Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Umejitafutia kuvuruga siku juu yako!
Unaweza kuta basi nawewe umepata kauteuzi Fulani basi ndio kanakutia upofu!
 
Wakuu kutokana na utendaji mzuri wa Rais JPM Magufuli na kuwa kiongozi wa kupigiwa mfano Africa na Duniani na ili Taifa letu lifike pale ambapo Nchi nyingi za Kiafrika kimaendeleo zimefikia.! Tukijielekeza katika Mfano wa Rwanda na Uganda.Na sudan kaskazini.
Napendekeza Rais wa Nchi Yetu Ndugu John Joseph Pombe Magufuli aongoze Nchi yetu mpaka 2050.
[HASHTAG]#Magufuli[/HASHTAG] mpaka 2050# mimi kura yangu nimeshapiga sijui wewe.

Labda uenyekiti wa CCM.
Halafu kama kuna mtu alishakuja na hoja hii hapa jamvini🙁
 
*UKIPATA NAFASI POPOTE PALE .... ONGEA HAYA KUHUSU RAIS WAKO JPM*
( _kuwa Mzalendo_)

*@katata...[emoji455]*


1. *JPM amerejesha nidhamu ya fedha habari za kutumia fedha kuleta ubabe hakuna, maneno nitakupiga nikulipe imebaki historia.*


2. *JPM amerejesha nidhamu kwenye ofisi za umma, tabia za watumishi wa umma kujimilikisha ofisi za umma imebaki historia, kauli toka ofisini kwangu, nipo ofisini tumezisahau.*


3. *JPM amekomesha tabia ya wanaCCM kadhaa kutumia chama kama mwamvuli wa kukopa kodi, kupiga madili na kuleta ubabe mtaani.*


4. *JPM amekomesha mtandao wa kupeana vyeo serikali, tabia ya kutumia watu na pesa kupata nafasi serikali imepotea rasmi*.


5. *JPM amefanya vizuri kwenye sekta ya miundombinu na usafirishaji , amethubutu kufanya mambo mazito kwenye reli, barabara, anga, nk*


6. *Kupitia JPM sasa uongozi ni kutumikia watu siyo kuvuma pesa kama ilivyokuwa sasa wabunge, madiwani, mawaziri, nk wanaishi kama viongozi siyo wafanyabiashara , kufikia 2020 wanasiasa wafanyabiashara watajiweka pembeni.*


7. *Kupitia JPM viongozi wamekuwa wasikivu kwa wananch, tabia ya viongozi hasa wanasiasa kujiona miungu imebaki historia.*


8. *JPM amevunja mwiko wa tabia ya kudhani watu fulani wa familia ndiyo special kuteuliwa ktk nafasi za kiserikali, kupitia JPM kupata uteuzi ni uwezo siyo historia ya familia*.


9. *JPM amethubutu kutazama utapeli tunaofanyiwa kwenye sekta ya madini, angalau ameunda tume kuchunguza usafirishaji wa Udongo kwenda ughaibuni hili siyo japo la mzaha.*


10. *JPM amekomesha ujangili sasa matukio ya ujangili yamepotea kabla Tanzania ilikuwa inakwenda kupoteza tembo na Wanyama wengine muhimu sasa Wanyama wetu wapo salama.*

11. *JPM amekomesha matumizi ya hovyo ya kodi zetu , semina za kulipana fedha hovyo hakuna, safari za kutengeneza kupiga pesa hakuna, manunuzi ya kisanii hakuna , kipindi hiki viongozi na watendaji wa serikali wanaheshimu kodi zetu.*


12. *JPM amethubutu kupambana na dawa za kulevya kwa vitendo hili siyo jambo dogo ukizingatia nguvu ya wauza dawa za kulevya.*


13. *JPM ameendeleza vema vita dhidi ya rushwa kuanzia kwenye chama (CCM) mpaka Taasisi za serikali , siyo jambo dogo kukomesha rushwa kwenye siasa zetu za Afrika yeye ameonesha njia kwenye uchaguzi wa wabunge wa EAL.*


14. *JPM amekomesha mtandao wa ufisadi BANDARINI enzi hizo bandari yetu ilikuwa chimbo la kujipatia utajiri wa kifisadi sasa BANDARINI amesafisha.*


15. *JPM amekomesha tabia ya viongozi kupeana tenda za serikali kihuni na kifisadi, kandarasi sasa zinatolewa kwa kufuata utaratibu kiasi cha kupunguza ufisadi kwenye halmashauri zetu.*


16. *JPM amerejesha uadilifu kwenye sekta ya afya, pamoja na changamoto za uhaba wa dawa, wataalam wa afya na vifaa angalau madaktari na wauguzi wana kauli nzuri zenye faraja kwa wagonjwa hata rushwa sekta ya afya siyo kama enzi zile.*


17. *JPM ameleta utaratibu mzuri wa viongozi kutoka ofisini kwenda mtaani kutazama matatizo ya wananch kuliko Kutegeana kusoma ripoti tu.*


18. *JPM amerejesha thamani ya elimu kwa kuteua wasomi ktk nafasi mbali mbali kuliko awali watu waliteuliwa kwa mazoea, sasa maprofesa, madaktari na wasomi kwa ujumla ndiyo viongozi wa wizara zetu*


19. *JPM amekomesha mtandao wa makundi kwenye chama na serikali sasa mtandao wa kupeana ukurugenzi wa halmashauri, UDC, URC, ukatibu wa chama, ukurugenzi wa mashirika ya umma umepotezwa hili siyo jambo dogo.*


*20. JPM amekomesha matapeli wenye mwamvuli wa uwekezaji waliojimilikisha ardhi kubwa nchini huku watanzania wakikosa maeneo ya kulima.*


KATATA.....


_Tanzania ni yetu_
_Magufulichaguo letu_
 
Watz walichagua ili afanye mazuri hvyo ni wajibu wake kifanya hayo na sio lazma asifiwe coz aliwekwa kwa hiyo...
Mwanaume alietimia hawez kujisifu kwa kuitunza familia yake kwan huo ni wajibu wake...
Na ile ya kula pesa za rambi rambi mbna umeliacha mkuu na pumba nyingne ambazo ni nying zaid ya hzo ulizotuandikia hapo...
Angalia pande zote za shiling!!!
.
Lakin kwa hayo mazuri [emoji106] [emoji106] [emoji106] [emoji106]
 
Bado sana kuanza kuhesabu faida! Kama ni safari ya Mwanza ndio kwanza yuko Chalinze. Kwa taarifa yako yote uliyoyataja kama mafanikio ni watu wamepoz kusoma ramani ya Magu, wakishamsoma utashangaa. Ona polisi barabarani wanavyotafuna. Hiyo #8 sio kweli, rejea uteuzi wa mke wa mkwere na wa tingatinga. Ninaweza sema alichofanya endelevu ni kukomesha viroba.
 
Sasa ninamuelewa Tundu Lisu anaposema tumepata Rais Wa ajabu...Yaani ndani ya kipindi kifupi amenunua ndege mbili....anajenga flying over mbili Mandela road....ameahakamilisha ujenzi wa hosteli pale Udsm ...Elimu bure inaendelea vema ....uwajibikaji upo juu...wauza Madawa ya kulevya taabani.....Ujenzi wa Reli ya kimataifa umeanza....sasa kwanini unabisha ukiambiwa Magufuli ni Rais wa ajabu?
 
Haswaa hata mafisadi sasa wanahaha nchi nzima.
 
Naunga mkono hoja pia....
...lakini, yakija masuala ya akina Lema, Lijualikali, Mathew and the like ndio nakuwa na mashaka. Pia jinsi alivyo liaddress suala la ibalozi wa Israel linaweza kuwachukiza wengine. Angetumia approach ndogo ya kuwakuta walevi baa na badala ya kuwatukana kwa ulevi unakaa nao lakini unaagiza soda for the sake of unity!
 
Kuna mpigaji zaidi ya Magufuli? Unakumbuka kivuko cha Bagamoyo na ukwapuzi wa pesa za wahanga na nyumba za Serikali!? Mpigaji mwingine huyu. Kweli akili iliyodumazwa kwa ujinga haina dawa.


Wenywenye akili wanajua Magufuli anafanyanini wapigaji ndio wanalia kila siku wazalendo wa nchi hii tunatamani Magufuli aendelee miaka 20 ijayo tubadili katiba
 
"Permanence, perseverance and persistence in spite of all obstacles, discouragements and impossibilities: It is this, that in all things distinguishes the strong soul from the weak"

Thomas Carlyle
 
Ujenzi wa Shule Bukoba
07cff0e96d62aa576c1a203a638988c7.jpg
 
Back
Top Bottom