Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

tutampima kwa matokeo kama vifaa vya kutosha mahospitalini, madawa ya kutosha, wafanyakazi wa kutosha hasa elimu na afya, vitendea kazi vya kutosha mashuleni, wanafunzi wenye sifa elimu ya juu wote wanapata mikopo, barabara nzuri, maji salama, umeme wa uhakika, uchumi wa mtu mmoja mmoja umekua n.k hatutampima kwa ziara maofisini
Kweli yetu macho
 
Ziara za magufuli na maagizo makali havikuwa vitu vipya kwangu kwani ata Mjomba alikuwa hivyohivyo.

namuona Raisi wangu anafanya maamuzi. Bila kujari yuko sahihi kiasi gani kwani ni bora kufanya maamuzi ukakosolewa na wachache kuliko kuogopa kufanya uamuzi. Ameanza kuikata kiu ya maamuzi magumu niliyoitamani kutoka kwa Lowassa.

Nashauri baada ya kuunda balaza la mawaziri Raisi wangu awapangie majukumu mazito mawaziri wake na awasisitize wawe wepesi kufanya maamuzi juu ya wizara zao na kuweka utaratibu utakaowezesha kujua na kusimamia hadi ngazi za chini kabisa ya idara zao.

Mfano waziri wa fedha aweze kuwajibishwa kwa kushindwa kuchukua hatua kwa ubadhilifu kwenye halimashauri

Au waziri wa elimu aweze kuwajubishwa kwa utoro na uzembe unaofanywa na walimu shuleni

Au Waziri wa afya awajibishwe kwa miji kujaa taka kila kona .

Hii inamaana kubwa sana hawezekani raisi agundue uozo mkubwa kwenye idara chini ya wizara unayoongozwa na waziri fulani na kuchukua hatua alafu waziri abaki salama. Waziri anasimamia wizara moja tu wakati raisi anaangalia wizara zaidi ya kumi na tano.

Hivyo hivyo waziri akigundua uozo kwenye idara iliyo chini yake sana mfano waziri wa elimu agundue shule fulani walimu hawahudhurii shuleni kabisa anatakiwa amwajibishe mkurugenzi na afisa elimu kwa tukio hilo kwani haiwezekani waziri agundue uozo chini alafu mkurugenz abaki salama wakati waziri anaangalia Tanzania nzima na mkurugenzi anaangalia halimashauri moja tu.

Pia mkurugenzi adili na wakuu wa shule.

Hivyo basi Rais wa ngu ukikuta uozo dili na mawaziri tu mawaziri ndio watajipanga, Na waziri wa kwanza kumfukuza hiyo wizara yake uisimamie wewe kwa muda ili mawaziri waone mfano.
Amejenga viwanda nchi nzima na mikopo kila mwanafunzi ni 100%
 
V
Binafsi nimefurahishwa na kasi ya Dkt. Magufuli. Naamini wapo pia wengi wanaoungana nami katika furaha hii. Magufuli ameanza kwa kasi ambayo kama ataimaintain, Tanzania haimalizi miaka mitano itakuwa tayari ni nchi yenye kipato cha kati.

Hata hivyo wapo baadhi yetu ambao wanakejeli kasi hiyo. Hao kwangu ni watu waliozoea ubwete na bora liende!. Wanamwona Magufuli kuwa ni mtu atakayekuwa kauzibe kwao!

Wapigaji wote, wavivu wote na wazee Wa madili wote watamchukia Magufuli ila mi niseme na niwaombe tu kwamba tumpe support huyu jamaa kiukweli atatufikisha mahali Fulani!

Tuwafichue wote wanapanga kumhujumu (najua wanajulikana), tuwakatae kwani hawana nia njema na taifa letu.
IPO BADO UNASEMA MANENOO HAYA HAHAHA UKUTE ULIFURUMUSHWA KWA CHETI FEKI😱😱😱😱
 
*UKIPATA NAFASI POPOTE PALE .... ONGEA HAYA KUHUSU RAIS WAKO JPM*
( _kuwa Mzalendo_)

1. *JPM amerejesha nidhamu ya fedha habari za kutumia fedha kuleta ubabe hakuna, maneno nitakupiga nikulipe imebaki historia.*

2. *JPM amerejesha nidhamu kwenye ofisi za umma, tabia za watumishi wa umma kujimilikisha ofisi za umma imebaki historia, kauli toka ofisini kwangu, nipo ofisini tumezisahau.*

3. *JPM amekomesha tabia ya wanaCCM kadhaa kutumia chama kama mwamvuli wa kukopa kodi, kupiga madili na kuleta ubabe mtaani.*

4. *JPM amekomesha mtandao wa kupeana vyeo serikali, tabia ya kutumia watu na pesa kupata nafasi serikali imepotea rasmi*.

5. *JPM amefanya vizuri kwenye sekta ya miundombinu na usafirishaji , amethubutu kufanya mambo mazito kwenye reli, barabara, anga, nk*

6. *Kupitia JPM sasa uongozi ni kutumikia watu siyo kuvuma pesa kama ilivyokuwa sasa wabunge, madiwani, mawaziri, nk wanaishi kama viongozi siyo wafanyabiashara , kufikia 2020 wanasiasa wafanyabiashara watajiweka pembeni.*

7. *Kupitia JPM viongozi wamekuwa wasikivu kwa wananch, tabia ya viongozi hasa wanasiasa kujiona miungu imebaki historia.*

8. *JPM amevunja mwiko wa tabia ya kudhani watu fulani wa familia ndiyo special kuteuliwa ktk nafasi za kiserikali, kupitia JPM kupata uteuzi ni uwezo siyo historia ya familia*.

9. *JPM amethubutu kutazama utapeli tunaofanyiwa kwenye sekta ya madini, angalau ameunda tume kuchunguza usafirishaji wa Udongo kwenda ughaibuni hili siyo japo la mzaha.*

10. *JPM amekomesha ujangili sasa matukio ya ujangili yamepotea kabla Tanzania ilikuwa inakwenda kupoteza tembo na Wanyama wengine muhimu sasa Wanyama wetu wapo salama.*

11. *JPM amekomesha matumizi ya hovyo ya kodi zetu , semina za kulipana fedha hovyo hakuna, safari za kutengeneza kupiga pesa hakuna, manunuzi ya kisanii hakuna , kipindi hiki viongozi na watendaji wa serikali wanaheshimu kodi zetu.*

12. *JPM amethubutu kupambana na dawa za kulevya kwa vitendo hili siyo jambo dogo ukizingatia nguvu ya wauza dawa za kulevya.*

13. *JPM ameendeleza vema vita dhidi ya rushwa kuanzia kwenye chama (CCM) mpaka Taasisi za serikali , siyo jambo dogo kukomesha rushwa kwenye siasa zetu za Afrika yeye ameonesha njia kwenye uchaguzi wa wabunge wa EAL.*

14. *JPM amekomesha mtandao wa ufisadi BANDARINI enzi hizo bandari yetu ilikuwa chimbo la kujipatia utajiri wa kifisadi sasa BANDARINI amesafisha.*

15. *JPM amekomesha tabia ya viongozi kupeana tenda za serikali kihuni na kifisadi, kandarasi sasa zinatolewa kwa kufuata utaratibu kiasi cha kupunguza ufisadi kwenye halmashauri zetu.*

16. *JPM amerejesha uadilifu kwenye sekta ya afya, pamoja na changamoto za uhaba wa dawa, wataalam wa afya na vifaa angalau madaktari na wauguzi wana kauli nzuri zenye faraja kwa wagonjwa hata rushwa sekta ya afya siyo kama enzi zile.*

17. *JPM ameleta utaratibu mzuri wa viongozi kutoka ofisini kwenda mtaani kutazama matatizo ya wananch kuliko Kutegeana kusoma ripoti tu.*

18. *JPM amerejesha thamani ya elimu kwa kuteua wasomi ktk nafasi mbali mbali kuliko awali watu waliteuliwa kwa mazoea, sasa maprofesa, madaktari na wasomi kwa ujumla ndiyo viongozi wa wizara zetu*

19. *JPM amekomesha mtandao wa makundi kwenye chama na serikali sasa mtandao wa kupeana ukurugenzi wa halmashauri, UDC, URC, ukatibu wa chama, ukurugenzi wa mashirika ya umma umepotezwa hili siyo jambo dogo.*

*20. JPM amekomesha matapeli wenye mwamvuli wa uwekezaji waliojimilikisha ardhi kubwa nchini huku watanzania wakikosa maeneo ya kulima.*

_Tanzania ni yetu_
_Magufuli ni presdent wetu
 
"Ni malaika sio binadamu".Hivyo ndiyo mtu mwenye akili timamu anavyoweza kum-describe Rais Magufuli..

Anafanya mambo ambayo hata Mwalimu Nyerere alishindwa; kwa mfano Mwalimu aliposhindwa kupambana na wanyonyaji wa madini yetu hapa nchini na kuamua kuacha migodi bila kuchimbwa hadi waTz tutakapopata akili.

Lakini Rais Magufuli anataka kupambana nao huku akiweka options mbili aidha wakubali masharti yetu waendelee kuchimba ama waondoke yachimbwe na wananchi wa kawaida.

Watanzania wenzangu tumuunge mkono malaika huyu.. NI bahati na huja mara moja ndani ya miaka 50..
 
Binafsi nimefurahishwa na kasi ya Dkt. Magufuli. Naamini wapo pia wengi wanaoungana nami katika furaha hii. Magufuli ameanza kwa kasi ambayo kama ataimaintain, Tanzania haimalizi miaka mitano itakuwa tayari ni nchi yenye kipato cha kati.

Hata hivyo wapo baadhi yetu ambao wanakejeli kasi hiyo. Hao kwangu ni watu waliozoea ubwete na bora liende!. Wanamwona Magufuli kuwa ni mtu atakayekuwa kauzibe kwao!

Wapigaji wote, wavivu wote na wazee Wa madili wote watamchukia Magufuli ila mi niseme na niwaombe tu kwamba tumpe support huyu jamaa kiukweli atatufikisha mahali Fulani!

Tuwafichue wote wanapanga kumhujumu (najua wanajulikana), tuwakatae kwani hawana nia njema na taifa letu.
Hata Azrael (Azrail; Malak al-maut) ni malaika pia..
 
"Ni malaika sio binadamu".Hivyo ndiyo mtu mwenye akili timamu anavyoweza kum-describe Rais Magufuli..

Anafanya mambo ambayo hata Mwalimu Nyerere alishindwa; kwa mfano Mwalimu aliposhindwa kupambana na wanyonyaji wa madini yetu hapa nchini na kuamua kuacha migodi bila kuchimbwa hadi waTz tutakapopata akili.

Lakini Rais Magufuli anataka kupambana nao huku akiweka options mbili aidha wakubali masharti yetu waendelee kuchimba ama waondoke yachimbwe na wananchi wa kawaida.

Watanzania wenzangu tumuunge mkono malaika huyu.. NI bahati na huja mara moja ndani ya miaka 50..

Teh teh teh....mkuu you are extremely naive Maskini!!

***Neeeeeeeeeeeext......................
 
Taifa lilikuwa limefikia pabaya kwa kuongezeka kwa magonjwa ya tabia baada ya wewe kuingia madarakani yafuatayo yametokea
1. Ule utaratibu wa kukodi bodaboda kwenda mtaa wa pili sasa umekufa kwa watu wengi, wameamua kutembea (kufanya mazoezi) na ni faida kiafya.
2. Mafuta ya kupikia sasa yanawekwa kidogo sana kwenye vyakula hivyo kupunguza hatari ya magonjwa ya moyo.
3. Mboga mboga, nafaka zisizo kobolewa, mazao jamii ya kunde na mimea mingine imekuwa chakula kikuu cha wengi ndomaana miili ya wengi imenawiri japo wanalia njaa.
4. Sukari inatumika kidogo sana kama kanuni zinavyoelekeza.
Kwakweli kwenye afya za watanzania wengi umesaidia kuokoa.
Hongera.
 
Mtakufa masikini tena kama ww ndo kiongozi wa ukoo wenu utawafanya wenzio wafe masikini kwa mawazo yako ya kimasikini
 
Taifa lilikuwa limefikia pabaya kwa kuongezeka kwa magonjwa ya tabia baada ya wewe kuingia madarakani yafuatayo yametokea
1. Ule utaratibu wa kukodi bodaboda kwenda mtaa wa pili sasa umekufa kwa watu wengi, wameamua kutembea (kufanya mazoezi) na ni faida kiafya.
2. Mafuta ya kupikia sasa yanawekwa kidogo sana kwenye vyakula hivyo kupunguza hatari ya magonjwa ya moyo.
3. Mboga mboga, nafaka zisizo kobolewa, mazao jamii ya kunde na mimea mingine imekuwa chakula kikuu cha wengi ndomaana miili ya wengi imenawiri japo wanalia njaa.
4. Sukari inatumika kidogo sana kama kanuni zinavyoelekeza.
Kwakweli kwenye afya za watanzania wengi umesaidia kuokoa.
Hongera.

UNA SPIRIT OF POVERTY.

unaroho ya umaskini.
 
Back
Top Bottom