Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

wenzako hamu
ya misri ilianza dakika chache baada ya kukutana na kikwazo cha bahari ya shamu wakasahau kbs kila tabu walizopata misri.
majamaa yakasahau mateso ya misri yakaanza kukumbuka mapapai,vitunguu, matikiti na nyanya chungu za misri.
 
Nani kakuakikishia kwamba safari hiyo bado miaka saba, huyu hata hii 3 iliyobaki hastahili kuendelea,
 
Nani kakuakikishia kwamba safari hiyo bado miaka saba, huyu hata hii 3 iliyobaki hastahili kuendelea,
Miaka iliyobaki Katika safari hii ni 7 hiyo mitatu ni yako na safari yako sijui ya kwenda wapi
 
Ni wazi kabisa Tanzania hii iliyobarikiwa utajiri mkubwa inakwenda kustawi kwenye huu ukanda nchi za majirani kaeni chonjo.Rais Magufuli amecheza game ya akili kaua ndege wa tatu kwa jiwe moja.

Nani hajui kama kwenye mfumo wa sheria palikuwa na utata! Rushwa na udhaifu Rais Magufuli ananyoosha kila sekta.

Wenye upeo wa juu na hekima wanaona nani asiyejua mafisadi wanaiba kwa kutumia wanasheria.Mimi nakiri kabisa hakuna rais bora kuwahi kutokea Tanzania mwenye maono,dira na dhamira ya kutubeba kila sehemu kama Magufuli.

Kila mtu na mtazamo wake ila sisi tunaomwamini Magufulu tutabaki hivyo.Mungu wetu mfalme wa tawala zote alipanga Tanzania ya 2015-2025 iwe hapa kazi tu.

Safi sana Magufuli wawekezaji watakuja wenyewe hakuna haja ya kutumia pesa ya nchi kwenda kuwatafuta.tanzania mpya tumaini kuu.

Ndio hivo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tunapoteza pesa na muda kujuwa nani analiyumbisha taifa letu take from me Rushwa ilioota mizizi mpaka mjengoni na mafisadi waliokuwa wakinunua watu kama nanii ndio wanatusumbuwa taifa..
Kama Rais nadhani we have to do some thing ikiwa bwawa limekuwa na mamba wakali nahawezekani kufugika na mji umekuwa taharuki kutokana na mamba hawa u have only one option hatuwezi kuendelea kuliwa na Mamba mamba ambaye mfugaji ni sisi....
Nilazima wajuwe serikali imesimama imara kuyapita mapito haya hakuna nin wala nin rushwa inalitesa hili taifa na ndio hawa hawa wanatumia mabilion yetu kuhonga wananchi wamchukie rais na kumbambika kila aina ya ubaya...
 
Haya ndio mambo yanayofanya Rais JPM kuchukiwa
1. Kuhamasisha ulipaji kodi kwa vitendo na kujitegemea.

2. Kuhamasisha watanzania kufanya kazi zilizo na tija kwa taifa.

3. Kupinga ubadhirifu wa mali, ufisadi, na uzembe makazini.

4. Kupiga marufuku siasa zisizokuwa na tija kwa taifa.

5. Kuboresha miundombinu ya nchi kama barabara, reli, viwanja vya ndege, mashule n.k

6. Kudhibiti uwizi wa mali za uma kama madini, mafuta na pia kupitia upya mikataba yote ya hovyo iliyoingiwa na viongozi wenye tamaa.

7. Kupiga vita uuzwaji na matumizi ya madawa ya kulevya kwa vitendo.

8. Kuhamasisha Ujenzi wa viwanda sababu ndio msingi wa uchumi wa nchi yeyote ile duniani.

9. Kupiga vita kwa vitendo ujangili na uharibifu wa nyara za serikali nchini kwote.

10. Kuwahamasisha watanzania kufanya kazi na kuwa na nidhamu katika matumizi ya ela.

Haya ni mambo machache yanayofanywa na Rais JPM yanayoleta yeye kuchukiwa na wahusika wa hayo mambo.
Hivyo kama wewe ni mmoja wa unayofanya hayo mambo lazima utamchukia Rais JPM.

In Our Time Let Us Do Good

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umofia kwenu wadau,

Nawaza na kuwaza na kufikiria na kuangalia listi ya wale wanaojidai kubeza juhudi, weledi na uaminifu wa Dkt Magufuli ktk taifa letu la Tanzania.

Nawaza na kufikiria jinsi alivyoweza kurudisha matumaini yetu watanzania.

Nawaza na kufikiria alivyoikemea rushwa na uzembe kazini na kusisitiza watu tufanye kazi tuache kubweteka.

Nafikiria na kuwaza jinsi ambavyo ameweza kuwakemea wazungu na kuwalazimisha waje meza ya mazungumzo ili kubadili makubaliano ya mikataba ili nchi nayo inemeeke utajiri wake.

Nafikiria fikiria jinsi ambavyo Dkt Magufuli alivyo weza kufanya yale ambayo wazungu wamekuwa wakitutukana kuwa viongozi afrika ni wala rushwa, wazembe na wapenda starehe, si wawajibikaji, wana matumizi makubwa.

Yaani nikiwaza sana nauona mkono wa Mungu aliye mkuu, na nina uhakika Tz baada mpaka 2025 chini ya Dkt Magufuli itakuwa yenye neema teke!

Mungu Mbariki Dkt Magufuli, Mungu Ibariki CCM, Mungu Ibariki Tanzania!
 
SIJAWAHI KUONA MTU ANASHINDWA KUMSIFIA MKEWE HADHARANI HATA KAMA NI MBAYA
 
Back
Top Bottom