Maeneo ya biashara Mbezi Louis stendi mpya walengwa ni kina nani?

Maeneo ya biashara Mbezi Louis stendi mpya walengwa ni kina nani?

One square meter Ni 399000 hivi mlimani city wamefika Bei hiyo.
It should be 3,990 kwa mita mraba otherwise .......
 
Na hapo ukute wenyewe ndio wenye kumiliki hivyo vyumba. Na hapo eti wanamjali mwananchi masikini. Hivi kuna watu wamekubali kuingia mkenge wa kupanga hivyo vyumba? Na kwa hali ya kibiashara ilivyo ngumu na mbaya kwa sasa nchini sidhani kama kuna mtu ataingia mkenge. Hii ilitokeaga soko jipya la mwanjelwa mbeya. Wakapanga bei kama hizo. Lakini unawafahamu mbeya?. Soko mpaka leo lipo lipo tu pamoja na zuri na eneo la kibiashara. Pamoja na kuendelea kushusha bei,bado hakujapendeza
 
Tangu lini serikali ikawa na bei kubwa namna hii, acheni wanyonge nao wafaidike angalau kwa bei ya buku 5 nao wapangishe kwa watu wengine. Ukifuatilia kwa karibu utakuta wameshajimilikisha wenyewe na ndugu zao..
 
Hapo n kutembeza biashara zako tuu ndan ya stand
 
Kuna akili huwa zinaitwa "Akili za Kujiongeza".

Mwaka 2009 - 2012 viwanja Mbezi Luis (Mbezi shamba mlivyokuwa mkiita) vilikuwa havifiki hata million 3 kwa eneo ilipojengwa stand hadi bar ya Tononeka, kupandisha mnarani ukishuka darajani (njia ya kwenda Makabe) ndio hata 1M ulikuwa unapata kiwanja kizuri tu.

Mkahangaika na Kigamboni pamoja na Chanika, leo hii mnapangishiwa vyumba vya biashara kwa bei hiyo mnalalama NI UJINGA tena mkae kwa kutulia kabisa.
Njoo kwenye frem zetu hapa Arapha dispensary tukunyooshe pia hutaki ACHA
Ni game of chance tu hiyo usitambe sana ! Kuna wenzetu wanalia stend inapohama ubungo kwa uwekezaji walioufanya pale , analgalia yale mahoteli makubwa pale kando na ubungo terminal, wakati stendi zinahamia pale kutoka kisutu na mnazi mmoja walikuwa katika position Kama yako.
 
Back
Top Bottom