*UKIPATA NAFASI POPOTE PALE .... ONGEA HAYA KUHUSU RAIS WAKO JPM*
( _kuwa Mzalendo_)
*@katata...[emoji455]*
1. *JPM amerejesha nidhamu ya fedha habari za kutumia fedha kuleta ubabe hakuna, maneno nitakupiga nikulipe imebaki historia.*
2. *JPM amerejesha nidhamu kwenye ofisi za umma, tabia za watumishi wa umma kujimilikisha ofisi za umma imebaki historia, kauli toka ofisini kwangu, nipo ofisini tumezisahau.*
3. *JPM amekomesha tabia ya wanaCCM kadhaa kutumia chama kama mwamvuli wa kukopa kodi, kupiga madili na kuleta ubabe mtaani.*
4. *JPM amekomesha mtandao wa kupeana vyeo serikali, tabia ya kutumia watu na pesa kupata nafasi serikali imepotea rasmi*.
5. *JPM amefanya vizuri kwenye sekta ya miundombinu na usafirishaji , amethubutu kufanya mambo mazito kwenye reli, barabara, anga, nk*
6. *Kupitia JPM sasa uongozi ni kutumikia watu siyo kuvuma pesa kama ilivyokuwa sasa wabunge, madiwani, mawaziri, nk wanaishi kama viongozi siyo wafanyabiashara , kufikia 2020 wanasiasa wafanyabiashara watajiweka pembeni.*
7. *Kupitia JPM viongozi wamekuwa wasikivu kwa wananch, tabia ya viongozi hasa wanasiasa kujiona miungu imebaki historia.*
8. *JPM amevunja mwiko wa tabia ya kudhani watu fulani wa familia ndiyo special kuteuliwa ktk nafasi za kiserikali, kupitia JPM kupata uteuzi ni uwezo siyo historia ya familia*.
9. *JPM amethubutu kutazama utapeli tunaofanyiwa kwenye sekta ya madini, angalau ameunda tume kuchunguza usafirishaji wa Udongo kwenda ughaibuni hili siyo japo la mzaha.*
10. *JPM amekomesha ujangili sasa matukio ya ujangili yamepotea kabla Tanzania ilikuwa inakwenda kupoteza tembo na Wanyama wengine muhimu sasa Wanyama wetu wapo salama.*
11. *JPM amekomesha matumizi ya hovyo ya kodi zetu , semina za kulipana fedha hovyo hakuna, safari za kutengeneza kupiga pesa hakuna, manunuzi ya kisanii hakuna , kipindi hiki viongozi na watendaji wa serikali wanaheshimu kodi zetu.*
12. *JPM amethubutu kupambana na dawa za kulevya kwa vitendo hili siyo jambo dogo ukizingatia nguvu ya wauza dawa za kulevya.*
13. *JPM ameendeleza vema vita dhidi ya rushwa kuanzia kwenye chama (CCM) mpaka Taasisi za serikali , siyo jambo dogo kukomesha rushwa kwenye siasa zetu za Afrika yeye ameonesha njia kwenye uchaguzi wa wabunge wa EAL.*
14. *JPM amekomesha mtandao wa ufisadi BANDARINI enzi hizo bandari yetu ilikuwa chimbo la kujipatia utajiri wa kifisadi sasa BANDARINI amesafisha.*
15. *JPM amekomesha tabia ya viongozi kupeana tenda za serikali kihuni na kifisadi, kandarasi sasa zinatolewa kwa kufuata utaratibu kiasi cha kupunguza ufisadi kwenye halmashauri zetu.*
16. *JPM amerejesha uadilifu kwenye sekta ya afya, pamoja na changamoto za uhaba wa dawa, wataalam wa afya na vifaa angalau madaktari na wauguzi wana kauli nzuri zenye faraja kwa wagonjwa hata rushwa sekta ya afya siyo kama enzi zile.*
17. *JPM ameleta utaratibu mzuri wa viongozi kutoka ofisini kwenda mtaani kutazama matatizo ya wananch kuliko Kutegeana kusoma ripoti tu.*
18. *JPM amerejesha thamani ya elimu kwa kuteua wasomi ktk nafasi mbali mbali kuliko awali watu waliteuliwa kwa mazoea, sasa maprofesa, madaktari na wasomi kwa ujumla ndiyo viongozi wa wizara zetu*
19. *JPM amekomesha mtandao wa makundi kwenye chama na serikali sasa mtandao wa kupeana ukurugenzi wa halmashauri, UDC, URC, ukatibu wa chama, ukurugenzi wa mashirika ya umma umepotezwa hili siyo jambo dogo.*
*20. JPM amekomesha matapeli wenye mwamvuli wa uwekezaji waliojimilikisha ardhi kubwa nchini huku watanzania wakikosa maeneo ya kulima.*
KATATA.....
_Tanzania ni yetu_
_Magufulichaguo letu_