Maeneo yenye maisha tofauti Dar es Salaam

Maeneo yenye maisha tofauti Dar es Salaam

Hizi ni nyumba za zamani enzi za Uhuru. Zilikuwa za nhc wakauziwa wakazi. Zimetitia kadiri muda unavyokwenda. Wengi sasa hivi wanafumua paa na kuongeza kozi tatu juu ziwe Sawa.
Hapo ndo unaanza kukutana na kawe, nyumba imezama chini ina ukuta mfupi kama banda la kuku
 
Hizi ni nyumba za zamani enzi za Uhuru. Zilikuwa za nhc wakauziwa wakazi. Zimetitia kadiri muda unavyokwenda. Wengi sasa hivi wanafumua paa na kuongeza kozi tatu juu ziwe Sawa.
Kule mikocheni uswahilini nyuma ya shoppers hakuna nyumba za nhc kule.

Nyumba za nhc zilizouzwa zipo migombani street na maeneo yanayoendana na yale ila kule uswekeni hakuna nhc pako ovyo balaaa.

Kule uswazi hata wanafunzi wa kairuki wanapaogopa
 
Kule mikocheni uswahilini nyuma ya shoppers hakuna nyumba za nhc kule.

Nyumba za nhc zilizouzwa zipo migombani street na maeneo yanayoendana na yale ila kule uswekeni hakuna nhc pako ovyo balaaa.

Kule uswazi hata wanafunzi wa kairuki wanapaogopa
Nyumba ninazozungumzia zipo maeneo mengi kama kinondoni,magomeni,ilala,mwananyamala ukiziangalia zimekuwa fupi sana.
 
maeneo yote karibu yana kila hali.kwa uzoefu wang sehem pekee naona ni oystebay na upanga ndikko washua wamejazana
 
Yafuatayo in baadhi ya maeneo yaliyokaribu sana kijeografia ila yana hadhi tofauti kimaisha.

1. Sinza na Tandale
Mitaa hii ipo karibu sana ila hali ya maisha ya watu wake in tofauti kabisa. Tandale watu wengi wana maisha ya chini na uswahili pia.

2. Kawe na mikocheni
Kawe kuna uswazi ila jirani zao mikocheni kwa warioba wanakula upepo

3. Masaki na msasani
Hapa tajiri anakutana na maskini moja kwa moja. Ukimaliza tu masaki na kuanza msasani unaanza kuona ladha ya umasikini. Msasani kuna slum.

4. Mtongani na bahari beach/ununio.
Watu wa mtongani wana maisha ya chini sana shughuli yao ni uvuvi, kokoto na bodaboda ila jirani zao bahari beach ni maghorofa na mitaa iliyopangika vizuri na watu maarufu wako huko.

Hayo ni maeneo ambayo wenye nacho na pangu pakavu wanaishi pamoja kwa ukaribu
Kwani ulikuwa hujui kwenye msafara wa mamba kenge hawakosekani?[emoji23][emoji23]
 
Serikali yetu ingekuwa na maono ya mbali wangeanza mkakati wa muda mrefu labda miaka 20+ ya kuyageuza maeoneo ya manzese na magomeni yawe kariakoo nyingine. Wakazi wa hayo maeneo wauze na watauftiwe maeneo mengine yaliyoboreshwa zaidi wakajenge huko. Tatizo la serikali yetu inaogopa kufanya maamuza magumu ya maendeleo kwa kuhofia kukosa kura jambo ambalo naona ni kutoona mbali na ndio maana miji yetu imejaa uswazi.
yap maeneo kama manzese mwananyama la buguruni.kwa mfano kuwahahamisha watu wa Gongo la Mboto si mchezo
 
Hii mada imenifanya niifikirie nchi ya India, ktk mji wa Mumbai ndio kuna nyumba ya mtu binafsi ya gharama zaidi duniani kulingana na jarida la Forbes yenye thamani zaidi ya dola za ki-Marekani bilioni 2 yaani zaidi ya trilioni 4 za ki-Tanzania na hapo hapo Mumbai ndipo mahala penye makazi duni (slums) zaidi duniani maeneo ya Dharavi.

Hiyo nyumba yenye thamani kubwa zaidi duniani inaitwa Atilia mmiliki wake anaitwa Mukesh Ambani, anaishi na familia yake hapo ila kilomita chache kabisa kutoka hayo makazi yake kuna makazi duni sana ya watu kuna mpaka njia za watu juu ya mapaa ya nyumba.

Pia, Hong Kong watu wanaishi ktk viota na majeneza (cage & coffin homes) nyumba ni gharama sana. Lakini kituko zaidi hapo hapo Hong Kong ndipo mahala penye matajiri wengi sana duniani kuliko mahala popote wenye ukwasi zaidi ya dola za ki-Marekani bilioni 1 kwa mujibu wa tafiti za jarida la Forbes.

Duniani kote kupo hivyo hivyo hapakosi utofauti wa kimaisha ndani ya miji illiyo karibu sana sio London wala New York wala Beijing tena utahamaki sana ukienda miji hiyo ukikutana na watu wanaoishi Corridor size apartments (very tiny places, below 300 square feet).
india nasikia masikini sana huko
 
Hii picha ni project ya msomali mmoja ununio imefikia hatua nzuri serikali ikamzuia kumalizia ujenzi
 

Attachments

  • FB_IMG_16018761259370037.jpg
    FB_IMG_16018761259370037.jpg
    41.6 KB · Views: 17
Mkuu we ni mgeni dar? Hujui kuwa nyuma ya uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere ni Buza!
 
Dar ni Jiji pekee lenye baraka,uvumilivu,Amani, fursa na mizunguko ya masilahi kwa kila mwenye ndiyo awezae kufika Dar-es-Salaam!!
Jiji lenye msamiati hali SALAAM !!
(( ukiingia kwa baya utapata ubaya))
 
Umenichekesha sana aisee! Ni kama Raia wa Kilimanjaro wote wawapo nje ya Kilimanjaro unapowauliza kwenu ni wap?
Wanajibu: Moshi.
Awe Mpare wa Chome, ndungu, Vudee n.k atasema Moshi.....huwa nacheka sana.
Nikagundua kuwa Mwanadamu anapenda vitu vizuri.
Ndungu....
Umenikumbusha miaka kadhaa nyuma mkuu. Huko mahali ni pagum balaa.
 
Back
Top Bottom