata yesu Alikuwa Myahudi
Wayahudi Wengi Ni wa dini ya Kijeweshi ambayo Asili yake Ni Kuamini Mungu Mmoja asiye asiye Na Mtoto(Haimaanishi kuwa Wao Ni waislamu)
Baadhi ya Sheria zao Zinafanana Na Sheria za Kiislamu Ambazo Zilikuwepo Hata kabla Ya Mussa,Je Ni nani Kakopi kwa Mwenzie?
Sheria Zote za Quran Zimetoka Kwenye Torati na Zaburi Hakuna Anayekataa "Na sio Kwamba Zimeanza Kwenye Torati Tu Na Zaburi,Ufunuo aliofunulia Nabii Adam Nao Ulikuwa Na Mafundisho Kama hayo yaliopo Kwenye torati na zaburi
3:3 Quran "Amekuteremshia Kitabu kwa haki, kinacho sadikisha yaliyo kuwa kabla yake. Na aliteremsha Taurati na Injili"
Uislamu Haujabadili Chochote Kutoka Kwa Nabii Adam Mpaka Mtume Wa Mwisho Muhammad (S.A.W) Hii Ni dalili Tosha Ya Dini Isiyokuwa na shaka Vitu Havibadilishwi
Je Nchi za kiislamu Ni Zipi?Je Zenye Waislamu wengi au vipi Kwa uelewa wako?
Turkey Uliibuka Uislamu Miaka Mingi Baada Ya Kifo cha mtume Muhammad (S.A.W) Miaka 100 au 200 baada Ya kifo chake vivo Hivo Kwa Lebanoni,Indonesia uliibuka baadae.
Turkey kabla ya Kuanguka kwa dollar Kubwa Ya Ottoman walikuwa wakifuata Sheria Za kiislamu vizuri(Kwan Huoni Hata kwenye Tamthilia ya Ottoman Azam two) Ila baada ya Kuanguka Kwa dollar 1923 Waliwekewa vikwazo ikiwemo kutotoa adhana, wanawake Kutovaa Hijab Na Baadhi ya Sheria za Kiislamu zilipigwa Marufuku.
Kama Ulivosema Baadhi Wa turkey,Lebanoni na Indonesia wanafutaka mila zao,Kweli Ni baadhi Si Kila mtu Allah Kamfungulia awe Mcha mungu,Pia kufuata Mila Haimaanishi Kuwa wewe Sio Muislamu au Ni dhambi Kuna mila na Desturi ambazo sio dhambi Kuzifuata Au mafundisho Yake Yanaendana Na quran,
Saudia Kufanya Uchafu na Starehe Kwanza Starehe Sio Dhambi Ila Inategemea Unafanya vipi starehe
Starehe Ya Ngono Kufanya mke Halali Si dhambi,Kufanya Na Mchepuko ndo dhambi(Saudia Hauwezi ingia lodge Na mwanamke Bila cheti cha ndoa)
Starehe Ya Kula na Kunywa Sio Dhambi Ila Kila haramu na Kufuru Ndio dhambi
Starehe ya Kutembea Nje Ya Nchi si dhambi
Starehe ya Kuvaa Sio dhambi.
Waache saudia Wafanye starehe Ila wasivuke mipaka Yao.Hata allah kasema Katika kuitafuta Akhera Usisahahau Dunia yako.
Hata Kama Saudia Wanafanya Dhambi basi Jua Kiyama kiko Karbu maana hakitasimama Kiyama Mpaka Udhalimu,Maovu Yatapakae Dunia nzima.
The Things matter Ni Mafunzo katika dini Ya Kiislamu na sio Waislamu Wanafanya Nini