Maeneo ambayo Waislam wanawapiga Bao Wakristo

Maeneo ambayo Waislam wanawapiga Bao Wakristo

Halafu sijui kuna uhusiano gani kati ya uislamu na biashara.

Walio wengi wa wafanyabishara na matajiri Kinyongo bongo na kiafrika Afrika ni waislam.
nadhani ni suala la kihistoria maana hata mtume muhamad alikuwa merchant.
IMG_20230619_092704.jpg
 
Naunga mkono ila hapo kwenye mahali tu nna chakusema

Ni kweli mahali anataja mlengwa mwenyewe ambaye anatakiwa kuolewa ila siku hizi baadhi ya waislam wengi wanapindisha hapo kwenye mahali naomba wakemewe yaani viongozi wa dini wakemee kipengele cha mahali

Unakuta binti ametaja vizur tu kiwango/kitu anachohitaji kama mahali ila wazee nao wanaongeza wanachotaka kiufupi haipendezi- tunaghahiri sana kuoa kutokana na hali ngumu ya maisha na hawa wazee wa kiislam kuongeza cha juu , haipendezi wakemewe watatuua na kuzini maana binti zao bado wanamiminika maghetoni Kwa masela na wao wenyewe ndio wanatia ugumu
Hivyo ndivyo ilivyo, mahali wazazi ndio wanao panga, maana Binti akisema wanamwambia weka na ya mama na baba, hapa hakuna tofauti ila tofauti viwango tu.
 
Sehemu Nayowapa Credit ni maswala ya UBINADAM(HURUMA NA KUSAIDIA)

Nadhani ni karibia hospital zote kubwa waislam Ndo wenye mchango mkubwa kuwasaidia wagonjwa wote bila kujali itikadi kwa kuwapa vyakula na maji.

Nilishawahi uguzaga Mgonjwa hospital mbili tofauti nikabahatika kuona hiyo hali , ilinivutia sana .Kwani ndani ya wodi alolazwa mgonjwa wangu karibia wote hawakuwa hata na ndugu wenye uwezo wa kukimu mahitaji la mlo kwa mara tatu. Hivyo ukipeleka chakula basi unazidisha angalau nae awape wenzake.Pia kupitia hizo taasisi za kiislam zilifanya wagonjwa wote kupata chakula na maji.

Nilijiuliza ni namna gani wanawasaidia watu katika hali ngumu kama ile huku imani ya pili huku ndo kwanza ni kuchangishana kwenye nyumba za ibada ili kujenga hospital alafu gharama zao ziko juuu.
Sisi tupo vizuri kwa watoto yatima na vituo vya afya vikubwa ni vyetu hata serikali uingilia ku support
 
Wengi wa waislamu ni wanafiki sana hasa Kwa wakristo,ni wamejaa zuluma sana hawana upendo,wavivu na watapeli ,waanaamini kumdhulumu mtu wa imani nyingine kwao siyo dhambi,hawataki kuwajibika hata Kwa watoto wanaowazaa ndiyo maana hukimbilia talaka,ulozi na ugannga ugannga ndio kitu pekee wanaweza kuongoza
Dhulma imekemewa sana kwenye Quran . Na mfanyaji wa dhulma lazima atakuja kuilipa hapa duniani na kesho akhera haijalishi uliyemtendea bi muislamu au si muislam.

Talaka haitolewi kwasababu ya kuwakimbia watoto/majukumu.

Ulozi(uchawi) ni kinyume na uislam. Mtu akifanya ulozi au hata kujifunza tu uchawi anakuwa tayari kashajivua kutoka ktk dini ya Uislam hata kama atakuwa na jina la kiislam.

Ushirikina na Uislam ni mfano wa mashariki na magharibi. Vitu viwili tofauti. Mtu hawezi kuwa muislam na mshirikina kwa wakati mmoja.
 
Hua nikiangalia hizi imani 2 kubwa hapa kwetu ni kama moja ni ya ujamaa na nyingine ni ya ubepari. Moja ikiwa inaamini katika kusimplfy mambo nyingine ikiwa inaamini kwenye kucomplicate mambo.
Hii nyingine ni kama huwezi kwenda peponi bila watu fulani, ni shida sana, hata mtoto anaweza asibatizwe kwakuwa hukutoa zaka. Ni shida sana. Mimi Niko huku ila Kuna vitu havijakaa sawa kabisa. Mungu anamilikiwa na watu fulani.
 
Kulinda imani yao.

Huwezi kusikia dini yao inachezewa ovyo ovyo tu halafu wakakuangalia tu. Yaani msanii muislam yupo tayari kutengenezea maudhui yake kanisani ila sio akachezee msikitini.

mavazi ya kina dada.

hapo wameupiga mwingi sana .
Hawaruhusu hata nukta. Ulijaribu tu unalo. Hakuna upuuzi wa hajui alitendalo. Nachukia sana hii kauli inahalalisha uovu wa makusudi kabisa.
 
unazungumzia sweeden hii wanaondaa kombe la dunia la ngono
Hivi hawa wavaa stara wakienda kutuwakilisha si wanaweza kuleta kombe bongo mkuu?

Hasa ustaadh Kumbuka na Shehe Lokoli wakikaba upande wa upinde lazima tushinde
 

Attachments

  • Screenshot_20230619-091523.jpg
    Screenshot_20230619-091523.jpg
    29.7 KB · Views: 5
  • Screenshot_20230619-093023.jpg
    Screenshot_20230619-093023.jpg
    33.1 KB · Views: 6
Hivi hawa wavaa stara wakienda kutuwakilisha si wanaweza kuleta kombe bongo mkuu?

Hasa ustaadh Kumbuka na Shehe Lokoli wakikaba upande wa upinde lazima tushinde
Sasa una uhakika gn kama hao ni waislamu? Hayo madera hata ww siunavaa tu
 
Ukristo umeharibiwa na mila za kipagani za Wazungu walizochomeka kwenye Ukristo ili kuuchakachua! Baada ya Uamusho sasa hivi Ukristo unarudi katika ile hali ya kwanza ya Ukristo halisi.Ukristo halisi wa Kwanza ni ule uliokuwako wakati wa Yesu na Kanisa lake aliloliacha kabla hajapaa kwenda mbinguni,wakati huo ya Dola ya Kirumi ndiyo iliyokuwa inatawala dunia nzima.Wakati Kanisa la kwanza linaeneza Injili,utawala wa Kirumi baada ya kuona Imani ya Kikristo ni tishio kwa dini zao za kipangani waliangamiza wakristo wengi mno,mpaka wakristo walipofikia mahali (baada ya kuteswa mno) kukubali mafundisho ya kipagani ya Kirumi kuingizwa katika Ukristo ndiyo ikazaliwa Roman Catholic! Vitu kama kuvika maiti suti sijui maua,kuvaa mavazi ya kihuni yasiyo na heshima,nk hivi vyote vimeletwa na wazungu walioleta dini zao nchi masikini na kwingineko.
Yesu hakuacha kanisa kamanda, kanisa limeanzishwa na hao hao warumi.

Yesu aliabudu kwenye masinagogi pamoja na wayahudi wengine na imani yake haikukinzana na imani yao isipokuwa wayahudi hawakutaka kumuamini kama yeye ni Messiah aliyekuja kwao na ujumbe wa Injili kutoka kwa Allah (yeye ndo atakayetumwa kuikomboa dunia kutoka katika fitna za Dajjal).

Hebu jiulize kitu kimoja, Yesu alisulubiwa na wayahudi au warumi? (Jibu ni Warumi), Je warumi walikuwa wanawauzia wayahudi kuabudu Mungu wao katika ardhi yao (Jibu ni hapana). Warumi walitawala kwa maslahi yao ya kiuchumi na umiliki wa dola bila kuingilia masuala ya kiimani ya wayahudi, then kwanini wamuue ikiwa yeye alikuwa ni only religious figure? Jibu ni kwamba warumi walitafsiri Yesu kuwa ni tishio kwa dola yao kwa kuwa alijitangazia u-Messiah (mamlaka ya ukombozi kwa wayahudi). So kwa warumi kwao wao ilikuwa ni kosa la kihaini na sio kosa la kiimani ila baadhi miongoni mwa wayahudi walisupport na infact ndio waliotia fitna wakitaka auliwe kwasababu waliamini Yesu hakuwa Messiah wa kweli (wengine walisema ni mtoto wa zinaa n.k)

Mpaka sasa kundi hili la wayahudi wanamsubiria Messiah atakayekuja kurudisha utawala wa Daud na wanaamini wataitawala dunia pindi atakaporudi. Hili ndo litakolopelea wengi katika wao kumfuata Dajjal (False Messiah), then hapo ndipo atakaporudi tena Yesu kwa ajili ya kuikomboa dunia kutoka kwa Dajjal.

Allahu Aalam
 
Sasa una uhakika gn kama hao ni waislamu? Hayo madera hata ww siunavaa tu
Kila mtu anajua Madera,majura,vijora ni mavazi ya wanawake wa kiislamu waishio maeneo ya pwani.Ni mavazi ya heshima na stara yakivaliwa ipasavyo ila baadhi ya wanawake wa kiislamu huyatumia kwenye mambo ya kikahaba kama hivyo.

Binafsi naamini wapo waislamu wasafi na waislamu wachafu.Rohoni na mwilini na pia wapo wakristo wasafi na wa chafu pia.

Ninachompinga mtoa mada ni kuandika upuuzi eti waislamu wote ni safi mwilini na rohoni ndo mana nikamuonesha picha za uchafu wa baadhi ya waislamu.

Mim navaa suruali na vimini.Similiki dera hata moja mkuu
 
Huo ni uongo ulio dhahili.Dini ya mitume na manabii siku Yao kuu ya ibada ni jumamosi(SABATO).Siku hiyo hakuna kufanya kazi yoyote,ni ibada tu(Kutoka 20:8-11, ISAYA 58:13,EZEKIEL 20:20,WAEBRANIA 4:9, QURAN 4:154,16:124,2:65).Yesu pia alikuwa akifuata hiyo dini(LUKA 4:16).Na waliabudu kwa namna tatu hadi nne.Kusujudu,kuanguka kifudifudi,kusimama,kupiga magoti.Zote zilikuwa zinakubalika mbele za MUNGU.Mtu hakulazimika kutumia namna moja tu.Nabii Danieli yeye alikuwa akipendelea sana kupiga magoti(DANIEL 6:10).Nyie hamna SABATO.Sasa utasema ni imani moja hiyo?Nyie mna ijumaa,ambayo hamuifanyi kama sabato.Unafunga biashara unaenda kuswali.Unamaliza unageuka kuendelea na biashara kitu ambacho ni kinyume kabisa na dini ya manabii.Manabii hawajawahi kuhalalisha,wala kula najisi iwayo yote(walawi 11 yote).Leo uislamu umeifanya najisi(ngamia) kuwa mnyama mtukufu wakati MUNGU wa manabii amekataza kabisa hata kugusa mizoga yao.Najisi haitakiwi iliwe hata katika mazingira yoyote yale,ila uislamu unaruhusu katika mazingira ya njaa.Sasa unathubutu vipi kutamba hadharani eti kina Musa Walikuwa waislamu wakati sheria za dini ya Musa zote uislamu unazipinga na kuzikanyaga!!Ili ujue dini ya Musa ni lazima uzichunguze sheria alizopewa na Mungu zifuatwe na wote wenye kujunasibu kuifuata dini aliyonayo Musa.Muhammadi ametamka tu"Musa ni muislamu".Mty yeyote anaweza kutamka tu katika kitabu chake.Hata uhindu kupitia vitabu vyao wanaweza kutamka tu.Ili tuamini ni lazima tuchunguze sheria zilizopo pande zote,zinaendana?
Tatizo lako ni jazba uliyo nayo dhidi ya haki inakutia upofu usiweze kuiona nuru.

Ipo hivi, Uislam ulianza kabla ya Adam kuumbwa , kauli mbiu ni moja tu , Aabudiwe Mungu mmoja pasi na kushirikishwa na chochote. Baada ya Adam kuumbwa kauli mbiu ilikiwa ni ile ile aabudiwe Mungu mmoja pasi na kushirikishwa na chochote na kisha kumkiri mtume au nabii aliyetumwa ktk zama hizo.

Kila Mtume alikuwa na miongozo aliyopewa kutoka kwa Mungu kwa ajili ya watu wake, mfano kipindi chanAdam ilikuwa rukhsa kwa mapacha waliozaliwa tofauti katika tumbo la mama mmoja (Hawa ), kuoana. Yaani pacha ya kwanza (kaka na dada) inaioa pacha nyingine (kaka na dada).Leo hii ikitokea mmezaliwa hivyo ni haramu kuoana. Ila kipindi cha Adam ililuwa ni halali.

Mungu anatuambia katika Quran kuwa kila umma ulikuwa na sheria zake hivyo sheria alizopewa Mtume Muhammad haziwezi kuwa sawa na sheria alizopewa Musa au Isa(yesu). Kwa faida tu ya wasomaji ,Mungu anaeleza kuwa Vyakula vyote vilikuwa ni halali kwa wana wa Israel isipokuwa kile alichojiharamishia Nabii israel (Yaqub/Yakobo/Jacob) juu ya nafsi yake. Mwanzo wana wa israel waliruhusiwa kula kila kitu ila baadae Yakobo alijiharamishia baadhi ya vyakula na Mungu aliwaharamishia baadhi ya vyakula vizuri wana wa israel kutokana na ukaidi wao. Mfano hawakuruhusiwa kula baadhi ya nyama katika vichinjo vyao, mfano leo hii wayahudi hawali stake ya paja la ng'ombe ,mbuzi n.k kama haijaondolewa baadhi ya neva. Ukiangalia hakuna nyama nzuri kama paja ila walikatazwa wasile, vilevile wanyaman ambao kwato zao hazijagawanyika walikatazwa wasile ndio maana hawali ngamia ila wakati wa Nabii Isa (yesu) waliruhusiwa kula baadhi ya vyakula walivyoharamishiwa hapo kabla na umma huu wa Mtume Muhammad umekuja kuruhusiwa kula vyakula vizuri ambavyo waliharamishiwa wana wa israel hapo kabla.

Uislam kipindi cha Mtume Musa na uislam wa kipindi cha Mtume Muhammad ni ule ule wa kumuabudu Mungu mmoja pasi na kumshirikisha na chochote ila sheria na hukumu ndio zimebadilika kutokana na vipindi.

Mfano Mussa na watu wake walifaradhishiwa swala/sala mbili tu kwa siku, waswali asubuhi na jioni. Mtume Muhammad akawekewa sheria ya kuwa aswali Mara 5 kwa siku (Alfajiri,mchana,alasiri,jioni na usiku) ila msingi mkuu wa KUMUABUDU MUNGU MMOJA PASI NA KUMSHIRIKISHA NA CHOCHOTE upo palepale.
 
Siwez kukaa na kusema eti kuna mahali muislam amenizidi

Uislam ni dini ya vinyongo, ubaguzi, uhasama, vitisho na sheria kali ambazo hazina faida yoyote.
Mkuu punguza hasira na chuki utapata pressure bure.
 
Back
Top Bottom