Maeneo yenye maisha tofauti Dar es Salaam

Maeneo yenye maisha tofauti Dar es Salaam

Dsm watu wengi wana maisha duni sana sana hawana kazi ni ubabaishaji tuu,hawana stock za vyakula hununua wanapotaka kula unga nusu,mafuta ya kula robo,fungu la dagaaa!!! Yani shida tupu !!! Ukikuta wana kunywa hizo supu zao za buku(1000) utacheka
Lakini wanajiona wajanjaaa!!!
Si wanajua kiswahili!!
 
Umasikini ni kitu kibaya sana mkuu. Umasikini ndio chanzo cha uovu mwingi sana hapa duniani.
Hapana mkuu ebu jaribu kufikiria tena, unadhani uovu uliopo sasa ni sawa na wa miaka1690 je watu wa miaka hiyo walikuwa matajiri au maskini?
 
Dsm watu wengi wana maisha duni sana sana hawana kazi ni ubabaishaji tuu,hawana stock za vyakula hununua wanapotaka kula unga nusu,mafuta ya kula robo,fungu la dagaaa!!! Yani shida tupu !!! Ukikuta wana kunywa hizo supu zao za buku(1000) utacheka
Lakini wanajiona wajanjaaa!!!
Mkuu acha porojo, twende kwenye takwimu za hali nzuri ya maisha tuone ni Mkoa gani hapa tz unaizidi dsm
 
Hii ndio style ya maisha tuliyochagua. Tunanunua cha kula leo,kesho tutajua kesho.
Achana naye huyu mkuu! Anataka mjenge vihenge mhifadhi mahindi na maharage kwa magunia, mm napenda staili ya mjini dar, you buy when you want to consume, utanunuaje kg 50 za unga hadi uozee ndani? Mji wenyewe kila kitu toka mikoa yote kinapatikana muda wote, hakuna cha msimu wala nn. Ukitaka ndizi ya bukoba, moshi, turiani nk unapata! Safi sana
 
Una mawazo kama yangu, Mimi ningevunja kuanzia ubungo hadi kimara nyuma zote za barabarani na kujenga maghorofa yanayofanana. Hill eneo ndio mdomo wa Tanzania
Serikali yetu ingekuwa na maono ya mbali wangeanza mkakati wa muda mrefu labda miaka 20+ ya kuyageuza maeoneo ya manzese na magomeni yawe kariakoo nyingine. Wakazi wa hayo maeneo wauze na watauftiwe maeneo mengine yaliyoboreshwa zaidi wakajenge huko. Tatizo la serikali yetu inaogopa kufanya maamuza magumu ya maendeleo kwa kuhofia kukosa kura jambo ambalo naona ni kutoona mbali na ndio maana miji yetu imejaa uswazi.
 
Mkuu inategemea sana utakavyo ishi, mimi nimezaliwa na nimekulia sinza ushuani kweli kila nyumba ukuta geti. Lkn niliishi Chocho moja tandale kati m/nyamala huko huko nilikua na ndinga narudi muda wowote naotaka sikuwai kukabwa. You know what? Sbb najua kuishi na aina zoooote za watu. Day one nilijichanganya nao sana tu sbb naelewa maisha, kweli uswahilini wamekwama maisha lkn hawapendi kudharauliwa kama mimi tu ukishare nao mambo yao unakua wao na wanakua walinzi wazuri sana kwako na familia yako hii naongea from experience. Kuna siku mtoto wangu alikua anazurura mitaani masela kitaa wakamdaka safari moja kwa moja home kwangu. Kachala akaniambia broo, dah dogo alikua anazurura kitaa tukamuona tukasema huyu si mwana wa kaka etu? Wote tukasema "mwenyewe" Sasa huku anatafuta nn? Ah nikamdaka nimemleta home!" Tukaona nini braza huyu mtoto ataharibikiwa ngoja tumuokoe!
Hayo ni maneno niliyoyasikia mwenyewe kutoka kwa wahuni wa kitaa. Nilifurahi sana but at the same time niliumia sana. Nilifurahi sbb kumbe jamii nayoishi nayo inajali maisha yangu na familia yangu lkn niliumia sana sbb watoto wao na familia zao hawazijali kabisa but why me? sbb nipo nao kwenye shida zao so wananiona mimi ni mwenzao ila ukumesap nao watakuzingua kinoma. Mimi kwa sasa naweza ishi sehemu yoyote na kula bata kadri navyotaka bila wasi!
Hata ukimpa mtu buku anashukuru sana na utaitwa mshua. Usiwadharau nao hawatakudharau
 
Hii mada imenifanya niifikirie nchi ya India, ktk mji wa Mumbai ndio kuna nyumba ya mtu binafsi ya gharama zaidi duniani kulingana na jarida la Forbes yenye thamani zaidi ya dola za ki-Marekani bilioni 2 yaani zaidi ya trilioni 4 za ki-Tanzania na hapo hapo Mumbai ndipo mahala penye makazi duni (slums) zaidi duniani maeneo ya Dharavi.

Hiyo nyumba yenye thamani kubwa zaidi duniani inaitwa Atilia mmiliki wake anaitwa Mukesh Ambani, anaishi na familia yake hapo ila kilomita chache kabisa kutoka hayo makazi yake kuna makazi duni sana ya watu kuna mpaka njia za watu juu ya mapaa ya nyumba.

Pia, Hong Kong watu wanaishi ktk viota na majeneza (cage & coffin homes) nyumba ni gharama sana. Lakini kituko zaidi hapo hapo Hong Kong ndipo mahala penye matajiri wengi sana duniani kuliko mahala popote wenye ukwasi zaidi ya dola za ki-Marekani bilioni 1 kwa mujibu wa tafiti za jarida la Forbes.

Duniani kote kupo hivyo hivyo hapakosi utofauti wa kimaisha ndani ya miji illiyo karibu sana sio London wala New York wala Beijing tena utahamaki sana ukienda miji hiyo ukikutana na watu wanaoishi Corridor size apartments (very tiny places, below 300 square feet).
Hiyo ya India inasikitisha sana
 
Mikocheni b yenyewe kuna sehemu moja katikati
Pako uswazi sana watu wanaishi hivyo
Hata hivyo bado mikocheni pamebanana sana

Ova
Kuna ile Mikocheni ya nyuma ya TMJ mpaka kule kama MRC [emoji119][emoji119][emoji119][emoji119]. Ile sehemu ni uswahilini sijapataga kuona.
 
Mkuu acha porojo, twende kwenye takwimu za hali nzuri ya maisha tuone ni Mkoa gani hapa tz unaizidi dsm
Achana nae huyo analeta stories za vijiweni.
Waziri Kalemani alipotoa takwimu za mahitaji ya umeme kwa mikoa
1. DSM megawatts 700
2. Mwanza megawatts 165
3. Mbeya megawatts 75
Mikoa mingine inafuatia
Hiyo tu inatosha kusema DSM huwezi ilinganisha na mkoa wowote Tz.
 
Yafuatayo in baadhi ya maeneo yaliyokaribu sana kijeografia ila yana hadhi tofauti kimaisha.

1. Sinza na Tandale
Mitaa hii ipo karibu sana ila hali ya maisha ya watu wake in tofauti kabisa. Tandale watu wengi wana maisha ya chini na uswahili pia.

2. Kawe na mikocheni
Kawe kuna uswazi ila jirani zao mikocheni kwa warioba wanakula upepo

3. Masaki na msasani
Hapa tajiri anakutana na maskini moja kwa moja. Ukimaliza tu masaki na kuanza msasani unaanza kuona ladha ya umasikini. Msasani kuna slum.

4. Mtongani na bahari beach/ununio.
Watu wa mtongani wana maisha ya chini sana shughuli yao ni uvuvi, kokoto na bodaboda ila jirani zao bahari beach ni maghorofa na mitaa iliyopangika vizuri na watu maarufu wako huko.

Hayo ni maeneo ambayo wenye nacho na pangu pakavu wanaishi pamoja kwa ukaribu
Kariakoo na Temeke
 
Hapo ndo unaanza kukutana na kawe, nyumba imezama chini ina ukuta mfupi kama banda la kuku
Hahahaaa.. sijakutana na za hivyo ila huko ndani ndani uswahilini nako balaa.
 
Achana naye huyu mkuu! Anataka mjenge vihenge mhifadhi mahindi na maharage kwa magunia, mm napenda staili ya mjini dar, you buy when you want to consume, utanunuaje kg 50 za unga hadi uozee ndani? Mji wenyewe kila kitu toka mikoa yote kinapatikana muda wote, hakuna cha msimu wala nn. Ukitaka ndizi ya bukoba, moshi, turiani nk unapata! Safi sana
DSM tunanunua kila siku hatujengi vichanja vya kuhifadhia mahindi mwaka mzima.
 
Back
Top Bottom