Maeneo nane yatakayofadhiliwa na Samia Scholarship

kweli kabisa umasikini, maradhi na ujinga ni adui wetu mkubwa lakini Rais Samia Suluhu ameweka mikakati ya kupambana na hawa maadui zetu wakubwa.

Suala la elimu amejenga madarasa mpaka vijijini, nyumba za walimu, ameajiri walimu wa kutosha mwaka huu, lakini pia kuna ajira za walimu zaidi ya elfu 42 zimepitishwa kwaiyo Mama ameiboresha elimu kwa kiasi kikubwa na bado anaendelea kuboresha.

Suala la maradhi mama amekuja na mpango wa bima ya afya kwa wote itakayosaidia kupunguza gharama za matibabu.

Vile vile suala la Umasikini Rais Samia Suluhu amefanikisha kuwawezesha vijana wengi nchini wasio na ajira kupata mikopo yenye masharti nafuu na kupitia miradi inayotekelezwa nchini inatoa fursa za ajira kwa wazawa na sio watu kutoka nje

Rais Samia Suluhu amefanya mapinduzi kila idara haachi gepu
 
Vigezo ni A,A,A na kila mwisho wa mwaka uwe na GPA 3.8 kudrop tu unapigwa chini. Utumwa huo.
Ndio ivo mzee sasa unataka ufike chuo urelax kusoma mwanzo mwisho safi sana napongeza sana hizi juhudi za Rais Samia Suluhu
 
Inakuaje wanafunz tuwatenge kisa ufaulu,
Huu ni upuuzi! Wanafunzi wote wanahitaji pesa ya kujikimu pamoja na ada kwa ajili ya masomo yao ya elimu ya juu

Sasa unampa scholarship mwanafunzi wa shamsiye boys anaelipa ada milioni 8 kwa mwaka then unamwach wa kata akahangaike chuoni kisa ufaulu mdogo! Still kafaulu kupitia shule yake kata.

Hivi ni kweli jamani!!! ni heri hiyo pesa ingeongezewa kwenye bajeti ya bodi ya mikopo wanafunzi wapate kunufaika wote kwani kigezo cha ufaulu hakina tija.
 
Unajua Hawa wanasiasa ambao hawakutegemea kuwa walipo ila wakajikuta pale wanalipeleka pabaya taifa,

Huu Kama sio ubaguzi na matumizi mabaya ya pesa za watu kitu GANI, nchi hii elim kwanza ulisha kuwa ya kibaguzi wakwetu tusiokua na uwezo wopo shule za kata,wa kwao wapo huko mwenye shule zao na wanakua na ufaulu mkubwa

Tunaviongozi wanaofikilia maisha ya kisiasa kwao ila sio nchi

Iyo pesa kwa nini isiongezwe bodi ya mikopo?

Wanasiasa wanazidi tuaribia nchi na hawafanyi kwa kutojua wanajua walifanyalo,lakini narudia tena twende tu ,hawezi kuwa kiongozi wa nchi tena
Ufaulu ndio sababu kubwa ya kuchaguliwa kama kweli mdogo wako anaufauluhu huo unaoitajika na hajachaguliwa hata mimi ntakusapot kulalamika
 
Inafikirisha sana..
 
Kigezo kikubwa ni ufaulu mzuri wa masomo ya sayansi
Kwa kigezo hiki watakao nufaika zaidi wenda wakawa sio watoto wa masikini maana mazingira ya shule zetu za serikali nyingi (ambazo masikini wengi tunasomesha watoto huko) hazina mazingira wezeshi ya kuwafanya watoto wengi kupata ufaulu huo.

Sijui Ata nasema nini
 
Ni upuuzi tu kama upuuzi mwingine , hiyo kazi si ingefanya wizara ya Elimu kwa kweli inahitaji wataalamu wa namna hiyo . Mbona Waziri wa Wizara husika yuko vizuri sana . Huku ni kutafuta Kiki tu
 
Kabisa
 
Rais Samia Suluhu ameweka mazingira wezeshi kufaulisha mfano mzuri ni matokeo ya mwaka huu advance shule za serika ziliongozo kwaiyo mama anawapa chachu ya kuongeza bidii zaidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…