- Thread starter
- #21
kweli kabisa umasikini, maradhi na ujinga ni adui wetu mkubwa lakini Rais Samia Suluhu ameweka mikakati ya kupambana na hawa maadui zetu wakubwa.Ni jambo zuri sana hili, kwani hata hayati, Mwl. Nyerere alisema tuna maadui 3 ambao ni maradhi, umasikini na ujinga, ila serikali kama kweli inataka kufanikisha hili la elimu basi ihakikishe kunakuwa na rasilimali watu wa kutosha, vifaa bora vya ujifunzaji, mazingira bora n.k. Nasema hivi kwa kuwa juzi hapa kuna mkuu wa wilaya alijitokeza na kudai katika wilaya yake kuna uhaba mkubwa wa wstumishi(Walimu) katika shule za msingi, jambo ambalo linasababisha wanafunzi wamalize shule bila kujua kusoma na kuandika.
Suala la elimu amejenga madarasa mpaka vijijini, nyumba za walimu, ameajiri walimu wa kutosha mwaka huu, lakini pia kuna ajira za walimu zaidi ya elfu 42 zimepitishwa kwaiyo Mama ameiboresha elimu kwa kiasi kikubwa na bado anaendelea kuboresha.
Suala la maradhi mama amekuja na mpango wa bima ya afya kwa wote itakayosaidia kupunguza gharama za matibabu.
Vile vile suala la Umasikini Rais Samia Suluhu amefanikisha kuwawezesha vijana wengi nchini wasio na ajira kupata mikopo yenye masharti nafuu na kupitia miradi inayotekelezwa nchini inatoa fursa za ajira kwa wazawa na sio watu kutoka nje
Rais Samia Suluhu amefanya mapinduzi kila idara haachi gepu